Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,873
Mmoja wa wabunge waliotajwa kwenye taarifa ya Kamati Teule ya Bunge anatarajiwa kujibu hoja zilizoelekezwa kwake na Kamati hiyo kwa kuleta taarifa "tofauti" ya Richmond ambayo anaamini ndiyo iliyokuwa sahihi. Mbunge huyo anadai kuwa "kama kuna ripoti mbili za Richmond mbona moja haitutaji mimi na EL lakini hii nyingine inatutaja".
Mbunge huyo anatarajiwa kuja na utetezi huo hasa baada ya kutakiwa na Bunge kuelezea madai yake kuwa ripoti iliyosomwa Bungeni na Mwakyembe "siyo yenyewe imebadilishwa" akiashiria kwamba yeye mwenyewe alikuwa ameipata ripoti hiyo kabla ya kuletwa Bungeni na alijua kilichomo.
Baada ya kampeni ya kusafishana magazetini kuingia kasoro baada ya siri ya kuundwa kwa "Agenda 21 kuwekwa hadharani na sasa inaonekana wameamua kwenda moja kwa moja Bungeni. Kwa vile mpango wao huo nao unafunuliwa siku chache kabla ya kikao cha Bunge kukutana kuna uwezekano mbunge huyo kuamua kuomba radhi kwa kauli yake ya Bungeni na kuamua "kufa kisabuni".
Hadi hivi sasa, inadaiwa bado kuna mgongano mkubwa kati ya viongozi wa CCM kiasi kwamba baadhi ya viongozi wa juu hawakuzungumza kwenye mkutano wao Richmond. Kama kampeni hiyo ya kumsafisha EL na Mbunge huyo itafanikiwa na kama itaonekana kuwa ripoti iliyosomwa Bungeni siyo "yenyewe" basi kuna wezekano wa Bunge kumuomba radhi Lowassa na Mbunge huyo.
Hata hivyo, kwa upande wao wajumbe wa kamati teule na wenyewe inasadikiwa kuwa wamejipanga vizuri kujibu mashambulizi yoyote dhidi yao na imesemwa kuwa Mbunge huyo anayetaka kuja na "ripoti nyingine" ya Richmond ajiandae kupata kibano cha kukumbukwa.
Wakati huo huo, uongozi wa Chama cha CUF kinatarajiwa kukutana kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kuelezea msimamo wao baada ya kusikia maelezo ya CCM kuhusu muafaka. Kuna dalili kuwa chama hicho kitatoa muda maalum kwa serikali ya Rais Kikwete na baada ya hapo kuanza kuingia "mitaani" kwa njia ya maandamano. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika saa nane mchana saa za Afrika ya Mashariki.