engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,150
- 1,437
Salaam waheshimiwa wabunge(wawakilishi wa watanzania)!
Waheshimiwa!
Mjadala huu naleta mbele ya BUNGE HURU LA WANAJAMIIFORUM. Hivyo yeyote atakayechangia au atakayesoma comments namwomba ajivishe cheo cha ubunge(uwakilishi wa watanzania).
Waheshimiwa wabunge!
Yamebaki takribani siku 4 tu tumalize huu mwaka wa 2013 na kuingia mwaka mwingine mpya 2014. Tukiwa kama wadau muhimu sana wa maisha ya taifa la tanzania, naombeni tufanye tathmini fupi fupi sana(tusichoshane na mithread mireeeeefu) kuhusu hali ya maisha ya watanzania mwaka 2013, na pia vipi dalili za mwaka 2014. Tusiache kugusa elimu, afya, uchumi(purchasing power), historia, siasa kwa ujumla wake, utendaji wa serikali ya Tanzania na maendeleo ya watanzania kwa ujumla wake.
Kwenye hii thread usimtaje member(mbunge) mwenzako kama mkuu, bali jivishe/mvishe uheshimiwa. Kwa mfano mimi nitatajwa mh UNDENIABLE badala ya mkuu UNDENIABLE
NB:
Tuweke uchadema na uccm pembeni. Tanzania kwanza vyama baadaye!
Kwenye hii thread usimtaje member(mbunge) mwenzako kama mkuu, bali jivishe/mvishe uheshimiwa. Kwa mfano mimi nitatajwa mh UNDENIABLE na sio mkuu UNDENIABLE
Ahsanteni , naomba kuwasilisha
UNDENIABLE
CC: Mzee Mwanakijiji, Pasco
Mh Spika
nashukuru kwa kunipa nafasi nami niseme machache juu ya nini kimejiri 2013 na nini tutegemee 2014.
Mh Spika,yapo mengi mazuri yamefanyika kwa mwaka huu tunaouaga 2013 na kwa mwonekano wa kawaida yataendelea kufanyika ama kutendeka mwaka ujao wa 2014,kama ulivyosema tusichoshane,lakini kiukweli,Nchi yetu inaonyesha kusonga mbele hususani ktk nyanja mbalimbali
1.barabara zinaendelea kupitika na asilimia 78 ya mikoa yetu imeungwanisha kwa rami,
2.Ktk mji wetu mkuu wa kibiashara msongamano wa magari unaendelea kutibiwa kwa kuwepo kwa train na barabara ya magari yaendayo kwa kasi inaonekana kukamilika na angarau tumeonyeshwa basi la mfano wake
3.Mh Spika,kwa sisi wa maeneo ya mito na mabonde,tunaendelea kushukuru baada ya kuona daraja la mto kilombero likifanyiwa kazi na hii itatusaidia sana kupitisha mipunga yetu na kuifikisha sokoni kwa haraka
4.tumeona mkonga wa Taifa,nao umekamilika ingawaje matumizi yake bado hayajaleta unafuu ktk bei za upigaji simu na mitandao,lakini Mh Spika nadhani mwaka 2014 mambo yatakuwa mazuri.
naomba nimalizie dakika zangu 3 zilizobaki kwa kusema kutoa angalizo langu kwa kiti
1.kiti kisimamie haki na kama inawezekana basi haya mapungufu yalionekana mwaka huu tunaoumaliza yasijirudie tena mwaka ujao,
2.tunategemea mwaka ujao,hakutakuwa na operation tokomeza,kuferi kwa vijana wetu hususani hawa wa darasa la 14 na pia mwaka 2014 hatutegemea kupata habari ya wanafunzi wasiojuwa kusoma kupatikana wakiwa kidato cah kwanza,hii ni aibu kwa bunge na kwa kiti pia.
3.tunagemea kuona uwajibikaji zaidi mwaka 2014,hususani kwa serikali,viongozi na wananchi kwa ujumla na mwisho kabisa
4,Mh Spika,ninge penda kuona AZIMIO LA ARUSHA likirudishwa 2014 na kama upo uwezekano mambo yake yawekwe ktk katiba,hii itasaidia sana kuwabana viongozi wanaoficha pesa nje ya Tanzania,viongozi wanaofanya biashara na kujilimbikizia mali na wala rushwa watabanwa kama azimio hili litalejeshwa.
Naomba nisiwachoshe,kwani namwona Mh Pasco kanyoosha kiganya chake juu,nadhani mwenzangu ataongelea zaidi mafanaikio ya KATIBA MPYA kwani hili ni swala nyeti sana na kiukweli sisi kama wabunge ni lazima tujipongeze kwa kulisimamia hili,kwani tumejitahidi kupita kwa wapiga kura wetu na tuliwahamasihsa na kuwapa elimu juu ya katiba na mungu akipenda mwaka 2014 tunaweza kupata katiba mpya.
Naona kengere inagonga kuashiria muda wangu kuisha,nashukuru kwa kunipa nafasi Mh SPIKA