Bulawayo, Zimbabwe 1993

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,907
30,249
BULAWAYO, ZIMBABWE 1993

Angalia picha hapo chini niko Bulawayo chini ya kibao na nyingine kipo kibao kitupu.

Hiyo ambayo nipo chini ya kibao nilipiga Bulawayo mwaka wa 1993 na hiyo nyingine kapiga ndugu yangu mmoja mwaka huu baada ya kuona picha hiyo ya kwanza.

Kaniambia anataka nirudishe kumbukumbu zangu za miaka 29 iliyopita.

Nilifika Bulawayo mwaka wa 1993 nikitokea Harare ambako ndiko nilipopiga kambi.

Ulikuwa mwezi wa Ramadhani na kuna kisa nilipata kueleza kuhusu hoteli ambayo nilifikia nikahama baada ya kuletewa futari ambayo waliweka na nguruwe si kwa makusudi bali kwa kutokujua.

Hoteli hii jina lake Ambassador Hotel.

Hii hoteli ina historia kubwa na wazalendo wawili wa Tanganyika Ally Sykes na Denis Phombeah.

Kuna mkasa wa Ally Sykes na Denis Phombeah walipokuwa wanakwenda Lusaka, Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa wapigania uhuru wa Afrika Chini ya Sahara.

Wazalendo hawa walibuku kukaa hoteli hii wakati wakiwa njiani kwenda Lusaka, Southern Rhodesia.

Hawakulala hoteli hii kwa kuwa walikamatwa uwaja wa ndege na wakapigwa PI yaani wahamiaji wasiotakiwa warudi walikotoka na usiku ule wakafungiwa kwenye banda la nguruwe walale hadi asubuhi warudishwe Tanganyika.

Siku ya pili nikahama nikahamia Holiday Inn baada ya kuona nguruwe kwenye futari yangu.

Usiogope ukadhani hii ni ile Holiday Inn hoteli ya Nyota Tano sawa na ile ya Marekani na kwengineko kwenye miji mikubwa duniani.

Afrika na sisi tuna ujanja wetu wa kucheza na haya majina maarufu kuvutia biashara.

Nimewahi vilevile kulala Holiday Inn Port Said Misri.
Ni janja hiyo hiyo.

Lakini si kuwa hizi ni hoteli mbovu.
Ni hoteli nzuri lakini si kama ile yenyewe Holiday Inn ya kikwelikweli.

Mji wa Bulawayo unanikumbusha George Sibanda ambae alikuwa mwanamuziki maarufu sana na muziki wake ukipigwa Sauti ya Dar es Salaam wakati wa utoto wangu katika miaka ya 1950.

Tukimsikiliza pia George Sibanda katika gramaphone majumbani kwetu.
Kwa ajili hii nikaamua kwenda kuutembelea mji huu.

Nilipopanda basi kuelekea Bulawayo kuna kitu kikanikumbusha Dar es Salaam ya zamani enzi za Dar es Salaam Motor Transport (DMT).

Nimepanda basi dereva kavaa unifomu ya khaki, kafunga tai na kavaa kofia anaonekana nadhifu kabisa.

Halikadhalika na konda wake yaani ''conducter'' wa basi kavaa shati safi la blue na kafunga tai.

Basi halisimami ovyo njiani kuna vituo maalum na linasimama sehemu zote za vituo kuna vyoo visafi na sehemu ya abiria kupata vinywaji na chakula.

Haya ndiyo niliyoyaona katika safari yangu nikielekea Bulawayo mji mkubwa wa pili kufuatia Harare, mji wa George Sibanda ambae nilipokuwa mdogo nikiimba nyimbo zake za Kishona lau kama siijui lugha hiyo.

Huyu George Sibanda kipaji chake kiliibuliwa na Hugh Tracey ambae alikuwa akizunguka katika makoloni akirekodi miziki ya Waafrika.

Hugh Tracey ndiye pia alimuibua Mwenda Jean Bosco mpiga gitaa maarufu kutoka Congo.

Nakumbuka watu wakimmwita George Sibanda wa Bulawayo.

Nilikuja kukutana na Hugh Tracey katika Nyaraka za Sykes wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes.

Hiki nacho ni kisa kinachohitaji kuhadithiwa kwa wakati wake maalum.

Kisa hiki kinamuhusu Joseph Kasella Bantu na Hugh Tracey kutokana na ugomvi wao ulioanzia Afrika ya Kusini katika miaka ya 1940s.

Kuna senema ilitengenezwa bila shaka Afrika Kusini katika miaka hiyo.
Filamu hii ilikuwa inatangaza sigara.

Filamu hii ikionyeshwa katika viwanja vya wazi naamini Tanganyika nzima kutangaza biashara mbalimbali moja ikiwa ''Sportsman Cigarette,'' iliyokuwa ikitengenezwa na kampuni ya British American Tobacco.

Filamu hii ikionyeshwa Mnazi Mmoja na Magomeni kila mwezi pamoja na filamu nyingine za cowboys na za Chale Mnene na Chale Mwembamba - Stan Laurel na Oliver Hardy.

