Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Tunahitaji katiba na sheria zinazoeleweka siyo huruma na bla bla ili watu wanaojipendekeza kama wewe waonekane na kupewa teuzi. Watanzania tumeona kwa macho uchaguzi ulivyokuwa.

Bashiru alisema wazi kuwa CCM itatumia dola kubaki madarakani na wametumia tayari.

Mpinzani yeyote atakayekubali teuzi siyo Mpinzani bali anaangalia tumbo na kusaliti watanzania.
Jibu unalo ww mwenyewe juu ya point yako
 
Nilipenda sana makala na hoja zake zikigusa maeneo mengi. Leo ni upande mmoja tu kusifia.
Nikiona makala yake huwa nasoma tu kichwa naishia.
Mkuu Mzamifu, karibu katika makala hii, uangalie jinsi ninavyosifu!.
P
 
Hoja ni nzuri katika mukhtadha wake,ila utekelezaji wake ni mgumu kutokana mbinu na mikakati iliyotumika kupata ushindi wa kimbunga.Wanamikakati wamezidisha mno ushindi wao kiasi cha kushtukiwa kuwa walifanya udanganyifu.Hizo nafasi kumi wakipewa wapinzani ili wakaunde kambi rasmi ya upinzani bungeni itapendeza zaidi.Hao waliotajwa kwa mtazamo wa kawaida ni ngumu,labda mbatia na sendiga,lakini wale miamba ni maajabu ya kisiasa kuteuliwa na kukubali uteuzi huo
 
Hakuna cha hoja nzuri hapa, nyie mulichafua uchaguzi na kuutia najisi na kujikwalia ushindi fake na kuihadaa dunia kwamba mmeshinda kwa kishondo na huku dunia nzima inajua mlichofanya, na zaidi ya yote mulikuwa tayari hata kuua ili tu mhakikishe mmepata kazi hizo za dhuruma.
Siasa mmeifanya ni ajira na ndo kinacho wasumbua,hamtumiki kwa masirahi ya taifa ila kwa ajiri ya matumbo yenu na familia zenu, kaene bungeni sasa peke yenu mjadili yote munayoweza na sisi watanzania tunawatazama na tutalipa kodi kama kawaida mfanye munayoyataka.Hata mkae mywe bia bungeni sisi hatusemi mana hatukuwachagua watu kama nyie, atasema aliewapeleka hapo kwa dhamira yake.
 
Mimi nakosa imani kabisa na bunge hili la kumi na mbili tunapoteza uimala wa muhimili huu muhimu katika nchi wapo wananchi wenye imani na upinzani kwa kiasi kikubwa kutokana na hoja za msingi na mchango wao katika maendeleo, kama tunataka kujenga umoja wa kitaifa jitihada za wakina zitto kabwe sio za kupuuzwa hata kidogo he done so much for us, kumbukeni maswala ya escrow, epa Richmond namna wapinzani walivopigania mali hizi za umma. Kukosa upinzani tunapoteza uwajibikaji na uwazi kwa kiasi kikubwa, the decision taken by taking into account deontological point of view by taking the action as the end and not the means but under teleological we have to consider the consequences of our actions to the public interest
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, Bunge letu jipya linalokwenda kuundwa hivi karibuni baada ya uchaguzi Mkuu, lina hali mbaya sana ya kuwa liko kwenye hati hati ya kutokuwepo kwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni.

Swali ni Jee NEC, Rais Dr. Mwinyi na Rais Dr. Magufuli wataingia huruma na kuokoa jahazi kwa kuliokoa Bunge letu la JMT ili liweze kuwa na kambi rasmi ya upinzani Bungeni?.

Declaration of Interest
Japo mimi ni kada wa chama cha siasa, na uchaguzi umekwisha, sasa narejea kwenye zile safu zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo zinatanguliza uzalendo kwa maslahi ya taifa letu Tanzania, hivyo nakuomba unisome with clear conscious kama mnamsoma Mtanzania mwingine yoyote, lakini kama tayari umeisha ni lebo mimi ni kada na kujiambia kila ninachoandika ni kwa maslahi ya chama changu na sio maslahi ya taifa, nakushauri uishie hapa, maana hata ukiendelea kunisoma with pre conceived opinion, hautaweza kuiona rationale ya bandiko hili.

Na kwa vile hili ndilo bandiko langu la kwanza Jukwaa la Siasa baada ya Uchaguzi, naomba kuchukua fursa hii kumpongeza Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa ushindi wa kishindo, nakipongeza Chama changu CCM, na kupongeza wote waliodhinda.

