BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Bunge kielelezo cha ukuaji wa demokrasia -Sitta
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,September 16, 2008 @00:03
Spika wa Bunge, Samuel Sitta amesema Bunge litaendelea kuwa kielelezo cha ukuaji wa demokrasia nchini, hasa baada ya kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha hamasa kwa wananchi kufuatilia uendeshaji wa shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria.
Sitta alisema ongezeko la hamasa ya wananchi kufuatilia mijadala bungeni ni matokeo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Bunge kwa kipindi cha mwaka 2008-2013 pamoja na mabadiliko ya Kanuni za Kudumu za Bunge.
Akitoa salamu zake kwa niaba ya wabunge nchini katika kuadhimisha Siku ya Demokrasia Duniani jana, Sitta alisema moja ya mabadiliko ambayo yamepanua upeo wa demokrasia ndani ya Bunge na kuwa mfano wa kuigwa na mabunge mengine ni utaratibu wa maswali ya papo kwa hapo ya Waziri Mkuu.
Alisema maswali hayo ya kila wiki katika kikao cha Alhamisi, Waziri Mkuu huulizwa maswali kadhaa ya moja kwa moja bila kuyaona ambapo majibu ya Waziri Mkuu hutoa picha ya namna serikali inavyoshughulikia kero na matatizo ya wananchi.
Sitta alisema hatua hiyo ni muhimu kwa ukuaji wa demokrasia ambapo nafasi ya upinzani imesaidia kuleta changamoto mpya katika mijadala bungeni na hotuba zenye changamoto, hivyo serikali kuwa makini katika kufuata misingi ya utawala bora na kurekebisha sheria zenye upungufu.
Spika alivipongeza vyombo vya habari ambavyo ni wadau wakuu wa demokrasia nchini kwa kuwa mstari wa mbele kukemea maovu na kuwataka wamiliki wa vyombo hivyo kuwaongezea ujuzi waandishi wa habari ili wafanye kazi yao vizuri zaidi na kutoa mchango katika kukua kwa demokrasia nchini.