jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,053
- 28,245
Naendelea kushangaa juu ya kigugumizi cha wabunge juu ya muswada huu muhimu unahusu afya za watanzania. Hili ni jipu la muda mrefu sana lenye kuhitaji tiba.
Siku za nyuma Serikali imekuwa inakwepa kuwasilisha muswada huu bungeni. Hata hivyo vision ya Rais Samia ilikuwa ni kuwasilisha muswada huu bungeni ili kupata suluhisho la namna bora ya uwezeshaji endelevu wa kifedha katika sekta ya afya. Kukwama kwa uwasilishaji muswada huu ni hasara kwa Taifa kwani katika kipindi kisichopungua mwaka mmoja sekta ya Afya kupitia wizara na wadau wamewekeza sana katika kujadili na kuja na muswada huu.
Ikumbukwe kuwa Sekta ya afya imeendelea kupitia wakati mgumu kwa kushindwa kujiendesha ipasavyo. Ikumbukwe kuwa bado bajeti ya sekta ya afya haijafikia azimio la abuja linalotaka Serikali kuwekeza 15% ya kipato chake kwenye maswala ya afya ili kuwa na sekta imara ya afya itakayojibu matakwa ya malengo ya milenia na malengo endelevu.
Bado sekta ya afya nchini inabakia kuwa ni sekta ya hisani ya watu wa Marekani n.k.
Bunge limehairisha bila kutaja ni lini haswa muswada huu utawasilishwa tena. Bunge limerejesha suala hili kwenye kamati ambayo imelikwamisha despite ushauri wa wataalamu ...Hili sio sawa. Hatuwezi kuwa na subira zisizo kikomo kungojea suala hili miaka nenda miaka rudi, ni muhimu kufikia maamuzi.
Bunge lina wajibu sasa wa kutueleza wananchi, wataalamu, Serikali, wadau ni namna gani tunahakikisha kuwa health sector financing itafanyika katika kipindi kingine cha kusubiri.
Nimpongeze Waziri Ummy kwa ujasiri wa kuzingatia maelekezo ya Mhe.Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan na kuandaa, kushirikisha na hatimaye kuwasilisha muswada huu hadi hatua iliyofikiwa.
Je Bunge kupitia kamati limekwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM Kifungu 83(e)????
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!