Bunge huru la wana JamiiForums: Tathmini ya maisha ya watanzania mwaka 2013!

UNDENIABLE

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
2,303
1,500
Salaam waheshimiwa wabunge(wawakilishi wa watanzania)!

Waheshimiwa!
Mjadala huu naleta mbele ya BUNGE HURU LA WANAJAMIIFORUM. Hivyo yeyote atakayechangia au atakayesoma comments namwomba ajivishe cheo cha ubunge(uwakilishi wa watanzania).

Waheshimiwa wabunge!
Yamebaki takribani siku 4 tu tumalize huu mwaka wa 2013 na kuingia mwaka mwingine mpya 2014. Tukiwa kama wadau muhimu sana wa maisha ya taifa la tanzania, naombeni tufanye tathmini fupi fupi sana(tusichoshane na mithread mireeeeefu) kuhusu hali ya maisha ya watanzania mwaka 2013, na pia vipi dalili za mwaka 2014. Tusiache kugusa elimu, afya, uchumi(purchasing power), historia, siasa kwa ujumla wake, utendaji wa serikali ya Tanzania na maendeleo ya watanzania kwa ujumla wake.

Kwenye hii thread usimtaje member(mbunge) mwenzako kama mkuu, bali jivishe/mvishe uheshimiwa. Kwa mfano mimi nitatajwa mh UNDENIABLE badala ya mkuu UNDENIABLE

NB:
Tuweke uchadema na uccm pembeni. Tanzania kwanza vyama baadaye!

Ahsanteni , naomba kuwasilisha
UNDENIABLE

CC: Mzee Mwanakijiji, PascoMODS NAOMBENI ILE MICHANGO MIZURI KUTOKA KWA MEMBERS(WABUNGE) ZIUNGANISHWE ZIWE JUU HUKU MWANZONI MWA THREAD. AHSANTENI SANA.
Invisible, @
Paw

Bunge hili litahairishwa tarehe 31.12.2013 saa 6:00 usiku

TAHADHARI:
HURUHISIWI KULETA MAMBO YA CHIT CHAT KWENYE HUU UZI. HAPA NI JUKWAA LA SIASA SIO CHIT CHAT

Kuelekea tathmini ya mwaka 2014. Naomba mnitumie PM kwa yeyote anaetaka kuwa mbunge wa jimbo fulani na chama chake, ama waziri wa wizara fulani. Ahsanteni sana!
 
Zipuwawa

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
3,058
2,000
Mheshimiwa hatuwezi kuweka vyama pembeni kwani kuna vyama ndio vinazidi kutuangamiza kila kukicha hivyo turuhusu tu wa bunge wa vyama vyote tuwawakilishe wananchi wenzetu la sivyo itakuw ngumu kuweka chama kama CCM pembeni kwenye janga hili la Taifa ndg mheshimiwa
 
Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
11,227
2,000
hali imekuwa ngumu kweli kwa wananchi,maboresho ya huduma mbalimbali za jamii yamefanyika kwa kiwango cha chini ya asilimia 50,huku elimu kwa wanafunzi ikizidi kudorora,tatizo mishahara hewa likishindikana kumalizwa lakini kwa watu kama wabunge hali ni nzuri sana na ya neema kubwa kweli kweli asanteni sana waheshimiwa,hizi sikukuu zimekwangua fedha yote,lkn nafikiri vikao haviko mbali toka sasa
 
Amwesiga

Senior Member
Oct 2, 2011
150
170
Mh: Mimi nalia na swala upandishwaji bei ya bidhaa kiholela bila kujali ongezeko la kipato cha Mtanzania wa kawaida, na tofauti kubwa iliyopo kwa walionacho na wasionacho. Kimsingi serikali tunapoelekea 2014 ingalie mfumo rasilimali ambazo zitapelekea mtanzania wa chini kufaidika na kumpa unafuu wa maisha. Tuombe aman na utulivu na upendo kwa wote bila kuangalia dini, kabila na itikadi za kichama. Nawasilisha
 
UNDENIABLE

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
2,303
1,500
Mheshimiwa hatuwezi kuweka vyama pembeni kwani kuna vyama ndio vinazidi kutuangamiza kila kukicha hivyo turuhusu tu wa bunge wa vyama vyote tuwawakilishe wananchi wenzetu la sivyo itakuw ngumu kuweka chama kama CCM pembeni kwenye janga hili la Taifa ndg mheshimiwa
Mh zipuwaa hoja yako imesikilizwa. Endelea mh!
 
Chimbuvu

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
4,399
2,000
Ndugu waheshimiwa tabia za vijana wa kitanzania kubadili wasichana kama nguo ikome na kwa upande wa wasichana kubadili wanaume kama nguo ikome.itungwe sheria iwapo mvulana atakapokutana kimwili na mwanamke basi huyo atakuwa ni mke halali na yeyote atakayebainika anatembea nje ya ndoa apewe adhabu ya miaka 7 jela na viboko 10,vitano akiwa anaingia na vitano akiwa anatoka ili akawaonyeshe watoto wake.
 
UNDENIABLE

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
2,303
1,500
hali imekuwa ngumu kweli kwa wananchi,maboresho ya huduma mbalimbali za jamii yamefanyika kwa kiwango cha chini ya asilimia 50,huku elimu kwa wanafunzi ikizidi kudorora,tatizo mishahara hewa likishindikana kumalizwa lakini kwa watu kama wabunge hali ni nzuri sana na ya neema kubwa kweli kweli asanteni sana waheshimiwa,hizi sikukuu zimekwangua fedha yote,lkn nafikiri vikao haviko mbali toka sasa
Mh upo live ujue. Wapiga kura wako wanakutazama na kukusikiliza!
 
UNDENIABLE

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
2,303
1,500
hali imekuwa ngumu kweli kwa wananchi,maboresho ya huduma mbalimbali za jamii yamefanyika kwa kiwango cha chini ya asilimia 50,huku elimu kwa wanafunzi ikizidi kudorora,tatizo mishahara hewa likishindikana kumalizwa lakini kwa watu kama wabunge hali ni nzuri sana na ya neema kubwa kweli kweli asanteni sana waheshimiwa,hizi sikukuu zimekwangua fedha yote,lkn nafikiri vikao haviko mbali toka sasa
Mh niggas vikao vya wabunge ni posho ya kawaida tu kama wafanyakazi kwenye taasisi zingne. Wapiga kura wasijeelewa vibaya!
 
UNDENIABLE

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
2,303
1,500
Ndugu waheshimiwa tabia za vijana wa kitanzania kubadili wasichana kama nguo ikome na kwa upande wa wasichana kubadili wanaume kama nguo ikome.itungwe sheria iwapo mvulana atakapokutana kimwili na mwanamke basi huyo atakuwa ni mke halali na yeyote atakayebainika anatembea nje ya ndoa apewe adhabu ya miaka 7 jela na viboko 10,vitano akiwa anaingia na vitano akiwa anatoka ili akawaonyeshe watoto wake.
Mh chimbuvu naamini viongozi wa serikali wataliangalia hili
 
LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,036
2,000
Mheshimiwa, wewe ni mdau kwa namna moja ama nyingine! Please wakilisha watanzania wenzako!

Mheshimiwa UNDENIABLE kwa kweli hali si nzuri hata kidogo kwa wanainchi wa wilaya yangu binafsi. Nikigusa upande wa elimu kidogo tu nakwambia Mh ya kwamba huko ni majanga makubwa yatatarajiwa huku tunakoelekea jamani. Shule za kata ni mzigo mkubwa kwa Taifa letu tulipendalo ambalo tunalitarajia kuwa na viongozi bora hapo baadae.
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom