Kimsingi bunge hili limeshindwa kutekeleza majukumu/wajibu wake. Hiki ndicho chanzo kikuu cha bunge kutoheshimika, kudharauliwa, hata kunyooshewa vidole na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na serikali kutozingatia yanayoamuliwa na bunge. Madhalani, huwezi pita barabarani ukatukanwa au ukazomewa na mtu asiyekujua kama hujafanya jambo lolote la kipuuzi lisilokubalika na jamii husika. Inawezekana hata rais hazingatii maamuzi ya bunge kwa sababu anajua maamuzi hayo hufikiwa kwa kukosa weledi, utashi na busara.
Wabunge wenyewe hawajui wajibu wao, wabunge wenyewe hawajitambui, wabunge wenyewe uchama umewajaa, wabunge wenyewe hawawakilishi hata hoja za jamii, wabunge wenyewe bendera fuata upepo, wabunge wenyewe hawatofautiani kwa hoja za msingi na wabunge wenyewe wanapangiwa cha kusema kama watoto.
Kama vile wengi wanavyopendekeza timu ya taifa isishiriki michuano ya kimataifa kwa miaka hata 5 ijipange kwanza kwa sababu ya udhaifu. Bunge hili lifutwe tu mpaka watanzania tutakapo jitambua ndipo lianze tena.