Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni atembelea Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe ambacho Mbunge wa Jimbo hilo, Dotto Biteko aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe, Jackson Kirahuka akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni sehemu mbalimbali za kituo hicho ambacho Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dotto Biteko (katikati) aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri. Aliyevaa Kaunda suti ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Amani Mwenegoha.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimfafanulia jambo Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (watatu kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo (wapili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.
Baada ya hapo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akazungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita ambao ni majirani wa Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo. Wananchi hao wamelalamika kuwepo na vitendo vya ukatili dhidi yao vinavyofanywa na baadhi wa askari wa kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.
Mkazi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita, Biosi Makongoro akitoa kero yake kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyekaa) dhidi ya Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo ambayo ipo jirani na kijiji hicho, kuwa askari wa kampuni hiyo wanadaiwa kuwanyanyasa wananchi hao wanapopita katika eneo la Kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.
Chanzo: Michuzi