Bundi wazua tafrani mkutano wa CCM Kahama! Watua meza ya Lembeli, Mgeja... Wagoma kutoka ukumbini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bundi wazua tafrani mkutano wa CCM Kahama! Watua meza ya Lembeli, Mgeja... Wagoma kutoka ukumbini!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Oct 1, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  • BUNDI WAZUA TAFRANI MKUTANO WA CCM KAHAMA,
  • WATUA MEZA YA LEMBELI, MGEJA,
  • WAGOMA KUTOKA UKUMBINI,
  • DIWANI ASEMA MATUKIO YA USHIRIKINA LAZIMA YAKEMEWE

  Na Patrick Mabula, Kahama

  KATIKA hali ya isiyo ya kawaida Bundi wawili wameingia kwenye ukumbi wa mikutano kisha kutua meza kuu wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Kahama uliofanyika Shule ya Msingi Rocken Hill.

  Kituko hicho kilitokea jana wakati ndege hao aina ya bundi walipotua katika meza waliyokaa Mbunge wa Jimbo la Kahama, Bw.James Lembeli na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bw.Hamis Mgeja.

  Mbali na kutua kwenye za watu hao ambao ni mahasimu kisiasa, pia waliendelea kukaa ukumbimbi wakati shughuli za uchaguzi zikiendelea hali iliyozusha hofu miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo.

  Shuhuda wetu alieleleza kuwa tukio hilo lilitokea wakati wajumbe wakijiandaa kuchagua viongozi wao, ndipo bundi ha wawili wawili waliingia kwenye ukumbi wa mikutano. Kitendo cha bundi hao kuvamia mkutano huo kiliwafanya wajumbe kutaharuki na kila mmoja akitafasiri tukio hilo kwa mtazamo wake na wengine kulihusisha na imani za ushirikana.

  Wakati wajumbe wakiwa wamekaa ukumbini ghafla bundi hao waliingia ukumbini na kisha waliruka hadi kwenye meza ya Bw. Lembeli na Bw. Mgeja, kisha kusababisha matafaruku mkubwa kwa wagombea nafasi mbali mbali.

  Diwani wa Kata ya Chambo Bw.Damas Joseph, alisema mambo hayo yanayodhaniwa kuwa ya kishirikina katika chaguzi za CCM ni lazima yakemewe kwa vile yanawapa hofu mbalimbali na kuwafanya baadhi kutojiamini .

  Bw. Deo Ndimila tangu Kata ya Ukune alithibitisha vitendo vya kishirikina katika chaguzi za CCM mara nyingi zimekuwa zikitawala kwa baadhi ya watu kuendekeza imani hizo potofu.


  Chanzo: Majira
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Vyeo hivi JAMANI... BASI TU... MBONA VISA? Nimecheka Mpaka Mkoja karibia Utoke...
   
 3. SIM

  SIM JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 1,637
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Tawireee
   
 4. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hii mpya Bundiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, lakini ni kawaida maana uchawi wa wasukuma ni bundi na fisi
   
 5. m

  malaka JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wenyewe walikuja kusimamia uchaguzi toka HQ.
   
 6. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Si magamba wanasema cdm cha wakristo na cuf cha waislam! Sasa tumeishajua ccm cha akina nani! Sijui tuseme cha mabundi!
   
 7. C

  Cognitivist JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 973
  Trophy Points: 180
  Hapo tunasema ngoma droo.
   
 8. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Kama sio chama cha mabundi basi ni cha shetani! Manaake mabundi mkutaanoni tena! Nadhani hata freemason hawako hivyo!
   
 9. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,770
  Trophy Points: 280
  Chama cha wachawi

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 10. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ok kumbe na wao ni chama cha washirikina siyo
   
 11. b

  bariadi2015 Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 26, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nexy time atakuwa fisi,hawa wajamaa bana,wanga wachawi,wezi,yaani kila baya lao.
   
 12. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  CCM aka CHAMA CHA MABUNDI!!
   
 13. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ccm aka chama cha mabundi!
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Walinzi wa k.j wametumwa kulinda usalama
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Wajameni KUNA NINI HUMO NDANI ya CCM-NEC ? MAPESA YA GAS nini ?
   
 16. maghambo619

  maghambo619 JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 60
  cha wachawi
   
 17. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  haa!!. walikuja kusimamia uchaguzi. ole wao wachakachue. mia
   
 18. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hawana Mungu.
   
 19. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Alikuwa Nape na Mukama hao walikuja ku inspekti ati.
   
 20. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Hapa hata shetani atawavulia kofia CCM kwani kwa kiwango chake shetani hajawafikia na hafui dafu kwa chama kikuu cha mashirikina aka CCM
   
Loading...