Watoto tukizipenda sana filamu hizi.

Hii filamu ya kutangaza sigara ilikuwa na nyimbo yake watoto wote tukiijua tukiimba.

Stori ya senema hii ni mtu kutoka shamba aliyekuwa na kipaji cha kupiga guitar anafika mjini pengine Salisbury (Harare) kisha anaibiwa guitar lake.

Anamkimbiza mwizi wake hadi anamkamata na hizi mbio sehemu moja inakuwa ndani ya soko.

Senema ya kuwafurahisha watoto jinsi meza za sokoni zilizokuwa na bidha zilivyokuwa zikipinduliwa.

Mimi nilikuwa naipenda sehemu ya mwisho ya filmu hii ambako huyu jamaa yuko nyuma ya pick up na guitar lake anapiga na kuimba baada ya kumtia mkononi mwizi wake na kulipata gitaa lake.

Nyimbo ambayo alikuwa akiimba ilikuwa na kiitikio, ''sigareti, sigareti, sigareti.''

Sehemu ya mwisho ya nyimbo hii anapiga guitar haimbi hapo inaingia flute (fiimbi) ya Spokes Mashiane mpiga filimbi maarufu aliyekuwa na kipaji cha juu sana.

Hapa ndipo palipokuwa pakinisuuza mimi.
Muziki aliokuwa akipiga ukiitwa Kwela.

Mimi nilikuwa napiga filimbi udogoni na waliokuwa wakinisikiliza walikuwa wanasema nampatia sana Spokes Mashiane.

Nyimbo hizi zilikuwa maarufu sana Tanganyika na zaidi Kenya na zikipigwa sana Voice of Kenya (VOK).

Kenya wakatokea wapigaji wengi sana wa magita kwa mtindo wa George Sibanda.

Tanganyika muziki uliopendwa ulikuwa ni wa Congo ukirekodiwa na kampuni maarufu ya Loningisa na nyimbo za Congo zikijulikana kwa namba zake kama Loni 1, 2,3 nk.

''Loni,'' ikiwa na maana Loningisa.

Baba yangu siku nilipomweleza kuhusu senama hii akaniambia kuwa hiyo nyimbo inayoimbwa, ''sigareti, sigareti,'' huyo ni George Sibanda.

Hiyo filimbi mpigaji ni Spokes Mashiane.
Spokes Mashiane yeye alikuwa kutoka Johannesburg.

Nilijaaliwa kufika Johannesburg mji ambao historia yake ya miaka ya 1950 ni ya kipekee sana kiasi wote watu wa Afrika Kusini wanasema kubadili jina la mji huo ni kupoteza historia yake yote kwa ukamilifu.

Huu ndiyo ulikuwa mji wa Spokes Mashiane, Miriam Makeba na Nelson Mandela pia.

Lakini vilevile huu ni mji wa Jim Bailey na gazeti lake la Drum.
Jim Bailey ana historia ya kuvutia.

Afrika Kusini imetengeneza filamu ya maisha ya Jim Bailey na gazeti lake.
Filamu hii inaitwa ''Drum.''

Filamu hii inatosha kukufunza maisha yalikuwaje nyakati zile na upekee wa Jim Bailey ukimlinganisha na Wazungu wenzake wabaguzi.

Nitaweka link ya movie hii mpate kuiona na kuisikia miziki ya Afrika Kusini ya miaka ya 1950.

Nilikuja kufahamiana na Jim Bailey miaka ya 1980 ambae nilijulishwa kwake na Ally Sykes.

Hiki ni kisa kingine kinachohitaji muda wa peke yake kukieleza.

Halikadhalika Johannesburg ulikuwa mji wa Dorothy Masuka ingawa asili yake yeye kazaliwa wa Bulawayo.

Kuna wakati ilikuwa vigumu kusema nani kamzidi mwenzake katika uimbaji kati ya Miriam Makeba na Dorothy Masuka.

Dorothy Masuka akapotea Afrika ya Mashariki ingawa aliendelea kuwapo jukwaani.

Kuna jambo la kushangaza lilinitokea mwaka 2000 katika safari yangu ya kwanza kwenda Johannesburg.

Nilipata taarifa ya kifo cha Jim Bailey ndani ya ndege katika mazungumzo ya kawaida na Mzungu mmoja Mwafrika Kusini.

Huyu bwana katika mazungumzo nilimwambia kuwa Johannesburg napita njia safari yangu ni Manzini, Swaziland lakini nikimaliza shughuli zangu nitakwenda Johannesburg kumuona Jim Bailey.

Alishangaa vipi nimemjua Jim Bailey.

Akanipa pole akanieleza kuwa Bailey amefariki mwezi uliopita na walikuwa majirani.

Huyu bwana akanishauri kuwa nisipande ndege kuja Johannesburg nipande mabasi madogo yanaitwa, ''Kubi,'' kutoka Mbabane ili nipite Kwa Zulu Natal niione Afrika Kusini.

