Bulyanhulu: Wachimbaji wadogo wapigwa mabomu walipotaka kuchimba karibu na mgodi wa ACACIA

jmchimbadhahabu

JF-Expert Member
Sep 26, 2014
218
106
Hii imetokea siku ya leo asubuhi ambapo baadhi ya wananchi kwenda kuchimba katika eneo la NAMBA 2 ambalo lipo karibu na mgodi wa ACACIA Bulyanhulu wilayani Kahama.

Mamia ya vijana,wazee na akina mama walionekana kumiminika katika eneo hilo na kuanza kuchimba huku wakiimba nyimbo za kumsifu Rais Magufuli kwa maamuzi aliyoyachukua dhidi ya ACACIA! Wananchi hao walisikika wakisema "Haiwezekani kila sie tunapogundua tunafukuzwa eti ni eneo la ACACIA, kumbe nae hana leseni kama sisi, asante Magufuli"!

Wakati wakiendelea na kuchimba gari za POLISI zipatazo tatu zikiwapo na gari za ACACIA zilifika katika eneo hilo na kuanza kupiga mabomu hali ilisababisha na kutawanyika kwa wachimbaji hao.

Kwa mujibu wa polisi wanadai hawaruhusu mtu kuchimba katika eneo hilo kwani ni eneo la mwekezaji!
 
Mwekezaji mxenge sana huyo.., hana leseni anafukuza tu watu kienyeji.., huyo polisi msaliti atumbuliwe mara moja! kampuni yenyewe haina usajili
 
"""Kwa mujibu wa polisi wanadai hawaruhusu mtu kuchimba katika eneo hilo kwani ni eneo la mwekezaji"""
Halafu raisi anasema jamaa hawana leseni Imekuwaje tena n eneo Lao????
 
Ha ha ha ha
Hiyo ndiyo ccm, walidhani watachimba? Acacia wapo kihalali na wanatambulika. Viongozi wa CCM na serikali yake walijichanganya kwenye mikataba mibovu.
Nenda kachimba, utapigwa risasi na kesi hakuna. Maghhufuli anawadanya nao wanajaa mazima.
Huyu huyu maghhhuufuli ndiyo alikuwa front seat kbsa huku akipiga meza ndiyo ndiyo ndiyo
Mjidanganye. Kwa utawala ccm. Acacia wanachimba madini kama kawaida.
 
Wananchi msifate bendera za wanasiasa.. Mtakufa, kesho watawakataa hao
 
yani kabisa kuna mafala wa acacia ambao pia wanashirikiana na polisi kuwajeruhi wananchi?
daah polisi wetu, mbona mnatuaibisha hivyo?
 
Back
Top Bottom