jmchimbadhahabu
JF-Expert Member
- Sep 26, 2014
- 218
- 106
Hii imetokea siku ya leo asubuhi ambapo baadhi ya wananchi kwenda kuchimba katika eneo la NAMBA 2 ambalo lipo karibu na mgodi wa ACACIA Bulyanhulu wilayani Kahama.
Mamia ya vijana,wazee na akina mama walionekana kumiminika katika eneo hilo na kuanza kuchimba huku wakiimba nyimbo za kumsifu Rais Magufuli kwa maamuzi aliyoyachukua dhidi ya ACACIA! Wananchi hao walisikika wakisema "Haiwezekani kila sie tunapogundua tunafukuzwa eti ni eneo la ACACIA, kumbe nae hana leseni kama sisi, asante Magufuli"!
Wakati wakiendelea na kuchimba gari za POLISI zipatazo tatu zikiwapo na gari za ACACIA zilifika katika eneo hilo na kuanza kupiga mabomu hali ilisababisha na kutawanyika kwa wachimbaji hao.
Kwa mujibu wa polisi wanadai hawaruhusu mtu kuchimba katika eneo hilo kwani ni eneo la mwekezaji!