Akaniambia kuwa basi hili litanifikisha Durban na nitaweza kukaa hapo siku mbili tatu hivi kuona mji.

Huyu bwana akanieleza kitu kingine akanielekeza hoteli nzuri ya kufikia akanambia kuwa hizo ni ''chain of hotels.'' ziko karibu miji yote mikubwa ya Afrika Kusini na huwa ziko barabara kuu wepesi kufikika na nikipanda ''kubi'' itanishusha mlangoni hotelini.

Nilipita Kwa Zulu Natal na sikujuta kufuata ushauri wa yule rafiki yangu.

Hapa ndipo niliposema hapo juu kuwa nilikutana na mambo ya kushangaza.

Nilipoingia chumbani kwangu hapo hotelini Durban nikawasha TV.

Naona kipindi cha Dorothy Masuka sasa mtu mzima anafanyiwa mahojiano anaeleza maisha yake.

Ndipo nikamsikia akieleza siku zake za ujana yeye na Miriam Makeba wakiwa marafiki wakubwa wanaanza muziki wao.

Ilikuwa miaka mingi sikupata kumsikia Dorothy Masuka.

Kipindi kile kikarejesha kumbukumbu zangu za hawa waimbaji wawili kutoka Afrika Kusini.

Nyimbo zao nyakati zile zilikuwa maarufu sana Tanganyika.
Kifo cha Jim Bailey nimekisikia kweye ndege nakuja Afrika Kusini.

Nafika Durban namuona Dorothy Masuka baada ya kupotea katika fikra zangu kwa miaka mingi sana.

Kusafiri ni elimu tosha.
View attachment 2271465
View attachment 2271468
View attachment 2271469
 
Umenikumbusha Zimbabwe, nakumbuka mwaka 1996 Zimbabwe walikuwa wanatumia sarafu mbili, Zim dollar na kwacha ya Zimbabwe.

Basi nilipokuwa jijini harare in transit niliingia take away nikatowa noti ya Zim dollar moja nikanunuwa hot dog na coca-cola can then nikarudishiwa chenji ya kwacha nilistaajabu sana.

Zim dollar ilikuwa powerful sana kipindi hicho, ndio maana tuliowahi kufika Zimbabwe kipindi hicho tukiiona Zimbabwe ya sasa lazima usikitike.

Nakumbuka niliingia Johannesburg na kuchenji dollar kwa magendo maana sikuona bereau de change dollar moja ilikuwa exchange rate yake sawa na rand 4 .

Mpaka sasa huwa nashindwa kujuwa tatizo la ngozi nyeusi ni nini? Kwa nini wazungu wanaweza sisi tunashindwa? Na haya yote hayajafanyika ulaya ni hapa kwetu Africa.
 
Tatizo letu weusi ni kubwa kwanza atukuwa tayari kujitawala Trump alikuwa sahihi juu yetu watu weusi...
 
Umenikumbusha Zimbabwe, nakumbuka mwaka 1996 Zimbabwe walikuwa wanatumia sarafu mbili, Zim dollar na kwacha ya Zimbabwe.

Basi nilipokuwa jijini harare in transit niliingia take away nikatowa noti ya Zim dollar moja nikanunuwa hot dog na coca-cola can then nikarudishiwa chenji ya kwacha nilistaajabu sana.

Zim dollar ilikuwa powerful sana kipindi hicho, ndio maana tuliowahi kufika Zimbabwe kipindi hicho tukiiona Zimbabwe ya sasa lazima usikitike.

Nakumbuka niliingia Johannesburg na kuchenji dollar kwa magendo maana sikuona bereau de change dollar moja ilikuwa exchange rate yake sawa na rand 4 .

Mpaka sasa huwa nashindwa kujuwa tatizo la ngozi nyeusi ni nini? Kwa nini wazungu wanaweza sisi tunashindwa? Na haya yote hayajafanyika ulaya ni hapa kwetu Africa.
Yes mkuu ukipita leo pale Harare au Bulawayo ndio utatambua kuwa lizards 🦎 ni tofauti kabisa na crocodiles 🐊, nchi imekuwa https://jamii.app/JFUserGuide up chini ya dictator mugabe na ndio maana 24%wa illegal immigrants ndani y SA ni wazimbabwe, what's will happen after 31st.dec.2022 only GOD knows kuhusu wakimbizi hawa.
 
BULAWAYO, ZIMBABWE 1993

Angalia picha hapo chini niko Bulawayo chini ya kibao na nyingine kipo kibao kitupu.

Hiyo ambayo nipo chini ya kibao nilipiga Bulawayo mwaka wa 1993 na hiyo nyingine kapiga ndugu yangu mmoja mwaka huu baada ya kuona picha hiyo ya kwanza.

Kaniambia anataka nirudishe kumbukumbu zangu za miaka 29 iliyopita.

Nilifika Bulawayo mwaka wa 1993 nikitokea Harare ambako ndiko nilipopiga kambi.

Ulikuwa mwezi wa Ramadhani na kuna kisa nilipata kueleza kuhusu hoteli ambayo nilifikia nikahama baada ya kuletewa futari ambayo waliweka na nguruwe si kwa makusudi bali kwa kutokujua.

Hoteli hii jina lake Ambassador Hotel.

Hii hoteli ina historia kubwa na wazalendo wawili wa Tanganyika Ally Sykes na Denis Phombeah.

Kuna mkasa wa Ally Sykes na Denis Phombeah walipokuwa wanakwenda Lusaka, Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa wapigania uhuru wa Afrika Chini ya Sahara.

Wazalendo hawa walibuku kukaa hoteli hii wakati wakiwa njiani kwenda Lusaka, Southern Rhodesia.

Hawakulala hoteli hii kwa kuwa walikamatwa uwaja wa ndege na wakapigwa PI yaani wahamiaji wasiotakiwa warudi walikotoka na usiku ule wakafungiwa kwenye banda la nguruwe walale hadi asubuhi warudishwe Tanganyika.

Siku ya pili nikahama nikahamia Holiday Inn baada ya kuona nguruwe kwenye futari yangu.

Usiogope ukadhani hii ni ile Holiday Inn hoteli ya Nyota Tano sawa na ile ya Marekani na kwengineko kwenye miji mikubwa duniani.

Afrika na sisi tuna ujanja wetu wa kucheza na haya majina maarufu kuvutia biashara.

Nimewahi vilevile kulala Holiday Inn Port Said Misri.
Ni janja hiyo hiyo.

Lakini si kuwa hizi ni hoteli mbovu.
Ni hoteli nzuri lakini si kama ile yenyewe Holiday Inn ya kikwelikweli.

Mji wa Bulawayo unanikumbusha George Sibanda ambae alikuwa mwanamuziki maarufu sana na muziki wake ukipigwa Sauti ya Dar es Salaam wakati wa utoto wangu katika miaka ya 1950.

Tukimsikiliza pia George Sibanda katika gramaphone majumbani kwetu.
Kwa ajili hii nikaamua kwenda kuutembelea mji huu.

Nilipopanda basi kuelekea Bulawayo kuna kitu kikanikumbusha Dar es Salaam ya zamani enzi za Dar es Salaam Motor Transport (DMT).

Nimepanda basi dereva kavaa unifomu ya khaki, kafunga tai na kavaa kofia anaonekana nadhifu kabisa.

Halikadhalika na konda wake yaani ''conducter'' wa basi kavaa shati safi la blue na kafunga tai.

Basi halisimami ovyo njiani kuna vituo maalum na linasimama sehemu zote za vituo kuna vyoo visafi na sehemu ya abiria kupata vinywaji na chakula.

Haya ndiyo niliyoyaona katika safari yangu nikielekea Bulawayo mji mkubwa wa pili kufuatia Harare, mji wa George Sibanda ambae nilipokuwa mdogo nikiimba nyimbo zake za Kishona lau kama siijui lugha hiyo.

Huyu George Sibanda kipaji chake kiliibuliwa na Hugh Tracey ambae alikuwa akizunguka katika makoloni akirekodi miziki ya Waafrika.

Hugh Tracey ndiye pia alimuibua Mwenda Jean Bosco mpiga gitaa maarufu kutoka Congo.

Nakumbuka watu wakimmwita George Sibanda wa Bulawayo.

Nilikuja kukutana na Hugh Tracey katika Nyaraka za Sykes wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes.

Hiki nacho ni kisa kinachohitaji kuhadithiwa kwa wakati wake maalum.

Kisa hiki kinamuhusu Joseph Kasella Bantu na Hugh Tracey kutokana na ugomvi wao ulioanzia Afrika ya Kusini katika miaka ya 1940s.

Kuna senema ilitengenezwa bila shaka Afrika Kusini katika miaka hiyo.
Filamu hii ilikuwa inatangaza sigara.

Filamu hii ikionyeshwa katika viwanja vya wazi naamini Tanganyika nzima kutangaza biashara mbalimbali moja ikiwa ''Sportsman Cigarette,'' iliyokuwa ikitengenezwa na kampuni ya British American Tobacco.

Filamu hii ikionyeshwa Mnazi Mmoja na Magomeni kila mwezi pamoja na filamu nyingine za cowboys na za Chale Mnene na Chale Mwembamba - Stan Laurel na Oliver Hardy.

Watoto tukizipenda sana filamu hizi.

Hii filamu ya kutangaza sigara ilikuwa na nyimbo yake watoto wote tukiijua tukiimba.

Stori ya senema hii ni mtu kutoka shamba aliyekuwa na kipaji cha kupiga guitar anafika mjini pengine Salisbury (Harare) kisha anaibiwa guitar lake.

Anamkimbiza mwizi wake hadi anamkamata na hizi mbio sehemu moja inakuwa ndani ya soko.

Senema ya kuwafurahisha watoto jinsi meza za sokoni zilizokuwa na bidha zilivyokuwa zikipinduliwa.

Mimi nilikuwa naipenda sehemu ya mwisho ya filmu hii ambako huyu jamaa yuko nyuma ya pick up na guitar lake anapiga na kuimba baada ya kumtia mkononi mwizi wake na kulipata gitaa lake.

Nyimbo ambayo alikuwa akiimba ilikuwa na kiitikio, ''sigareti, sigareti, sigareti.''

Sehemu ya mwisho ya nyimbo hii anapiga guitar haimbi hapo inaingia flute (fiimbi) ya Spokes Mashiane mpiga filimbi maarufu aliyekuwa na kipaji cha juu sana.

Hapa ndipo palipokuwa pakinisuuza mimi.
Muziki aliokuwa akipiga ukiitwa Kwela.

Mimi nilikuwa napiga filimbi udogoni na waliokuwa wakinisikiliza walikuwa wanasema nampatia sana Spokes Mashiane.

Nyimbo hizi zilikuwa maarufu sana Tanganyika na zaidi Kenya na zikipigwa sana Voice of Kenya (VOK).

Kenya wakatokea wapigaji wengi sana wa magita kwa mtindo wa George Sibanda.

Tanganyika muziki uliopendwa ulikuwa ni wa Congo ukirekodiwa na kampuni maarufu ya Loningisa na nyimbo za Congo zikijulikana kwa namba zake kama Loni 1, 2,3 nk.

''Loni,'' ikiwa na maana Loningisa.

Baba yangu siku nilipomweleza kuhusu senama hii akaniambia kuwa hiyo nyimbo inayoimbwa, ''sigareti, sigareti,'' huyo ni George Sibanda.

Hiyo filimbi mpigaji ni Spokes Mashiane.
Spokes Mashiane yeye alikuwa kutoka Johannesburg.

Nilijaaliwa kufika Johannesburg mji ambao historia yake ya miaka ya 1950 ni ya kipekee sana kiasi wote watu wa Afrika Kusini wanasema kubadili jina la mji huo ni kupoteza historia yake yote kwa ukamilifu.

Huu ndiyo ulikuwa mji wa Spokes Mashiane, Miriam Makeba na Nelson Mandela pia.

Lakini vilevile huu ni mji wa Jim Bailey na gazeti lake la Drum.
Jim Bailey ana historia ya kuvutia.

Afrika Kusini imetengeneza filamu ya maisha ya Jim Bailey na gazeti lake.
Filamu hii inaitwa ''Drum.''

Filamu hii inatosha kukufunza maisha yalikuwaje nyakati zile na upekee wa Jim Bailey ukimlinganisha na Wazungu wenzake wabaguzi.

Nitaweka link ya movie hii mpate kuiona na kuisikia miziki ya Afrika Kusini ya miaka ya 1950.

Nilikuja kufahamiana na Jim Bailey miaka ya 1980 ambae nilijulishwa kwake na Ally Sykes.

Hiki ni kisa kingine kinachohitaji muda wa peke yake kukieleza.

Halikadhalika Johannesburg ulikuwa mji wa Dorothy Masuka ingawa asili yake yeye kazaliwa wa Bulawayo.

Kuna wakati ilikuwa vigumu kusema nani kamzidi mwenzake katika uimbaji kati ya Miriam Makeba na Dorothy Masuka.

Dorothy Masuka akapotea Afrika ya Mashariki ingawa aliendelea kuwapo jukwaani.

Kuna jambo la kushangaza lilinitokea mwaka 2000 katika safari yangu ya kwanza kwenda Johannesburg.

Nilipata taarifa ya kifo cha Jim Bailey ndani ya ndege katika mazungumzo ya kawaida na Mzungu mmoja Mwafrika Kusini.

Huyu bwana katika mazungumzo nilimwambia kuwa Johannesburg napita njia safari yangu ni Manzini, Swaziland lakini nikimaliza shughuli zangu nitakwenda Johannesburg kumuona Jim Bailey.

Alishangaa vipi nimemjua Jim Bailey.

Akanipa pole akanieleza kuwa Bailey amefariki mwezi uliopita na walikuwa majirani.

Huyu bwana akanishauri kuwa nisipande ndege kuja Johannesburg nipande mabasi madogo yanaitwa, ''Kubi,'' kutoka Mbabane ili nipite Kwa Zulu Natal niione Afrika Kusini.

Akaniambia kuwa basi hili litanifikisha Durban na nitaweza kukaa hapo siku mbili tatu hivi kuona mji.

Huyu bwana akanieleza kitu kingine akanielekeza hoteli nzuri ya kufikia akanambia kuwa hizo ni ''chain of hotels.'' ziko karibu miji yote mikubwa ya Afrika Kusini na huwa ziko barabara kuu wepesi kufikika na nikipanda ''kubi'' itanishusha mlangoni hotelini.

Nilipita Kwa Zulu Natal na sikujuta kufuata ushauri wa yule rafiki yangu.

Hapa ndipo niliposema hapo juu kuwa nilikutana na mambo ya kushangaza.

Nilipoingia chumbani kwangu hapo hotelini Durban nikawasha TV.

Naona kipindi cha Dorothy Masuka sasa mtu mzima anafanyiwa mahojiano anaeleza maisha yake.

Ndipo nikamsikia akieleza siku zake za ujana yeye na Miriam Makeba wakiwa marafiki wakubwa wanaanza muziki wao.

Ilikuwa miaka mingi sikupata kumsikia Dorothy Masuka.

Kipindi kile kikarejesha kumbukumbu zangu za hawa waimbaji wawili kutoka Afrika Kusini.

Nyimbo zao nyakati zile zilikuwa maarufu sana Tanganyika.
Kifo cha Jim Bailey nimekisikia kweye ndege nakuja Afrika Kusini.

Nafika Durban namuona Dorothy Masuka baada ya kupotea katika fikra zangu kwa miaka mingi sana.

Kusafiri ni elimu tosha.
Yes kusafiri ni kujifunza sana,Nkanini anakusoma sana na kuelimika mno na mada zako,salute mkuu, yes Nami nimepita hivi karibuni pale Bulawayo,Harare,Chinoyi, yaani inasikitisha mno, mtu mweusi tunaongea sana na utendaji wetu ni mbovu na wa kizembe, miji yote ya Zimbabwe 🇿🇼 umeharibiwa na utawala wa 🦎, tujadili kwa facts ni nchi gani ya black peoples hapa duniani inayofanya vema kiuchumi, kidemokrasia?,huku SADC ni Botswana 🇧🇼 ,Namibia ambazo kidogo zinatutoa aibu, watch out Zambia 🇿🇲 wanakuja vizuri sana ,nchi imeanza kuonekana na haki za raia zinaheshimika, nchi yangu Tanzania 🇹🇿 tumsaidie sana our president ingawa amezungukwa na wadau wengi wa ccm wasiopenda mabadiliko, wao wanajipigania wao na koo zao . welldone mkuu kwa kunipa mada zenye mafundisho na rich history
 
Bulawayo nakumbuka film ya More time ya mwaka 93 kama sijakosea..
bibi yake na Thandiwe anamwambia Thandiwe kuwa hali ya ukimwi ni mbaya sana pale kijijini, na hata huko mjini bulawayo. ila pale kijijini hali ni mbaya zaidi maana hakuna hospitali.
 
Nimesoma ila sijaelewa lengo la uzi huu ni kutwambia wapi na wapi amefika na hotel au lengo ni lipi aliyeelewa anisaidie
 
Agresive,
Lengo ni kueleza ninayokumbuka kuhusu Bulawayo.

George Sibanda na muziki wake Tanganyika wakati mimi mtoto mdogo 1950s.

Kutokea hapo nimeeleza mambo mengi Jim Bailey, Hugh Tracey nk. nk.

Hii makala hukuipenda?
Mbona si ngumu kusomeka?

Lakini ukitaka kufaidika ingia Google na watafute hao niliowataja uwajue.
 
BULAWAYO, ZIMBABWE 1993

Angalia picha hapo chini niko Bulawayo chini ya kibao na nyingine kipo kibao kitupu.

Hiyo ambayo nipo chini ya kibao nilipiga Bulawayo mwaka wa 1993 na hiyo nyingine kapiga ndugu yangu mmoja mwaka huu baada ya kuona picha hiyo ya kwanza.

Kaniambia anataka nirudishe kumbukumbu zangu za miaka 29 iliyopita.

Nilifika Bulawayo mwaka wa 1993 nikitokea Harare ambako ndiko nilipopiga kambi.

Ulikuwa mwezi wa Ramadhani na kuna kisa nilipata kueleza kuhusu hoteli ambayo nilifikia nikahama baada ya kuletewa futari ambayo waliweka na nguruwe si kwa makusudi bali kwa kutokujua.

Hoteli hii jina lake Ambassador Hotel.

Hii hoteli ina historia kubwa na wazalendo wawili wa Tanganyika Ally Sykes na Denis Phombeah.

Kuna mkasa wa Ally Sykes na Denis Phombeah walipokuwa wanakwenda Lusaka, Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa wapigania uhuru wa Afrika Chini ya Sahara.

Wazalendo hawa walibuku kukaa hoteli hii wakati wakiwa njiani kwenda Lusaka, Southern Rhodesia.

Hawakulala hoteli hii kwa kuwa walikamatwa uwaja wa ndege na wakapigwa PI yaani wahamiaji wasiotakiwa warudi walikotoka na usiku ule wakafungiwa kwenye banda la nguruwe walale hadi asubuhi warudishwe Tanganyika.

Siku ya pili nikahama nikahamia Holiday Inn baada ya kuona nguruwe kwenye futari yangu.

Usiogope ukadhani hii ni ile Holiday Inn hoteli ya Nyota Tano sawa na ile ya Marekani na kwengineko kwenye miji mikubwa duniani.

Afrika na sisi tuna ujanja wetu wa kucheza na haya majina maarufu kuvutia biashara.

Nimewahi vilevile kulala Holiday Inn Port Said Misri.
Ni janja hiyo hiyo.

Lakini si kuwa hizi ni hoteli mbovu.
Ni hoteli nzuri lakini si kama ile yenyewe Holiday Inn ya kikwelikweli.

Mji wa Bulawayo unanikumbusha George Sibanda ambae alikuwa mwanamuziki maarufu sana na muziki wake ukipigwa Sauti ya Dar es Salaam wakati wa utoto wangu katika miaka ya 1950.

Tukimsikiliza pia George Sibanda katika gramaphone majumbani kwetu.
Kwa ajili hii nikaamua kwenda kuutembelea mji huu.

Nilipopanda basi kuelekea Bulawayo kuna kitu kikanikumbusha Dar es Salaam ya zamani enzi za Dar es Salaam Motor Transport (DMT).

Nimepanda basi dereva kavaa unifomu ya khaki, kafunga tai na kavaa kofia anaonekana nadhifu kabisa.

Halikadhalika na konda wake yaani ''conducter'' wa basi kavaa shati safi la blue na kafunga tai.

Basi halisimami ovyo njiani kuna vituo maalum na linasimama sehemu zote za vituo kuna vyoo visafi na sehemu ya abiria kupata vinywaji na chakula.

Haya ndiyo niliyoyaona katika safari yangu nikielekea Bulawayo mji mkubwa wa pili kufuatia Harare, mji wa George Sibanda ambae nilipokuwa mdogo nikiimba nyimbo zake za Kishona lau kama siijui lugha hiyo.

Huyu George Sibanda kipaji chake kiliibuliwa na Hugh Tracey ambae alikuwa akizunguka katika makoloni akirekodi miziki ya Waafrika.

Hugh Tracey ndiye pia alimuibua Mwenda Jean Bosco mpiga gitaa maarufu kutoka Congo.

Nakumbuka watu wakimmwita George Sibanda wa Bulawayo.

Nilikuja kukutana na Hugh Tracey katika Nyaraka za Sykes wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes.

Hiki nacho ni kisa kinachohitaji kuhadithiwa kwa wakati wake maalum.

Kisa hiki kinamuhusu Joseph Kasella Bantu na Hugh Tracey kutokana na ugomvi wao ulioanzia Afrika ya Kusini katika miaka ya 1940s.

Kuna senema ilitengenezwa bila shaka Afrika Kusini katika miaka hiyo.
Filamu hii ilikuwa inatangaza sigara.

Filamu hii ikionyeshwa katika viwanja vya wazi naamini Tanganyika nzima kutangaza biashara mbalimbali moja ikiwa ''Sportsman Cigarette,'' iliyokuwa ikitengenezwa na kampuni ya British American Tobacco.

Filamu hii ikionyeshwa Mnazi Mmoja na Magomeni kila mwezi pamoja na filamu nyingine za cowboys na za Chale Mnene na Chale Mwembamba - Stan Laurel na Oliver Hardy.

Watoto tukizipenda sana filamu hizi.

Hii filamu ya kutangaza sigara ilikuwa na nyimbo yake watoto wote tukiijua tukiimba.

Stori ya senema hii ni mtu kutoka shamba aliyekuwa na kipaji cha kupiga guitar anafika mjini pengine Salisbury (Harare) kisha anaibiwa guitar lake.

Anamkimbiza mwizi wake hadi anamkamata na hizi mbio sehemu moja inakuwa ndani ya soko.

Senema ya kuwafurahisha watoto jinsi meza za sokoni zilizokuwa na bidha zilivyokuwa zikipinduliwa.

Mimi nilikuwa naipenda sehemu ya mwisho ya filmu hii ambako huyu jamaa yuko nyuma ya pick up na guitar lake anapiga na kuimba baada ya kumtia mkononi mwizi wake na kulipata gitaa lake.

Nyimbo ambayo alikuwa akiimba ilikuwa na kiitikio, ''sigareti, sigareti, sigareti.''

Sehemu ya mwisho ya nyimbo hii anapiga guitar haimbi hapo inaingia flute (fiimbi) ya Spokes Mashiane mpiga filimbi maarufu aliyekuwa na kipaji cha juu sana.

Hapa ndipo palipokuwa pakinisuuza mimi.
Muziki aliokuwa akipiga ukiitwa Kwela.

Mimi nilikuwa napiga filimbi udogoni na waliokuwa wakinisikiliza walikuwa wanasema nampatia sana Spokes Mashiane.

Nyimbo hizi zilikuwa maarufu sana Tanganyika na zaidi Kenya na zikipigwa sana Voice of Kenya (VOK).

Kenya wakatokea wapigaji wengi sana wa magita kwa mtindo wa George Sibanda.

Tanganyika muziki uliopendwa ulikuwa ni wa Congo ukirekodiwa na kampuni maarufu ya Loningisa na nyimbo za Congo zikijulikana kwa namba zake kama Loni 1, 2,3 nk.

''Loni,'' ikiwa na maana Loningisa.

Baba yangu siku nilipomweleza kuhusu senama hii akaniambia kuwa hiyo nyimbo inayoimbwa, ''sigareti, sigareti,'' huyo ni George Sibanda.

Hiyo filimbi mpigaji ni Spokes Mashiane.
Spokes Mashiane yeye alikuwa kutoka Johannesburg.

Nilijaaliwa kufika Johannesburg mji ambao historia yake ya miaka ya 1950 ni ya kipekee sana kiasi wote watu wa Afrika Kusini wanasema kubadili jina la mji huo ni kupoteza historia yake yote kwa ukamilifu.

Huu ndiyo ulikuwa mji wa Spokes Mashiane, Miriam Makeba na Nelson Mandela pia.

Lakini vilevile huu ni mji wa Jim Bailey na gazeti lake la Drum.
Jim Bailey ana historia ya kuvutia.

Afrika Kusini imetengeneza filamu ya maisha ya Jim Bailey na gazeti lake.
Filamu hii inaitwa ''Drum.''

Filamu hii inatosha kukufunza maisha yalikuwaje nyakati zile na upekee wa Jim Bailey ukimlinganisha na Wazungu wenzake wabaguzi.

Nitaweka link ya movie hii mpate kuiona na kuisikia miziki ya Afrika Kusini ya miaka ya 1950.

Nilikuja kufahamiana na Jim Bailey miaka ya 1980 ambae nilijulishwa kwake na Ally Sykes.

Hiki ni kisa kingine kinachohitaji muda wa peke yake kukieleza.

Halikadhalika Johannesburg ulikuwa mji wa Dorothy Masuka ingawa asili yake yeye kazaliwa wa Bulawayo.

Kuna wakati ilikuwa vigumu kusema nani kamzidi mwenzake katika uimbaji kati ya Miriam Makeba na Dorothy Masuka.

Dorothy Masuka akapotea Afrika ya Mashariki ingawa aliendelea kuwapo jukwaani.

Kuna jambo la kushangaza lilinitokea mwaka 2000 katika safari yangu ya kwanza kwenda Johannesburg.

Nilipata taarifa ya kifo cha Jim Bailey ndani ya ndege katika mazungumzo ya kawaida na Mzungu mmoja Mwafrika Kusini.

Huyu bwana katika mazungumzo nilimwambia kuwa Johannesburg napita njia safari yangu ni Manzini, Swaziland lakini nikimaliza shughuli zangu nitakwenda Johannesburg kumuona Jim Bailey.

Alishangaa vipi nimemjua Jim Bailey.

Akanipa pole akanieleza kuwa Bailey amefariki mwezi uliopita na walikuwa majirani.

Huyu bwana akanishauri kuwa nisipande ndege kuja Johannesburg nipande mabasi madogo yanaitwa, ''Kubi,'' kutoka Mbabane ili nipite Kwa Zulu Natal niione Afrika Kusini.

Akaniambia kuwa basi hili litanifikisha Durban na nitaweza kukaa hapo siku mbili tatu hivi kuona mji.

Huyu bwana akanieleza kitu kingine akanielekeza hoteli nzuri ya kufikia akanambia kuwa hizo ni ''chain of hotels.'' ziko karibu miji yote mikubwa ya Afrika Kusini na huwa ziko barabara kuu wepesi kufikika na nikipanda ''kubi'' itanishusha mlangoni hotelini.

Nilipita Kwa Zulu Natal na sikujuta kufuata ushauri wa yule rafiki yangu.

Hapa ndipo niliposema hapo juu kuwa nilikutana na mambo ya kushangaza.

Nilipoingia chumbani kwangu hapo hotelini Durban nikawasha TV.

Naona kipindi cha Dorothy Masuka sasa mtu mzima anafanyiwa mahojiano anaeleza maisha yake.

Ndipo nikamsikia akieleza siku zake za ujana yeye na Miriam Makeba wakiwa marafiki wakubwa wanaanza muziki wao.

Ilikuwa miaka mingi sikupata kumsikia Dorothy Masuka.

Kipindi kile kikarejesha kumbukumbu zangu za hawa waimbaji wawili kutoka Afrika Kusini.

Nyimbo zao nyakati zile zilikuwa maarufu sana Tanganyika.
Kifo cha Jim Bailey nimekisikia kweye ndege nakuja Afrika Kusini.

Nafika Durban namuona Dorothy Masuka baada ya kupotea katika fikra zangu kwa miaka mingi sana.

Kusafiri ni elimu tosha.
picha hujatuwekea mzee said
 
Bila kuelewa kwanza hili ni jukwaa gani ni ngumu pia kuelewa malengo ya uzi huu.

Msiwe mnaparamia tu vitu without know how.
Matola,
Nimekuelewa.

Ndugu yetu kakosea katika lugha yake katika swali lake.

Mimi nimemtambua na sikutaka kumpatiliza.

Mimi nasaidiwa na uzee wangu.
Hapo kwako kakikwaa kisiki.
 
Always kila nikiona nyuzi zako najua nna cha kujifunza kutoka kwenye maisha waliyoishi wazee wetu zamani , Hongera kwa Kuandika vizuri Nyuzi zako Mkuu
 
Back
Top Bottom