Japo ni lengo la kila mwana CCM, kuona chama chake kinashinda viti vyote na kata zote, ila pia kuna baadhi ya wana CCM, ambao ni makada wazalendo zaidi, wamefurahishwa na ushindi wa kishindo wa CCM, ila pia ni wazalendo zaidi kwa nchi kuliko chama, tungependa kuona wapinzani makini wachache wakiingia Bungeni ili kujenga ile dhana ya Bunge la vyama vingi. Hivyo kushindwa kwa mtu kama Zitto ni masikitiko kwa wana CCM wazalendo wengi wa type yangu!. Tunapenda Bunge la CCM, lakini pia lenye mwamko na msisimko wa challenges za upinzani.

Hivyo kwenye kushangilia ushindi, nawasihi viongozi wetu na wana CCM wazalendo wenzangu, tushangilie kwa kiasi, tusiwatambie upinzani, tusiwakejeli, kuwatukana wala kuwabeza, kwasababu nao ni Watanzania wenzetu na wamechaguliwa na Watanzania, ila kura zao hazikutosha, hivyo kwenye hotuba zetu, tupunguze kujimwambafy na badala yake tuongeze humility na kuhutubia hotuba za upendo ku heal na sio za ku hurts ili kuliponya taifa na machungu ya kushindwa na kuliunganisha taifa tuwe na upendo, umoja, mshikamano na ushirikiano kuijenga nchi yetu.

Wapinzani
Asiyekubali kushindwa sio mshindani, uchaguzi umekwisha, aliyeshinda ameshinda kwa haki na kihalali, aliyeshindwa ameshindwa kwa haki na kihalali, kwa kutumia kanuni ya " the end justifies the means", tukubali matokeo, kazi sasa ibaki ni moja tuu, kuijenga nchi yetu kwa kutoa kila aina ya ushirikiano kwa washindi.

Vitabu vya dini zote vinafundisha Wananchi kutii mamlaka halali. Baada ya uchaguzi kumalizika na rais kupatikana na kuapishwa, kile kitendo cha kuapishwa ni kumhalalisha rasmi hivyo baada ya rais Magufuli kuapishwa, sasa yeye ni mamlaka halali, ndiye rais wa JMT, ni rais wa Watanzania wote, waliomchagua, wasio mchagua, hata ambao hawakupiga kura, rais Magufuli ndiye rais wa nchi, tutii mamlaka halali.

Baada ya kuapishwa na kuanza kazi, hakuna kitu kinachoitwa kususa, kutokubali matokeo au kutomtambua rais, huko ni kujifurahisha tuu, kwa sababu tayari rais yupo na ana exist, umtambue, usimtambue, yeye ndio rais wako na yupo kwa ajili yako. Unaweza usimpende, unaweza usimkubali, lakini huwezi kutomtambua!. Hivyo viongozi wa upinzani acheni hadaa za kuwahadaa wafuasi wenu kuwa hamumtambui rais. Rais ni mtu mwenye status of duality.

1. Rais Magufuli ni mtu, ni binadamu, unaweza usimpende, usimkubali na ukakataa kutambua ushindi wake, that is human, kama humpendi mtu, hakuna anayeweza kukulazimisha umpende au umkubali, hilo una uhuru nalo.

2. Rais Magufuli ni Taasisi ya urais, president institution, hii ni mamlaka, hakuna choice ya kuipenda, kuikubali au kuitambua, ipo kisheria hivyo ni lazima uiheshimu, na kuitii mamlaka hii, it's not a matter of choice, its an obligation, ni lazima kuitii mamlaka na usipotii, mamlaka inakushughulikia, ndio maana hata sheria, kutokujua jambo fulani ni kosa kisheria, is not an excuse sheria isi act on you, hivyo hakuna kitu kinachoitwa kutokumtambua rais.

Huo ulikuwa ni utangulizi tuu kuwekana sawa, mada ya leo ni hii.
Kufuatia poor performance ya vyama vya upinzani kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, kwa Watanzania kuvikataa na badala yake kukichagua CCM pekee, but 4!, idadi hiyo haiwezi kutimiza akidi inayotakiwa kuweza kuunda kambi rasmi ya upinzani Bungeni.

Ibara ya 14 ya Kanuni za Bunge zinaeleza
2) Wabunge wote wa Upinzani wanaweza kuunda Kambi Rasmi ya Upinzani iwapo idadi yao itakuwa si chini ya asilimia kumi na mbili na nusu ya Wabunge wote.
(3) Chama cha Upinzani hakitakuwa na haki ya kuchagua Kiongozi wa Upinzani Bungeni, isipokuwa tu kama kina idadi ya Wabunge wasiopungua asilimia kumi na mbili na nusu ya Wabunge wote.

Idadi ya Wabunge wote wa Bunge la JMT ni 357, hivyo asilimia 12.5% ni wabunge 44.

Kwa matokeo ya uchaguzi huu, hata baada ya allocation ya wabunge wa viti maalum, idadi hiyo haiwezi kufikiwa, hivyo Bunge lijalo, lina hati hati ya kutokuwa na kambi ya upinzani Bungeni, kambi hii ikikosekana, maana yake, hakutakuwa na serikali kivuli, hivyo bajeti za serikali tuu zitawasilishwa bila maoni ya kambi ya upinzani, jambo ambalo is not healthy kwa Bunge la vyama vingi.

