Bulaya: Makonda amenipigia simu na kudai wabunge sio chochote kwake, yupo karibu na bwana mkubwa

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Wabunge Ester Bulaya na Msukuma wamemshambulia tena mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda bungeni leo

Bulaya amedai Makonda amekuwa akiwapa vitisho wabunge wa upinzania akisema ataendelea kuwachafua kadri apendavyo kwa kuwa yupo karibu na bwana mkubwa.

Bulaya amedai Makonda alimpigia simu na kudai atawashughulikia kwa kuwa wao sio chochote kwake, na kuwauliza kuwa wanashangaa nini yeye kwenda Marekani na wabunge hawana akili



Musukuma nae amemshambulia vikali Makonda akidai yeye ndiye aliyetajwa kuwa ni mchekeshaji, lakini amesema hajawahi kusinzia na ameshinda ubunge kwa kuwashinda maprofesa wengi
 
Back
Top Bottom