Bulembo atingisha Chato, mkurugenzi wa ulinzi na usalama CHADEMA ahamia CCM

Hivi mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa CHADEMA si LWAKATARE???

Hicho cheo mbona kipya??? Haaaaaa

Halafu si Kuna malaika mwenye heri alizuia siasa mpaka 2020??? Nini kimetokea???
7aa8850b0677929680b166073d88b68f.jpg
 
Tusikae kulalamika lalamika kama watoto wajameni. Siasa za majukwani ndio hazina budi kusitishwa. Lakini siasa kama hizi za kukutana ndani ya chama ndani ya ukumbi nani amekatazwa. Siasa kama kamati kuu ya chadema iliyokutana dodoma mbona haikukatazwa. Kwa nini msifuate mtindo huu wa kistaarabu. Saiz hatutaki makelel mitaani kamanda tunajenga uchumi wa taifa na wetu mmojammoja
c4d287073354b999415d81811e1f6395.jpg
 
Tungejikita hasa kuangalia kipi kilichompeleka Bulembo huko chato na manufaa yake kwa wananchi ingekuwa poa kabisa. Sasa hii sijui fulani kahamia kijannjano kutumalizia muda na akili zetu ni upuuzi tu.

Walishahama wangapi kutoka chadema kwenda kijanjano? Na walishahama wangapi kutoka kijanjano kwenda chadema?
 
Chama kinachotawala ndicho kinachoratibu misingi ya nchi. Ccm hawafanyi siasa za uchaguzi..wanahimiza utendaji kazi
Unajua tofauti ya serikali na chama?? Kwani chadema hawana majimbo na halmashauri ambazo wanatakiwa kuhimiza utendaji kazi maana zipo chini yao????? Au misingi ni ccm tu
 
Kumbuka ni std VII. Sina uhakika sana kama ataelewa hii lugha
Kuna ras hapa mtaani anapiga kiingereza cha ki Jamaica ,cha kiingereza na cha USA na shule hana

Hebu tofautisha lugha na masomo ,lugha yeyote anaweza kujua akifahamu tu ..

Kuna chalii yangu std7 alikataa kwenda seco lakini cha kushangaza akawa anawafundisha wanafunzi wa seco ngeli
 
Wenyewe wapo busy na Anna Nghwira. Kila ofisi anayoingia lazima walete update, huku Bulembo anawavuna wanachama wao tu.
Mghwira keshashirikiana na dikteta kuzuia mikutano ya kisiasa..... naye tutamshtaki kwa wananchi 2020 ili wawaadhibu wasaliti wakubwa nyie
 
Kilichofanywa na Bulembo ni kikao cha ndani, sio mkutano wa hadhara,vikao vya ndani vimeruhusiwa kwa vyama vyote.Acha kupotosha umma.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alahj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Chato, Wajumbe wa Mabaraza ya Juuia za CCM, Madiwani, Mabalozi na Watendaji wa Serikali, katika Ofisi ya CCM ya Wilaya hiyo mkoani Geita, leo Juni 9, 2017.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimpongeza Joseph Chacha ambaye alitangaza kuhamia CCM wakati wa kikao hicho. Chacha alikuwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema katika Wilaya za Geita na Chato.
Mtabadirisha watu kwa rangi za sare zenu lakini asilani, Mioyo ya watu hamtaibadilisha,,
 
Congratulation Hon MP however I have an opinion if we really need opposition parties in the Country to me I would we could have back to single party may be Later Our Children would by then Think of bringing them back I could see these parties divide us more than they Unite Us I may be wrong but these I my Opinions welcome let me here from You
Tumia tu Kiswahili au hata kiluga basi make kwa hali hii nina uhakika 100% kuwa hata wewe hujui unachomaanisha. Nyie ndo wale mkiombwa vyeti mnakimblia kudai vililiwa na panya kwenye nyumba ya Bibi. Very pathetic. Bashite-type.
 
Mghwira keshashirikiana na dikteta kuzuia mikutano ya kisiasa..... naye tutamshtaki kwa wananchi 2020 ili wawaadhibu wasaliti wakubwa nyie
Jitahidi.
Mara nyingi wapambe kama wewe ACT huwa tunawapenda sana.
Hongera mtumishi wa Mbowe.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alahj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Chato, Wajumbe wa Mabaraza ya Juuia za CCM, Madiwani, Mabalozi na Watendaji wa Serikali, katika Ofisi ya CCM ya Wilaya hiyo mkoani Geita, leo Juni 9, 2017.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimpongeza Joseph Chacha ambaye alitangaza kuhamia CCM wakati wa kikao hicho. Chacha alikuwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema katika Wilaya za Geita na Chato.

Huyu bulembo ana vyeti???
 
Back
Top Bottom