Watu watatu pekee wenye uwezo wa kuokoa jahazi hili, ni
1. Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ikubali kutoa nafasi ya upendeleo kwa viti maalum vya upinzani hata kama hawakukidhi vingezo.
Mfano, maadam sifa ya kupata viti maalum ni chama kupata asilimia 10 ya kura zote, then Tume inaweza kuamua, wale wagombea urais wote waliopata kura zaidi ya asilimia 10%, wote waingie Bungeni.

2. Rais wa Zanzibar, anazo nafasi 10 za uteuzi wa wawakilishi, katika nafasi hizo zote 10, ateue wawakilishi 10 wa vyama vya upinzani, kati ya hao 10, wawakilishi 5, waingie kwenye GNU, na wawakilishi 5 waingie kwenye Bunge la JMT toka Baraza la Wawakilishi. This is a very big sacrifice to make.

3. Rais wa JMT, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na yeye ana nafasi zake za uteuzi wa wabunge 10. Usually lengo la uteuzi huu ni ili rais aweze kupata watu wa kutosha kumsaidia, kwa kuwa mawaziri, lakini kwa line up ya walioshinda CCM, kuna line up ya kushibisha mawaziri wote, na bado akabakiwa na reserve team inayoweza kuunda Baraza la Mawaziri la akiba.

Hivyo kama rais Magufuli akiingia huruma, akaamua kuliokoa Bunge letu tukufu, then na yeye ateue angalau wabunge 6 wa upinzani kuingia Bungeni kwenda kuimarisha upinzani, na rais Magufuli anaweza kuitumia kete hii kupiga ndege wawili kwa jiwe moja.
1. Kuuokoa Upinzani 2. To heal the nation from the election wounds ambazo to some ni very painful na kuna watu wako very bitter!.

Kwa ushauri wangu, napendekeza rais Magufuli awateue hawa wafuatao
1. Tundu Lissu- aligombea nae
2. Zitto Kabwe - Most Interactive MP
3. James Mbatia- Very Compromising
4. Prof Haruna Lipumba - Good Puppeteer
5. JJ.MNYIKA- Mjengaji hoja mzuri
Nafasi tano zilizobaki ni za wanawake, tunamuomba Magufuli amuangazie yule Queen Sendiga miongoni mwa wanawake hao.

Hili likifanyika, litatibu makovu ya uchaguzi Mkuu huu, na kuingiza vichwa vya upinzani ambavyo vitalichangamsha Bunge letu na kuliongezea msisimko.

Hili lusipofanyika, Bunge la chama kimoja, bila any challenges, japo litaharakisha maendeleo bila upinzani, litakosa msisimko na lita bore!.

Kwa kumalizia, namalizia kwa lile swali la msingi, kuwa Bunge jipya lina hali mbaya liko kwenye hati hati ya kutokuwepo kambi rasmi ya upinzani Bungeni.

Swali ni Jee NEC, Rais Dr. Mwinyi na Rais Dr. Magufuli wataingia huruma kuliokoa Bunge letu la JMT ili liweze kuwa na kambi rasmi ya upinzani Bungeni?.

Jibu la swali hili, litapatikana ndani ya kipindi cha wiki moja kuanzia Jumatatu Ijayo.

Nawatakia Jumamosi Njema

Paskali
Rejea za Bunge la Chama Kimoja



Ccm wameshashinda, full stop. Hizi sarakasi za kutaka uwepo wa wapinzani bungeni ni danganya toto tu.

Kwani CCM walivyokuwa wanaiba kura hawakujua kuwa wapinzani walitakiwa wawepo bungeni?
 
Tundu Lisu yupi? Huyu ambaye sio raia wa Tanzania? Kesha ukana uraia kwa nini abembelezwe? Hawa wapumbavu wakae huko huko ndiko size yao.

Zito Kabwe yupi? Huyo mnafiki mwenye chama cha mfukoni? Kama umeshindwa kumwelewa huyu mnafiki toka atishiwe maisha yake kule Kenya hutamwelewa kamwe.

CCM ipo imara haina haja ya upinzani Bungeni. Watanzania sio wajinga, watu ambao kila uchwao wanatusengenya tena kwa makuwadi ati ushoga ndio kitu muhimu hapa duniani. P usipotoke.

Wajinga ndio waliwao!!!
 
Inamaana hufahamu au hujui kuwa chairman wako anaongea KILA dakika kuwa "upinzani unatucheleweshea maendeleo,msichague wapinzani sitaleta maendeleo"acha kujitoa UFAHAMU KAKA....LEO MNAWATAKA WAPINZANI WA NINI?

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom