Bunge imekuwa sehemu ya malalamiko tu! Hakuna mbinu mpya za kusaidia maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge imekuwa sehemu ya malalamiko tu! Hakuna mbinu mpya za kusaidia maendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Jul 13, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Bunge letu la Tanzania limekuwa na vitu vikubwa viwili (1) Sehemu ya malalamiko (2) Sehemu ya kusemana vyama vya upinzani na serikali. Hivyo ni vitu vizuri lakini je nani Tanzania anaongelea mbinu mpya za mandeleo kuanzia kwenye elimu, Afya, Biashara, Viwanja na Barabara je mbinu mpya ziko wapi na ni nani anaongea. Pamoja na Maendeleo ya hapa Marekani kila siku kuna mbinu mpya watu wanakuja nazo za kutatua matatizo tofauti kuanzia kuboresha elimu, Afya na biashara. Mimi natafuta kwenye magazeti, bunge na hapa JF watu wenye mawazo mapya ili tukosoane lakini sipati napata malalamiko tu kuanzia bungeni mpaka hapa!. Umasikini wetu unatokana na vitu vingi na ni lazima kila siku tufikirie mbinu mpya za kujiendeleza. Ukifikiria vizuri hata sisi vijana tulioko nje tulikuja kama mbinu ya kujiendeleza hata kama tusikofanikiwa lakini mafanikio hayatatoka kama hubadilishi mbinu kutokana na hali yako.
   
 2. m

  muchetz JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Naamini una maana pana ya bunge la CCM.
   
 3. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  UONGOZI ni UBUNIFU. Ni kweli hakuna hilo bungeni, "wanajuana"
  Wanaenda kujadili unyonge wetu, eti unasikia cheko za kimbea, mizaha, mijitu inalala ovyo, wanakurupuka, kushangilia kama wapo disko, wote wamoja. Mwerevu yeyote hawezi kukaa kwenye jumba lenye uozo kama lile! Silipendi kabisa! Fujo, vijembe, cheko, kelele, mizaha, dharau, utoto, ulimbukeni, upunguani, ubishoo, misifa ya kijinga, umajinuni, udaku, porojo, uropokaji, kujikweza, nk.vimejaa ndani ya jengo lile, eti wanajadili mustakabali wa mtanzania, ni wazi msafi yeyote angeingia mle mara 1 tu, akawasema na asingerudi tena hadi heshima na hadhi yake itakaporejeshwa.
  Mungu wetu anaita!
   
Loading...