Bukoba: Waziri Kagasheki asoma maoni ya wana JF jukwaani, adai ni uongo!

KAUDO

Senior Member
Aug 10, 2011
138
67
Mkutano wa jana mjini Bukoba waziri Kagasheki pamoja na mambo mengine aliutumia kuishambulia JF kuwa inamwandika uongo.

Alisoma pia baadhi ya maoni ya wachangiaji Kuwa yeye ndiye alimchongea Meya wa Bukoba Dk. Anatory Aman na hata kapata nafasi hiyo, kwamba alikuwa raia wa Uganda ila wakati alipokuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani alimsaidia kupata uraia wa TZ. Haya yote yalimwagwa hadharani mbele ya wananchi uwanja wa Mayunga.

Kagasheki amemwaga mboga tunasubiri atakayemwaga ugali.

attachment.php

Kagasheki akishuka jukwaani baada ya kuhutubia
 
Attachments

  • kagashe.jpg
    kagashe.jpg
    36.7 KB · Views: 2,612
Mchunguze sana anaelia sana msibani, Kaghasheki ni mmoja wao.

Ni kwanini viongozi hawapendi kukosolewa?.
 
Akisifiwa hapa jf mbona hasemi chochote!
Nani amsifie wakati anamwacha katibu wake wa chama anamaliza tembo wetu? Hana la kusifiwa, hii shehena ya pili ya pembe za tembo iliyokamatwa HongKong, ilikuwa inatosha kabisa kumfanya ajiuzuru, lakini ndiyo ile ile kasumba ya watanzania, akipewa madaraka basi kutoka ni hadi iletwe winchi hata kama hapo madarakani hana jipya.
 
Katika biashara hii haramu, nahisi huyu katibu ni agent wa mkuu wa kaya na inaonekana biashara anaimudu vizuri na ndio akapewa nafasi hii kama kulipana fadhilla.

Hivi tujiulize kama sisi watu wa kawaida kabisa tumepata habari ingawa sio rasimi kuwa huyu jamaa huenda anahusika na hii biashara sasa inakuwaje anapewa cheo licha ya kashifa kama hii kumwandama!Ina maana mkuu wa kaya hana habari au taarifa hizi?Au ndio kusema habari hizi ni uzushi mtupu?Ikija ikithibitika kuwa anahusika na biashara hii, huyu mkuu wa kaya tumpe adhabu gani zaidi ya kumtimua madarakani?
 
Kichwa kibovu mbona ana sifiwa kila siku hapa hajawai kusema!

Kusoma maoni na habari si uthibitisho wakuwa Member!

Nimefurahi kujua nayeye ana fuatilia jf! Jf juu!
 
Huyu naye ni miongoni mwa viongozi wanaojua kulialia na kutafuta sifa. Hiyo wizara ni ya kupeana ulaji, sijui akitoka yeye itakuwa zamu ya nani kula.
 
kagasheki bwana... yeye ndo aliemsaidia dr amani? mie nimebahatika kufika mpaka kijijini kwake kabisa dr amani..kipindi nasoma kwenye shule yake amani primary school. walikuwa wakimshtumu kuwa sio raia wa tz tangu zamani huyu mzee watu...mambo ya siasa bwana...
 
Akisifiwa hapa jf mbona hasemi chochote!

Kagasheki nafikiri anajisahau kwa maana anafikiri labda yeye kuwa waziri kunamfanya awe binadamu wa aina ya pekee mwenye sifa zote nzuri. Lakini hata sifa nzuri bado haziwezi kuwa nzuri kwa wote na wakati wote. Anasahau kuwa tunamjua udhaifu wake na kuwa waziri hakuondoi udhaifu huo. Kwanza ni mtu mwenye majivuno na jaziba. Kwa kuwa yeye ni mfuatiliaji namkumbusha zogo lake na pilot wa AURIC pale mwaka 2008 na ajitazame upya kama mtu mwenye hadhi ya uwaziri je alivyofanya ilkuwa sawa? Halafu na upambanaji wake dhidi ya wale wasiofanya vizuri kwenye TANAPA hauko principled na asipofuata sheria na taratibu naweza kullingizia shirika na wizara hasara kubwa na mwisho wa siku atakuja kuhukumiwa kama Mhaya na sio waziri
 
Katika biashara hii haramu, nahisi huyu katibu ni agent wa mkuu wa kaya na inaonekana biashara anaimudu vizuri na ndio akapewa nafasi hii kama kulipana fadhilla.

Hivi tujiulize kama sisi watu wa kawaida kabisa tumepata habari ingawa sio rasimi kuwa huyu jamaa huenda anahusika na hii biashara sasa inakuwaje anapewa cheo licha ya kashifa kama hii kumwandama!Ina maana mkuu wa kaya hana habari au taarifa hizi?Au ndio kusema habari hizi ni uzushi mtupu?Ikija ikithibitika kuwa anahusika na biashara hii, huyu mkuu wa kaya tumpe adhabu gani zaidi ya kumtimua madarakani?

Naomba Kagasheki akatae na hili pia
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom