Bunduki Mpya ya Marekani Yenye Uwezo Kumlenga Adui Sehemu Aliyojificha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunduki Mpya ya Marekani Yenye Uwezo Kumlenga Adui Sehemu Aliyojificha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 8, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Bunduki Mpya ya Marekani Yenye Uwezo Kumlenga Adui Sehemu Aliyojificha
  [​IMG]
  Bunduki mpya ya Marekani XM25 yenye uwezo wa kumtungua adui hata kama amejificha nyuma ya ukuta Monday, June 08, 2009 4:57 PM
  Jeshi la Marekani limetengeneza bunduki mpya ambayo ina uwezo wa kumtungua mtu popote pale alipojificha iwe ni nyuma ya ukuta au kwenye mabonde. Picha za bunduki hiyo mwisho wa habari hii. Bunduki hiyo iitwayo XM25 inatumia risasi ambazo hulipuka na kusababisha mvua ya risasi nyingi ndogo ndogo baada ya kwenda umbali uliosetiwa na mtumiaji wa bunduki hiyo.

  Jeshi la Marekani litatumia bunduki hizo kuwatungua maadui zao wanaojificha nyuma ya ukuta au kwenye mashimo kwani risasi za bunduki hiyo zikishafika eneo ambalo wamejificha hulipuka na kutoa risasi zingine ndogo ndogo nyingi sana ambazo kuzikwepa ni vigumu sana.

  Kwa mfano fikiria mtu amejificha kwenye shimo liliopo nyuma ya mwinuko wa ardhi na kwa mazingira ya kawaida risasi haiwezi kumpata kwa kuwa mwinuko utakuwa kama kinga yake, lakini kwa kutumia bunduki hiyo mpya, risasi itapigwa kwa juu hadi kwenye sehemu ambayo shimo hilo lilipo na itakapofika juu ya shimo hilo italipuka na kutoa risasi ndogo ndogo ambazo zitaelekezwa kwenye shimo hilo.

  Bunduki hizo zinatumia mfumo kama wa kompyuta kupiga mahesabu ya sehemu inayotakiwa kulengwa na risasi zake pia zina uwezo wa kupiga mahesabu zimesafiri umbali gani kabla hazijalipuka.

  XM25 zimeelezewa na kampuni iliyozitengeneza ya Alliant Techsystems kwamba zitasaidia kupunguza gharama kwani badala ya kurusha bomu ambalo lingerimu maelfu ya dola, bunduki hiyo ikitumika itagharimu dola 20 tu. Bunduki Mpya ya Marekani Yenye Uwezo Kumlenga [​IMG] Jeshi la Marekani limetengeneza bunduki mpya iitwayo XM25 ambayo ina uwezo wa kumtungua mtu popote pale alipojificha iwe ni nyuma ya ukuta au kwenye mabonde. [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 2. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mbona uchina wanayo siku nyingi tu.
   
 3. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Inatumika kufyatua 25 mm grenade.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jun 8, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  It fires [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/25_mm_grenade"]25 mm grenades[/ame] that can be set to explode in mid-air after traveling a certain distance....

  XM25 Prototypes in testing – 500% lethality increase over existing weapon systems

  [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/XM25_Individual_Airburst_Weapon_System"]XM25 Individual Airburst Weapon System - Wikipedia, the free encyclopedia[/ame]
   
  Last edited: Jun 9, 2009
 5. Natty Bongoman

  Natty Bongoman JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ushahidi vile ambavyo hawajali kuua wananchi ... so-called 'collateral deaths'
  ... badala ya kutengeneza darubini ambazo zitamuona adui aliejificha nyuma ya ukuta, wanatengeneza bunduki itakayolipua yeyote aliejificha nyuma ya ukuta... sa watoto na wanawake wakijificha, watajulikana vipi ka wao si adui?
  ...mfano, kule Iraki, so-called adui hawavai nguo za kijeshi, sa watajuaje nani ni adui ???
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  dunia hii inakwisha tena watu badala ya kumrudia mungu ndo kwanza wanatengeneza madubwana ya kuangamizana.
   
 7. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ila yao ni feki, haina risasi

  teh heh heh
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,496
  Likes Received: 1,057
  Trophy Points: 280

  Mkuu nakubaliana na wewe,
  Sasa subiri uone waarabu na waafrica tutakavyo zinunua kwa wingi ili tufyekane sawasawa!! Wamarekani wenyewe kimyaaaa kwao!
   
 9. Kiteitei

  Kiteitei JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 1,253
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  zote hizi ni za kummaliza binadamu huyu huyu nayemfahamu ambaye "mbu" (sio wa jf) anamdhibiti???!!
   
 10. Nostradamus

  Nostradamus JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [
  Marekani inamiliki silaha za nyuklia zenye uwezo wa kuangamiza dunia mara tatu(sijui naeleweka), wana bomu linaloitwa AMOEBI ambalo exploding power yakE ni mara nane ya kombora la nyuklia.isitoshe wana neutron bombs ambayo yana uwezo wa kuua viumbe hai tu na kuacha miji ikiwa ni mizima bila kuharibika.
  kwa hizi bunduki mpya sio ajabu,bali cha kujiuliza ni kwamba,wanajiandaa kwa vita ili waje wapigane na nani? THINK ABOUT IT........
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Naweza ipata wapi niitumie kwa JF members wanaonikera? teh teh teh teh....
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,598
  Trophy Points: 280
  Duuu hiyo binduki balaaa....sasa sisi africa tunahangaika na mlo mmoja kwa siku wenzetu ......wanafikiriaa mambo mengine kabisa.....
   
 13. D

  Dina JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Niliposoma kichwa cha habari, nikajua hizo risasi zinakata kona mpaka adui alipo!

  Malengo ya kutengeneza madubwesha yote haya, adui anayekusudiwa ni nani? Mimi nafikiri upande wa silaha, wafike mahali waseme sasa basi, kwa sababu watatumaliza!
   
 14. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #14
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mwalimi wangu wa Falsafa, aliwahi kunambia...

  "Mtawala Mwenye kuwapa Haki Raiya zake, Hana haja ya kununua Silaha"

  Hii yote ni dalili ya ubabe na ukandamizaji, wa kutaka kutawala hata wale wasio kuwa kwenye territory yako.
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  x-paster,
  sadakta.
   
Loading...