Bulaya: Mafunzo ya kutumia silaha kwa JKT yatolewe kwa Vijana wachache ili kupunguza wanaokosa kazi na kufanya uhalifu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Mbunge wa viti maalum, Ester Bulaya ameishauri Serikali ya Tanzania kutoa mafunzo ya kutumia silaha kwa vijana wachache wanaoshiriki mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) badala ya kuwafundisha wengi.

Bulaya amesema kutoa mafunzo ya silaha kwa vijana wengi wakati hawapati nafasi za kujiunga na jeshi hilo, baadhi si waaminifu wanaweza kutumia mafunzo hayo kufanya uhalifu.

Bulaya ameeleza hayo leo Jumatano Machi 31, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akimuuliza swali la nyongeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa.

Katika majibu yake Kwandikwa amesema jeshi hutoa mafunzo ya silaha kwa vijana katika idadi inayotakiwa na kwamba hakuna shida katika jambo hilo.

Amesema mafunzo ya JKT yanalenga kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea badala ya kuajiriwa, kwamba jeshi linafanya tathmini ya kuboresha zaidi mafunzo hayo.

Wakati huohuo, Serikali imetoa sababu za kuwarudisha nyumbani mapema vijana waliokuwa kwenye mafunzo ya JKT.

Kwandikwa ametaja sababu hizo ni kuangalia mtaala utakaosaidia kuboresha mafunzo na kuangalia muda wa mafunzo ya miezi mitatu ya waliomaliza kidato cha sita yafikie mwaka mmoja na kuwafanya vijana wapate ujuzi wa kujitegemea.

Chanzo: Mwananchi
 
Badala ya kushauri itatue tatizo la ajira anashauri kitu kingine kabisa. Vijana wataingia kwenye uhalifu si kwa sababu wanamafunzo ya kutumia silaha ni sababu hawana ajira.
 
Hahahahahahahahahaha kudadeki bulaya angekuwa

Israel au North Korea
Angeomba jeshilifutwe
 
Ajira hili neno limesikika mara nyingi tangu 2016........
hivi kwann mtaala wa elimu usibadilishwe.... Elimu itolewe kulingan na mazingira yetu... Iwe applicable kweny mazingira yetu.. Vijana wakihitimu wajiaajiriii..
Serikali itengeneze uchumi wa kijasiliamali... Iboreshe masoko ya vitu mbalimbali watu wakazamie huko......
 
Ujinga mtupu badala ya kutafuta namna ya kuwatumia vijana kwenye shughuli za kimaendeleo mnawaza kuwanyima mafunzo ili wakikosa ajira wasiwe waarifu.
 
Bulaya umefanya research kwamba chanzo kikuu ( Over 50%) cha uhalifu kwa vijana wanatumia Silaha ni waliotoka JKT ?

Kama huna evidence basi hoja yako ni void.
 
Mbunge wa viti maalum, Ester Bulaya ameishauri Serikali ya Tanzania kutoa mafunzo ya kutumia silaha kwa vijana wachache wanaoshiriki mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) badala ya kuwafundisha wengi.

Bulaya amesema kutoa mafunzo ya silaha kwa vijana wengi wakati hawapati nafasi za kujiunga na jeshi hilo, baadhi si waaminifu wanaweza kutumia mafunzo hayo kufanya uhalifu.

Bulaya ameeleza hayo leo Jumatano Machi 31, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akimuuliza swali la nyongeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa.

Katika majibu yake Kwandikwa amesema jeshi hutoa mafunzo ya silaha kwa vijana katika idadi inayotakiwa na kwamba hakuna shida katika jambo hilo.

Amesema mafunzo ya JKT yanalenga kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea badala ya kuajiriwa, kwamba jeshi linafanya tathmini ya kuboresha zaidi mafunzo hayo.

Wakati huohuo, Serikali imetoa sababu za kuwarudisha nyumbani mapema vijana waliokuwa kwenye mafunzo ya JKT.

Kwandikwa ametaja sababu hizo ni kuangalia mtaala utakaosaidia kuboresha mafunzo na kuangalia muda wa mafunzo ya miezi mitatu ya waliomaliza kidato cha sita yafikie mwaka mmoja na kuwafanya vijana wapate ujuzi wa kujitegemea.

Chanzo: Mwananchi

"UHALIFU NI NINI?​

Uhalifu ni utendaji wa jambo lolote lililokatazwa kutendwa Kisheria au kwa sheria ndogondogo(By Laws) za Mtaa,Kijiji,Kitongoji,Kata/Shehia, Halmashauri au nchi."

Bulaya naye ni mmoja wa wahalifu, aane kwanza kujihukumu yeye
 
Mbunge wa viti maalum, Ester Bulaya ameishauri Serikali ya Tanzania kutoa mafunzo ya kutumia silaha kwa vijana wachache wanaoshiriki mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) badala ya kuwafundisha wengi.

Bulaya amesema kutoa mafunzo ya silaha kwa vijana wengi wakati hawapati nafasi za kujiunga na jeshi hilo, baadhi si waaminifu wanaweza kutumia mafunzo hayo kufanya uhalifu.

Bulaya ameeleza hayo leo Jumatano Machi 31, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akimuuliza swali la nyongeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa.

Katika majibu yake Kwandikwa amesema jeshi hutoa mafunzo ya silaha kwa vijana katika idadi inayotakiwa na kwamba hakuna shida katika jambo hilo.

Amesema mafunzo ya JKT yanalenga kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea badala ya kuajiriwa, kwamba jeshi linafanya tathmini ya kuboresha zaidi mafunzo hayo.

Wakati huohuo, Serikali imetoa sababu za kuwarudisha nyumbani mapema vijana waliokuwa kwenye mafunzo ya JKT.

Kwandikwa ametaja sababu hizo ni kuangalia mtaala utakaosaidia kuboresha mafunzo na kuangalia muda wa mafunzo ya miezi mitatu ya waliomaliza kidato cha sita yafikie mwaka mmoja na kuwafanya vijana wapate ujuzi wa kujitegemea.

Chanzo: Mwananchi
Kumbe bado wapo bungeni wanakula posho na mishahara aisee
 
Bulaya umefanya research kwamba chanzo kikuu ( Over 50%) cha uhalifu kwa vijana wanatumia Silaha ni waliotoka JKT ?

Kama huna evidence basi hoja yako ni void.
Kuna mtu ambaye ametaka kuwa jambazi akashindwa kwa sababu hana mafunzo ya silaha? Kutumia bunduki kwa uhalifu mbona ni mtu yoyote anaweza kujifunza? Hivi anafikiri majambazi hayapeani mafunzo?
 
Mbunge wa viti maalum, Ester Bulaya ameishauri Serikali ya Tanzania kutoa mafunzo ya kutumia silaha kwa vijana wachache wanaoshiriki mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) badala ya kuwafundisha wengi.

Bulaya amesema kutoa mafunzo ya silaha kwa vijana wengi wakati hawapati nafasi za kujiunga na jeshi hilo, baadhi si waaminifu wanaweza kutumia mafunzo hayo kufanya uhalifu.

Bulaya ameeleza hayo leo Jumatano Machi 31, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akimuuliza swali la nyongeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa.

Katika majibu yake Kwandikwa amesema jeshi hutoa mafunzo ya silaha kwa vijana katika idadi inayotakiwa na kwamba hakuna shida katika jambo hilo.

Amesema mafunzo ya JKT yanalenga kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea badala ya kuajiriwa, kwamba jeshi linafanya tathmini ya kuboresha zaidi mafunzo hayo.

Wakati huohuo, Serikali imetoa sababu za kuwarudisha nyumbani mapema vijana waliokuwa kwenye mafunzo ya JKT.

Kwandikwa ametaja sababu hizo ni kuangalia mtaala utakaosaidia kuboresha mafunzo na kuangalia muda wa mafunzo ya miezi mitatu ya waliomaliza kidato cha sita yafikie mwaka mmoja na kuwafanya vijana wapate ujuzi wa kujitegemea.

Chanzo: Mwananchi
inasikitisha kuwa na wwapinzani wa namna hii yani ndo waliwataka hawa wawe wakosoaji wa serikali
 
Back
Top Bottom