Elections 2010 Bunge kuendeshwa bila kufuata kanuni za Bunge?

Paul J

Senior Member
Oct 25, 2010
193
62
Sofia Simba kupita bila kupigiwa kura wala kuhojiwa kuwa Mbunge wa SADC ilikuwa sahihi?

Ndungai anasema Mnyika alikuwa sahihi kulingana na kifungu cha 5 (2c) cha kanuni za bunge lakini alichelewa kutoa hoja na Spika wa Bunge, Anna Makinda ndiye aliyeanza mchakato wa uchaguzi kabla ya kumuachia kiti hicho. Kwa ukiukwakaji wa Kanuni za Bunge mwanzoni tu mwa Bunge unattupa picha gani waku kuhusu umakini wa Anna Makinda kuliongoza Bunge letu tukufu na uzoefu wake wa kuwa Bungeni tangia 1975 hadi leo hii?

Source Tanzania Daima (CHADEMA yamwadhiri Ndungai)
 
sofia simba kupita bila kupigiwa kura wala kuhojiwa kuwa mbunge wa sadc ilikuwa sahihi?

ndungai anasema mnyika alikuwa sahihi kulingana na kifungu cha 5 (2c) cha kanuni za bunge lakini alichelewa kutoa hoja na spika wa bunge, anna makinda ndiye aliyeanza mchakato wa uchaguzi kabla ya kumuachia kiti hicho. Kwa ukiukwakaji wa kanuni za bunge mwanzoni tu mwa bunge unattupa picha gani waku kuhusu umakini wa anna makinda kuliongoza bunge letu tukufu na uzoefu wake wa kuwa bungeni tangia 1975 hadi leo hii?

source tanzania daima (chadema yamwadhiri ndungai)


wote mavi kanyaga mpaka raisi wao
 
Ahadi ya 1 ilikuwa Bunge litaendeshwa kwa kanuni imekuwa je tena ; nadhani bado anazisoma kanuni baada ya miezi 6 atakuwa ameziweka kwenye permanent memory yake .
 
Tuendelee kuona vituko mwaka huu. Nadhani kanuni ni vitu vya kuvielewa siyo vitu vya kukurupuka navyo kama anavyofanya Makinda. Safari hii Bunge la Tanzania litaaibisha nchi yetu kwa watu wa nje.
 
Hawa Jamaa wa CCM hawajui kanuni hata kidogo wanatumia mabavu tu hawana jipya hata kidogo.

2015 lazima tuwamwage.
 
Kama ameshindwa kuzielewa tangia mwaka 1975-2010 unadhani zitaingia tena kichwani? Ataendeshwa na remote kutoka Ikulu! Subirini mtaona vijimambo bungeni Sita ataamka sana kumfuata mwanasheria mkuu ama Makinda mwenyewe na muda wa Bunge huenda ukawa mrefu zaidi ama hoja nyingi zitakuwa zinazimwa kimababe kwa kuzidi kuvunja kanuni za Bunge! Hoops tutaongelea wapi wajamani? Kama Bunge nalo limetekwa?
 
Jamani muoneeni huruma kwani hili bunge la kumi atakuwa anajifunza kanuni na uzoefu then bunge la kumi na moja atawaomba tena wamchague ilibunge liwe bora kwani atakuwa ameshazifahamu kanuni za Bunge. hata mkuu wa kaya alisema miaka mitano ya kwanza alikuwa anatafuta uzoefu.
 
Huyu mama hakuna kitu kabisa. Bora km ni mwanamke wangemchagua Anna Abdalah kwani yeye anao uwezo mkubwa kiutendaji na confidence sio huyu. Dont expect any changes kwani alikuwa hivi tangu bunge lililopita so no changes. Kuhusu Simba, huyo ndo aliyeingiza hoja ya kuchagua wanawake watupu and she was against Sitta, kwa hiyo mafisadi wanajua what they are doing with her. Kwani kwa mujibu wa Mwanahalisi la jana, majina yaliyopitishwa na kamati kuu kabla ya kuletwa kwenye CC, yaliuwa ni Sitta, Anna makinda & Anna Abdallah, ila hapo ndo moto wa watu wa Rostam akiwemo Makamba ulipowaka baada ya kuoan jina la Sitta na huyu mama akakomaa sana.Huoni Kinana kajitoa kwenye haya mambo?? Yeye alitaka Sitta aendelee kuwa spika na ht Membe, Nchiligati wote walikuwa kwa Sitta.
 
Sisiemu wamekalia kuti kavu!!!!!!!!!!!!!!!!!! Wabunge front liners wa CDM ni ma-advocates, wao haya mabishano ya vipengele vya sheria ndiyo ujira wao-kazi ya kila siku-wanaenjoi !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mhe Mabere Marando wakati wa kampeni kwa kiti cha spika alitahadharisha bunge kuwa spika awe mwanasheri kama alivyokuwa Mr 6 ili kumsaida katika majukumu yake ya kila siku.Lkn Mhe. Spika na Naibu wake wote ni mazuzu wa sheria (Spika=utaalam wa fedha; Naibu=elimu ya mimea UDM). Sasa kama mapema namna hii tu kabla ya vikao vya bunge kuanza vya kujadili mambo magumu kuelewa/kutetea/kupinga kwa mujibu wa kanuni za bunge, kambi ya sisemu itapata shida kweli kweli!!!!!!!!! Sisiemu wamezoea vya kunyonga, ni wazi vya kuchinja vitawapa shida sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom