Bunduki zitanunuliwa kwa urahisi nikishinda, DP Ruto asema

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,457
2,000
  • Ruto anasema serikali yake itaweka wazi bajeti ya kununua silaha kama njia moja ya kuwezesha uwazi kwenye biashara ya kununua bunduki
  • Alisema bajeti hiyo huwekwa siri na hivyo kuwa mbinu ya wachache kujitajirisha kwa kufanya udanganyifu wa bei ya bunduki
  • Aliambia viongozi wa kanisa kwamba alitetea afisi ya IG ipatiwe bajeti lakini akaambiwa huwezi kumpa mtu bunduki na umpe pesa
Kiongozi wa Kenya Kwanza William Ruto amesema akishinda uchaguzi wa urais suala la kununua bunduki halitakuwa kibarua tena.

Bunduki Zitapatikana kwa Urahisi Nikishinda: DP Ruto Asema


Naibu rais William Ruto kwenye pich ya awali. Picha: DP

Alisema kwa sasa ununuzi wa silaha kama vile bunduki na mali nyingine ya vikosi vya usalama huwa ni siri kali. Aliahidi kuhakikisha kuwa hilo linafika kikomo na kila kitu kuwekwa wazi kuhusu bajeti na silaha zinazonunuliwa.

Kulingana na kiongozi huyo anayemezea mate kiti cha urais, ufisadi umeingia katika ununuzi wa silaha kutokana na siri inayozunguka shughuli hiyo. "Kwa nini isiwe tenda ya wazi? Hizi siri katika kununua silaha ndizo zinasababisha ufisadi kushamiri," alisema DP Ruto.

Kwenye kikao na wanainjili katika kanisa la Nairobi Baptist, Ruto alisema bei ya bunduki imekuwa ikiongezwa pakubwa ili kufaidi watu fulani. "Kwa nini iwe siri na kufanywa gizani? Hizi bunduki ziko huku mitaani ambapo zinabebwa na maafisa wa polisi, ni nini hiyo kubwa inafichwa? Inaitwa ununuzi wa siri kwa sababu zinanunuliwa KSh 20, 000 lakini bei inayopewa serikali ni KSh 60, 000," alisema Ruto.

Aliongeza kuwa serikali yake itahakikisha kuwa afisi ya inspekta mkuu wa polisi imetengewe bajeti ili kufanya kazi vilivyo. Kwa mujibu wa DP, kwa sasa afisi hiyo haina bajeti na hivyo haiwezi kutekeleza wajibu wake kwa njia huru na ya haki.

"Ni lazima tupatie inspekta mkuu wa polisi bajeti yake kama vile katiba inavyosema ili iwe afisi huru kwa sababu leo hii hilo halifanywi. Wakati niliuliza, niliambiwa eti huwezi kumpa mtu pesa na umpe bunduki eti anaweza kuleta shida kwa taifa," aliongeza DP Ruto

TUKO
 

abnormal

JF-Expert Member
May 6, 2017
274
1,000
Kwa hiyo hili ni jambo ambalo anapingana wazi wazi na polisi wa kenya, na sijui kama watamuelewa.

Ila nchi zetu hizi zina watu wa hovyo sana kwa kweli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom