Bunge Jipya: CHADEMA yapaa, CCM yaporomoka!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,
Uchaguzi umeisha, pamoja na kuukosa urais kwa mgombea wa Chadema kwa sababu zozote zile ikiwa ni pamoja na uchakachuaji, lazima tukubali, Chadema inastahili pongezi, na imetingisha kiukweli kweli na sio kutikisa tuu kama walivyodai.

Kutoka viti 4 vya kuchaguliwa bunge lililopita, mpaka viti zaidi ya 20, ni ongezeko la asilimia zaidi ya 500%, huku ni kupaa wakati CCM imeporomoka kwa asilimia kadhaa!.

Wakati mshindi atatangazwa leo, na hakuna ubishi ni mgombea wa CCM, wana CCM wote wenye akili timamu, japo watafurahia ushindi wao, lakini kimoyomoyo, wanajua kwa dhati, ndani ya mioyo yao, Chadema sio chama cha kubezwa ila kama kawaida, mataahira wasio na uelewa wa kweli wa mambo, hawatakosena kuibeza Chadema!.
Sahihisho:
Niliwahesabu Majimbo manne tuu
1.Karatu-Dr.Slaa
2.Kigoma Kasaskazi- Zitto Kabwe
3.Moshi Mjini -Ndesamburo
4.Tarime-Mwera
nikalisahau
5-Mpanda Kati -Arfi

hiyo idadi halisi ni kutoka 5-20 ni ongezeko la Asilimia 400%.
 
Wanabodi,
Uchaguzi umeisha, pamoja na kuukosa urais kwa mgombea wa Chadema kwa sababu zozote zile ikiwa ni pamoja na uchakachuaji, lazima tukubali, Chadema inastahili pongezi, na imetingisha kiukweli kweli na sio kutikisa tuu kama walivyodai.

Kutoka viti 4 vya kuchaguliwa bunge lililopita, mpaka viti zaidi ya 20, ni ongezeko la asilimia zaidi ya 500%, huku ni kupaa wakati CCM imeporomoka kwa asilimia kadhaa!.

Wakati mshindi atatangazwa leo, na hakuna ubishi ni mgombea wa CCM, wana CCM wote wenye akili timamu, japo watafurahia ushindi wao, lakini kimoyomoyo, wanajua kwa dhati, ndani ya mioyo yao, Chadema sio chama cha kubezwa ila kama kawaida, mataahira wasio na uelewa wa kweli wa mambo, hawatakosena kuibeza Chadema!.

Hello Pasco
Nakubaliana nawe, kwangu miye naona kama ushindi huo mkubwa pamoja na jitihada za wote katika kuufanikisha, pongezi nyingi zimwendee Mheshimiwa Dr Slaa, kwangu namuona kashinda pamoja kwamba hatakuwa Raisi lakini umuhimu wake na jitihada zake kwa kushirikiana na wadau wote wamewezesha kufanikisha mabadiliko makubwa katika uchaguzi uliomalizika, ameweza kuwa chachu kubwa na watu wengi wamefaidika na kuwepo kwake katika kinyang'anyiro cha Urais.
 
Nithibitishie kama kweli Chadema watapata hivyo vitimaalum 20 ili nikanywe mbege sasa hivi!
 
Pasco tena ushindi huo wa 500% zingatia umekamata majimbo yenye hadhi kama - Ubungo, Kawe, Ilemela, Nyamagana, Arusha Mjini, Mbeya Mjini, Moshi Mjini - hii inaonyesha kuwa CCM hawakubaliki katika sehemu za mijini ambapo watu wana elimu ya uraia.

JK ataapishwa lakini akumbuke kuwa wananchi zaidi ya 60% toka Dar, Mwanza, Arusha, Mbeya, Moshi na Iringa HAWAMTAKI yeye pamoja na chama chake.

Hii ni challenge kubwa sana kwa CCM hii miaka 5 ijayo. Pongezi zetu za dhati kwa DR. Slaa kwa kazi kubwa sana aliyoifanya akishirikiana na chama chake kwa Ujumla.
 
Baada ya kuona CHADEMA kimepata mafanikio haya najua kila mtu atajifanya mwanachama....MAFISADI wataingia kwa nguvu ndani ya CHADEMA kwani wanajua sasa RUZUKU ya Chama ni kubwa mno baada ya kuongeza majimbo kibao!!!!! Tutegemee migongano na mivurugano kama kawaida yetu ya kutanguliza MASLAHI BINAFSI mbele....!! Wananchi tunashangilia USHINDI viongozi wanashangilia MAPESA ya Ruzuku...Hii ndiyo Tanzania.....
 
Natamani CHADEMA kiwe chama rasmi pinzani bungeni, lakini bila shaka wawashirikishe wenzao kupata upinzani wa nguvu. Je, kwa matokeo ya kura za uraisi na za wabunge ambazo tayari zimeshaonekana, chama gani cha upinzani kinatarajiwa kuwa na wabunge wa viti maalumu vingi, say Chadema , CUF kila chama kinaweza kupata viti vingapi??
 
Wanabodi,
Uchaguzi umeisha, pamoja na kuukosa urais kwa mgombea wa Chadema kwa sababu zozote zile ikiwa ni pamoja na uchakachuaji, lazima tukubali, Chadema inastahili pongezi, na imetingisha kiukweli kweli na sio kutikisa tuu kama walivyodai.

Kutoka viti 4 vya kuchaguliwa bunge lililopita, mpaka viti zaidi ya 20, ni ongezeko la asilimia zaidi ya 500%, huku ni kupaa wakati CCM imeporomoka kwa asilimia kadhaa!.

Wakati mshindi atatangazwa leo, na hakuna ubishi ni mgombea wa CCM, wana CCM wote wenye akili timamu, japo watafurahia ushindi wao, lakini kimoyomoyo, wanajua kwa dhati, ndani ya mioyo yao, Chadema sio chama cha kubezwa ila kama kawaida, mataahira wasio na uelewa wa kweli wa mambo, hawatakosena kuibeza Chadema!.
Umesema kweli PAsco
Inahitajika akili kujua, hayo yote uliyoyasema, lakini kama akili za wana ccm za kutingisha bsi
watafurahia sana ushindi wa mbinu chafu, Daima pesa tamu kuitumia ni ile ya kupata kwa njia halali
laikini si ya kupora ama kuiba hiyo hata chakula chake hishibi
 
Mhh, hesabu gani hizo za asilimia 500, wakati ni ongezeko 4-20 + against 239-(4 +), be careful. thanks

Sina shaka una mswaki (F) wa hesabu ndiyo maana mnashindwa kuchakachua bila kujulikana. UKiwa na maembe manne, ukaongezewa manne ni sawa na ongezeko la asilimia ngapi? Kama siyo 100%? Kama asilimia ni shida basi tumia folds na utaona ni ongezeko la 5 folds (au mara tano zaidi)!

CHADEMA has enjoyed an increase of 20/4 * 100 = 500%
 
Wanabodi,
Uchaguzi umeisha, pamoja na kuukosa urais kwa mgombea wa Chadema kwa sababu zozote zile ikiwa ni pamoja na uchakachuaji, lazima tukubali, Chadema inastahili pongezi, na imetingisha kiukweli kweli na sio kutikisa tuu kama walivyodai.

Kutoka viti 4 vya kuchaguliwa bunge lililopita, mpaka viti zaidi ya 20, ni ongezeko la asilimia zaidi ya 500%, huku ni kupaa wakati CCM imeporomoka kwa asilimia kadhaa!.

Wakati mshindi atatangazwa leo, na hakuna ubishi ni mgombea wa CCM, wana CCM wote wenye akili timamu, japo watafurahia ushindi wao, lakini kimoyomoyo, wanajua kwa dhati, ndani ya mioyo yao, Chadema sio chama cha kubezwa ila kama kawaida, mataahira wasio na uelewa wa kweli wa mambo, hawatakosena kuibeza Chadema!.

Uchaguzi umeisha , hivi sasa gumzo si CHADEMA tena yameisha pita hayo na mgombea wao slaa , hivi sasa watu wana discuss nafasi ya u-spika na muundo wa baraza la mawaziri.
 
the dreamer,
haya tuanze. kuna kura 4 kati ya 239 sawa na 1.67% then unaongeza uwezo toka kura 4 hadi 20, sawa na 8.37%
kwa hiyo unatokea 1.67% kwenda 8.37% sawa na ongezeko la 6.70%
Hii ni taaluma mwana jf, hakuna mbege wala chadema hapa. thanks
 
Mhh, hesabu gani hizo za asilimia 500, wakati ni ongezeko 4-20 + against 239-(4 +), be careful. thanks

Yaonekana wewe hesabu ulikwepa kuanzia darasa la kwanza kwa taarifa yako wangeongezeka 2 ingekuwa 50%, angalia ulivyo kilaza wa hesabu uanadiriki kuweka utumbo kama 4-20 + against 239-(4 +) rudi darasa la pili ujifunze kuhesabu
 
the dreamer,
haya tuanze. kuna kura 4 kati ya 239 sawa na 1.67% then unaongeza uwezo toka kura 4 hadi 20, sawa na 8.37%
kwa hiyo unatokea 1.67% kwenda 8.37% sawa na ongezeko la 6.70%
Hii ni taaluma mwana jf, hakuna mbege wala chadema hapa. thanks

Rejea tena post yangu nimerekebisha ili uweze kuelewa. Usipoelewa sina msaada. Hapa hesabu siyo wana fraction ngapi ya viti vyote bali wamepata ongezeko gani. Tembelea hii page kuona mtu akisema 800% anakuwa na maana gani Percentage - Wikipedia, the free encyclopedia

Kwa style yako hata CCM hawawezi kupita 100%. Inabidi ujue mtu ana maana gani anapotumia neno ongezeko!

Halafu sijwahi kusikia au kuona percentage zikijumlishwa au kutolewa kama ulivyofanya...sijawahi!!!!
 
the dreamer,
haya tuanze. kuna kura 4 kati ya 239 sawa na 1.67% then unaongeza uwezo toka kura 4 hadi 20, sawa na 8.37%
kwa hiyo unatokea 1.67% kwenda 8.37% sawa na ongezeko la 6.70%
Hii ni taaluma mwana jf, hakuna mbege wala chadema hapa. thanks

Hutakaa uelewe umezoea kuchakachua, hesabu huwa haichakachuliwi elewa kilichoandikwa wewe kichwa mbofu mbofu ni ongezeko la idadi ya wabunge from 4 to 20 huelewi nini aghhhhhhhhhh!!!!!!! Ke*ge
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom