Bunge halina uwezo kutunga Katiba mpya;MWANASHERIA Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge halina uwezo kutunga Katiba mpya;MWANASHERIA Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 9, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Saturday, 09 April 2011 08:39

  Salma Said, Zanzibar

  MWANASHERIA Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Othman Masoud amesema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halina uwezo wa kutunga Katiba mpya, bali kuifanyia marekebisho iliyopo."Bunge la Jamhuri halina uwezo wa kutunga Sheria ya Katiba hili ni jambo la msingi sidhani Zanzibar na watu wake kama watakubali kuvunja Katiba," alisema.

  Masoud alisema hayo jana akitoa mchango wake katika mjadala wa maoni ya Muswada wa Sheria wa Mapitio ya Katiba unaoendeshwa na Kamati ya Bunge, Sheria na Katiba ya Bunge la Muungano
  uliofanyika katika Hoteli ya Bwawani mjini hapa.

  Alisema msingi wa hoja yake unatokana na Kifungu cha 98(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano kinachoeleza. Kifungu hicho kinasema: "Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii au masharti yoyote ya Sheria yoyote yanayohusika na jambo lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika Orodha ya Pili kwenye Nyongeza ya Pili iliyoko mwishoni wa Katiba hii, utapitishwa tu iwapo utaungwa mkono kwa kura za Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Zanzibar."

  Orodha hiyo ya pili kwenye nyongeza ya pili iliyoko mwishoni wa Katiba inaeleza mambo ambayo mabadiliko yake yanahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Tanzania bara na theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Tanzania visiwani moja likiwa mambo ya muungano ambalo suala la Katiba ni mojawapo.

  Alisema Bunge lililopo sasa haliwezi kutunga Katiba mpya, bali kazi yake ni kurekebisha hivyo linatakiwa liwepo Bunge jingine ambalo litakuwa maalumu kwa ajili ya kutunga Katiba.

  Akiwasilisha madhumuni na sababu za muswada huo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta alisema umependekeza kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya nchi ya mwaka 2011 na unakusudia kuanzishwa kuweka masharti ya uanzishaji wa tume pamoja na sekretari kwa madhumuni ya kuendesha na kusimamia mchakato wa mabadiliko ya hayo.

  Mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na mambo mengine, utaangalia chimbuko na uhusiano wa katiba iliyopo kwa kuzingatia uhuru wa wananchi na mfumo wa siasa.

  Alisema pindi muswada huo utakapopitishwa na kuwa sheria, utakuwa na utaratibu wa kisheria utakaomwezesha Rais kuunda tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba na kuunda Bunge la Katiba kwa madhumuni ya kutunga Katiba mpya.

  Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan Juma amesema muswada wa marekebisho ya Katiba ya Muungano una upungufu mwingi ukiwemo kutoshirikishwa kwa Serikali ya Zanzibar ambayo alisema haikushirikishwa kikamilifu ili kutoa maoni yake na wala haukupelekwa katika Baraza la Wawakilishi kupata maoni ya Baraza, hivyo haukustahiki kupelekwa Bungeni kujadiliwa kwani umekosa ridhaa za pande mbili.

  “Muswada huo ni vyema kurudi serikalini na ukafanyiwe marekebisho na badala yake upelekwe katika Baraza la Wawakilshi ili upate ridhaa ya nchi mbili zilizoungana,” alisema Hamza.

  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Dk. Omar Dadi Shajak alisema kwa kuwa utaratibu haukufuatwa basi muswada huo haufai.“Taratibu hazikufuatwa na misingi ya kujadili kama Jamhuri ya Muungano mchakato wa muswada huu haukubaliki kwani utaratibu haukufuatwa,” alisema Shajak.

  Alisema mu8swada huo uko upande mmoja na umepitishiwa bungeni bila kuzingatia pande mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jambo ambalo haliwezi kuachiwa kupita hivyo hivyo kwani kufanya hivyo ni kuidharau Zanzibar ambayo ni mshirika kamili katika Muungano huo.

  “Muswada huu wote urejeshwe bungeni na utengenezwe tena kama kwa kuweka usawa au vyinginevyo, lakini kwa hivi haukubaliki kabisa,” alisema Shajak.

  Shajak alisema katika Bunge, jambo linalohusu Katiba ya Zanzibar na suala lolote lile la Muungano ni vyema kutumika usawa wa wajumbe Zanzibar na Bara na siyo kuamuliwa tu na wajumbe kutoka upande wa Tanzania bara peke yao.Mjumbe kutoka CCM, Ali Mwinyi Msuko aliwataka wanasheria wa Zanzibar kukutana na wenzao wa Tanzania bara kuupitia upya muswada huo akisema hakuna sababu ya kuuharakisha kuufikisha bungeni.

  Waziri wa Kilimo, Mansour Yusuf Himid alisema muswada huo una lengo la kuwadanganya Wazanzibari na hakuna jambo jingine.“Nashukuru siku hii ya leo, Kamati ya Bunge imekuja kutudanganya Wazanzibari na siku ya leo nina huzuni kubwa sana kama Mtanzania, kama Mzanzibari, naona kiini macho tu tunafanyiwa kama Baraza la Wawakilishi hawajashirikishwa, basi hakuna haja ya kukubali hilo,” alisema kuongeza:

  “Lazima tushirikishwe ipasavyo. Tumeungana kwa hiari. Hii ni Jamhuri ya pande mbili tumekwenda kwa hiari, tutarudi kwa hiari, tutabaki kwa hiari. Kama Wazanzibari hawajashirikishwa kupitia kura ya maoni na kufanyiwa kiini macho hicho, basi wasikubali kudanganywa," alisema huku akiungwa mkono na wananchi wengine walioshiriki mjadala huo.

  Mansoor ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki (CCM), alisema binafsi anaupinga muswada huo huku akisema hiyo ni nafasi pekee ya kuhakikisha muungano unafanyiwa marekebisho na kwamba hiyo ni fursa ya pekee kwa wananchi wa Zanzibar kupinga kwani hawataipata tena iwapo muswada huo utapita.

  “Hii ndiyo fursa yetu ya mwisho Wazanzibari, nikwamabie tukicheza hapa ndiyo basi hatutakiona kitu chochote ndiyo basi tena,” alisisitiza.Mwandishi wa habari mwandamizi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Ally Saleh alisema muswada huo haukugusia Katiba ya Zanzibar jambo alillotafsiri kama dharau juu ya makubaliano ya Muungano.

  “Kura ya maoni ni kitu gani? Je, Wazanzibari wakisema hawataki athari yake itakuwa nini? Tusifikiri Wazanzibari watapinga Katiba je, athari zake zitakuwa ni nini? Kusema tume isipelekwe mahakamani huko ni kuizuia demokrasia,” alisema.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  naona wazanzibar wanaakili kushinda bara aisee! wameungana hakuna uccm wala ucuf!
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  habari ndio hiyo, sasa wajuvi wameze au wateme

  enzi za usanii kwisha,

  sasa tuna enzi za ulikrusha kombora na sisi tutalirusha.

  tuache kudharauliana na tukae kama watu wazima tujadili hatima ya muungano wetu, haiwezekani tukae kujadiliana kumalizana kwa amani

  huo ndio ukweli wa mambo
   
 4. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ukweli utabaki pale pale-wahafidina wa ccm wanataka kuwaaminisha wananchi wa sasa kuwa mambo yako shwari na mchakazo wa sheria hii ni safi tu, huku wakijua kuwa mswada unabaka demokrasia kwa waliowengi. hayo ni mambo ya kizamani kwa sasa hayakubaliki. Watanzania wanatakiwa kuweka masilahi mbele ya utanzania na si uccm kama wanavyofanya wana ccm bara-kufikiri kila kitu apewe Rais au waziri mwenye dhamani-ridiculus!!
   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Si kweli kwamba Wazanzibari wana akili kushinda Wabara! Hizi general comments hazina maana yoyote, kwamba eti watu wooooote wana akili kuliko watu fulani wooooote! Very ridiculous statement, indeeed!
   
 6. a

  ali mc Member

  #6
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mwaka huu wabara watakiona cha moto maana walizoea kuburuza wazanzibari kiubabe. Wameamka na wanadai chao na heshima yao iliyopotezwa. - kwetu sisi muungano ni ishara, ilivyotupata hasara, kupoteza yetu dira na heshima ya uzawa. Kuanzia sasa liwalo na liwe mpaka tuipate haki yetu
   
 7. r

  rassadata Member

  #7
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kimsingi watanzania tubadilike,tuchangie kwa kujenga nchi yetu sote.Nampongeza huyo mchangia mada kwa kweli.

  Big up sana wazanzibari.
   
 8. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama sio akili ni nini??
   
 9. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Who is ridiculous..? You or ZnZ Peoples?? kama hawana akili zaidi basi wana mshikamano zaidi hawanunui watoto kwenda kulala kwenye mjadala muhimu kama mlivofanya wa bara..none sence
   
 10. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Unafiki mtupu. Kwa nini mnashindwa kuisema ccm yenu? Wazanzibar siyo wanaoiunga mkono ccm na vibaraka wao? Huo muswada umeandaliwa na ccm. Au mtwambie kumbe wale wote walioupinga pale Nkurumah walikuwa Wazanzibar??? Double standard wakisema Watanganyika tunaambiwa ni wanasiasa wanapotosha uma, wakisema visiwani ni wazanzibar wote.. Mwaka huu tutaona mengi.
   
 11. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  Wengi wa watangika wanawazarau sana wazanzbari na hasa vijana wa sasa,mutambue kuwa zanzbar kuna 1.2milioni people,katika ho wasomi kwa kukisia ni kama laki tatu,kiukweli ni wengi wasomi ukilinganisha na population ya tanganyika 43milion,wasomi hawafiki hata milioni moja,hao ma profesor wanajulikana kwa hesabu na wingi mulionao,angalia zanzibar wako wangapi na ma profesor wangapi ?

  Kiukweli na kwamba wazanzibar wanatumia hoja kujadili kitu sio jazba,ndio ukaona mswaada umepingwa tena kwa points na maelezo ya uhakika na kisheria,lakini angalieni upande ya bara,ngumi mtu,,,,sasa munafanyaje ? Tumieni usomi wenu tumieni akili zenu na upeo wenu,wakati wangumi umemaliza.

  Shikamaneni kwa umoja tumalize migogoro hii ya kisiasa,mana hapa kuna usiasa sio uzalendo.

  NAWAKILISHA
   
 12. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  Wembe ndio huu huu ni suhindi tu utapatikana,kuvunja muungano,au tujadili upya muungano tena kwa pande mbili zilizoungana sio tanzani noo tunataka tanganyika,kama hamuezi basi tuvunjee.
   
 13. F

  Falconer JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Ushabiki wa vyma uishe sasa hivi tunaangalia katiba ya nchi. Tusikubali kuburuzwa na chama tawala kwa sabau tukifanya hivo tunakosa umuhimu wa utaifa. Chama tawala na uendeshaji wa serikali ni vitu viwili tafauti. CUF kuikubali CCM ni strategy za kisiasa sabau CCM waliiba kura za CUF majimbo yote ya pwani sasa CUF watafanya nini. Lazima watumie akili na CCM kwa kuwa ndio wenye nguvu ya dola, wanafanya wanavotaka. Tumeweza kufanya serikali ya umoja Zanzibar na tunaona uzembe wa ma CCM wakati wakuchagua viongozi wa serikali. Wamejichagua wenyewe lakini wamesahau kuwa 80% ya wazanzibari ni CUF. Mchakato wa mswada huu unaendelea. Tutahakikisha wananchi wameelimishwa kufahamu muungano na katiba yake na ukweli tulipofika sasa.
  Lazima wananchi wote wahakikishe haki yao wameidhibiti. Watanganyika musilale amkeni sana maana kuna wizi unataka kufanyika juu ya katiba na haki ya wananchi. AMKENI ndugu zetu maadamu mumeyasikia ya zanzibar, hakuna tena kurudi nyuma. SONGA MBELE ndio slogan ya kuwashinda hawa.
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Na hiyo signature, umechakachuwa quran hiyo aya inasema hivi:

  Qur'an 46:9 Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi.

  Qur'an 46:10. Sema: Mwaonaje yakiwa haya ni kweli yametoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi mmeyakataa, na akashuhudia shahidi miongoni mwa Wana wa Israili juu ya mfano wa haya, na akaamini, na nyinyi mnafanya kiburi? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.
   
 15. m

  mbungula Member

  #15
  Apr 10, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nikweli wa wazenji wanauelewa zaidi ya
  watu wabara ambao wamekalia unafiki bila
  hata yakufikiria tz ya kesho maana
  hata watu ccm wanaukataa mswada huu wakati
  bara ccm wanaukubali
   
 16. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #16
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Henge tunaomba ufafanuzi wa maoni yako ukitoa mifano halisi.
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sijakuelewa ndugu yangu, kwani bara wote ni ccm, je wanachama wa ccm wakiukubali ina maana watanzania tote wameukubali? Hebu elezea kidogo tukuelewe.
   
Loading...