Tetesi: Bunge halitakuwa LIVE Juni 10 kupitia mkataba wa bandari

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
214
686
Kuna tetesi kuwa wabunge wa CCM wametoa shinikizo kwa Spika, Dk. Tulia kuhakikisha kikao cha kesho cha kupitisha azimio la kuuza bandari zote za Tanzania bara kwa Mwarabu hakionyeshwi LIVE kwenye Tv ili kuwanusuru kwa wananchi ambao wako kwenye taharuki kubwa.

Wabunge hao inasemekana wameomba pia waandishi wa habari wasiruhusiwe kuingia kwenye kikao cha kesho ili kuwezesha kupitisha azimio hilo bila kujulikana na wananchi ni mbunge gani alisema nini katika kuunga mkono azimio hilo.

Uamuzi huo wa wabunge umetajwa kuchochewa na mashinikizo makubwa waliyoyapata kutoka kwa wananchi ambao wamewapigia simu, kuwatumia ujumbe wa maandishi na kuwaandikia barua wabunge kuwa wakipitisha azimio hilo wasirudi majimboni wapitilize moja kwa moja Dubai.
 
Watu kama wakina msukuma na kibajaji(tabu darasa) wasiojua hata kutafsiri mikataba ya kimataifa ndio wanatuletea shida yote hii na mama yao
 
kama ni msiba wimbo huu ungefaa kuwa kama pambio kwa Tanganyika yangu ambao blass bend huupiga wakati mwingine wa dhifa za kuitafuna nchi
1. Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2...

2. Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

3. Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2
 
Mbona Migodi iliuzwa kwa Wazungu kwa miaka 99 na Wananchi hawakupatwa na taharuki?

Bunge lionyeshwe live kwanza wengi humo ni Wabunge wa kuteuliwa na Magufuli hawakuchaguliwa na Wananchi wanaogopa nini? waache unafiki.
 
Najaribu kuvaa viatu vya mwalimu kama angekuwa hai nashindwa nashindwaaaaa kikwete unahuruma na mwalimu wewe?
 
Back
Top Bottom