Bunge halina mguso na wananchi 'out of touch | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge halina mguso na wananchi 'out of touch

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyundo Kavu, Feb 2, 2012.

 1. Nyundo Kavu

  Nyundo Kavu Senior Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Zitto Kabwe

  Bunge halina mguso na wananchi 'out of touch'

  Inasikitisha kwamba Bunge laweza kukaa wiki nzima na kujadili masuala mbalimbali bila kutoa muda kujadili suala la mtikisiko katika sekta Afya.
  Siku ya kwanza ya Bunge nilisimama kutaka taarifa ya serikali kuhusu mgomo wa madaktari na taarifa hiyo ijadiliwe na Bunge. Spika akalojulisha Bunge kwamba Serikali imempa taarifa na itawasilishwa. Bunge likaahirishwa siku bila kurejea. Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipohitaji taarifa ya Serikali, Serikali haikuwa na taarifa. Kwa hiyo walifanya ujanja ujanja kuzuia mjadala wa mgomo wa madaktari.

  Leo wabunge kwa mara nyingine wamesimama kutaka mjadala huu wa dharura. Naibu Spika wa Bunge akatumia sababu za kiufundi kuzuia mjadala. Inawezekana wabunge hawakuwaandaa wabunge kusimama kuunga mkono hoja, lakini ni jukumu la Kiti kuona umuhimu na udharura wa mijadala.

  Hii inadhihirisha kwamba sasa Bunge kama Mbunge mmoja mmoja au kwa ujumla wake na Taasisi ya Bunge imekosa mguso na Hali ya wananchi (out of touch). Hali hii ni hatari sana. Wananchi wanapoona chombo kinachowawakilisha hakitoi nafasi kwa masuala yanayowagusa, watachukua hatua zao wao wenyewe na hivyo kuhatarisha utulivu wa nchi. Bunge liache shughuli nyingine zote na kutoa fursa ya kupokea taarifa ya serikali kuhusu madai ya Madaktari, kuijadili na kuazimia kwa kuelekeza hatua za kutekelezwa na serikali.

  https://www.facebook.com/zittokabwe   
 2. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Wanaogopa kunyang'anywa posho zao.
   
 3. fikrapevu sungura

  fikrapevu sungura Senior Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=6]Zitto Kabwe
  [/h][h=6]Bunge halina mguso na wananchi 'out of touch'

  Inasikitisha kwamba Bunge laweza kukaa wiki nzima na kujadili masuala mbalimbali bila kutoa muda kujadili suala la mtikisiko katika sekta Afya.
  Siku ya kwanza ya Bunge nilisimama kutaka taarifa ya serikali kuhusu mgomo wa madaktari na taarifa hiyo ijadiliwe na Bunge. Spika akalojulisha Bunge kwamba Serikali imempa taarifa na itawasilishwa. Bunge likaahirishwa siku bila kurejea. Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipohitaji taarifa ya Serikali, Serikali haikuwa na taarifa. Kwa hiyo walifanya ujanja ujanja kuzuia mjadala wa mgomo wa madaktari.

  Leo wabunge kwa mara nyingine wamesimama kutaka mjadala huu wa dharura. Naibu Spika wa Bunge akatumia sababu za kiufundi kuzuia mjadala. Inawezekana wabunge hawakuwaandaa wabunge kusimama kuunga mkono hoja, lakini ni jukumu la Kiti kuona umuhimu na udharura wa mijadala.

  Hii inadhihirisha kwamba sasa Bunge kama Mbunge mmoja mmoja au kwa ujumla wake na Taasisi ya Bunge imekosa mguso na Hali ya wananchi (out of touch). Hali hii ni hatari sana. Wananchi wanapoona chombo kinachowawakilisha hakitoi nafasi kwa masuala yanayowagusa, watachukua hatua zao wao wenyewe na hivyo kuhatarisha utulivu wa nchi. Bunge liache shughuli nyingine zote na kutoa fursa ya kupokea taarifa ya serikali kuhusu madai ya Madaktari, kuijadili na kuazimia kwa kuelekeza hatua za kutekelezwa na serikali.

  [/h]
   
 4. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  halina tofauti na kijiwe cha kahawa hasa wale watoa maamuzi.
   
Loading...