Bukoba: Waziri Kagasheki asoma maoni ya wana JF jukwaani, adai ni uongo!

Tumshukuru kwa kuwaambia watanzania hata wasiojua kuwa kuna JF inayowatoa roho.Wanaongeza publicity kwa watu huk mikoani ambao pengine kwa internet zaidi ya kusoma email kupitia hotmail.com na kutafuta scolarship hakuna kingine.sasa hwa watu wanawezajua JF kuliko hata kuijua yahoo na gmail na skypes.
 
Kwanini anakwenda kukanusha kwenye mkutano wa hadhara?.ambapo hawezi kuhojiwa wala kujibiwa kuhusu taarifa zilizoandikwa jf.si angejitokeza hapahapa jf ili apambane na vichwa vya jf.kulialia huku akiwa amejificha hakusaidii chochote.
 
kagasheki bwana... yeye ndo aliemsaidia dr amani? mie nimebahatika kufika mpaka kijijini kwake kabisa dr amani..kipindi nasoma kwenye shule yake amani primary school. walikuwa wakimshtumu kuwa sio raia wa tz tangu zamani huyu mzee watu...mambo ya siasa bwana...

Mkuu hivi Dr.Amani anatoka kijiji gani, Kagondo/Katoma, Burifani Kyaka au Minziro? Wakulahumiwa ni madiwani walio mchagua mtu ambaye uraia wake una utata, kama alipewa urai kihalali basi hasipewe Key Post, hawezi kuwa commited na Taifa letu 100% tuna msemo "EMBEHO TEYEBWA OWABO" tangu nisikie hizi ngojera za ujenzi wa soko la munispaa ya Bukoba miaka imepita sana bila ujenzi wowote, malumbano tu yasiyo kwisha - nakwambia hata kama wangefanikiwa kupata wakandarasi/wajenzi jamaa ange enda kutafuta ndugu zake Uganda kuwapa contract, tusije tukijidanganya HAPA!

Wazungu wana msemo "Action speaks VOLUME" kama anaweza kuwa na guts za kumgeuzia kibao KISIBANTE aliye msadia kupata Uraia (kama ni kweli), mtu mwenye traits kama hizo za kuwa kigeu geu unaweza kujuwa kesho atafanya nini? Tunawezaje kumpa mkoba wa kuendeleza mji wa BUKOBA kwa mtu ambaye anapendelea kuendeleza turmoil zaidi kuliko maendeleo ya kweli! - no wonder kuna vurugu tupu na malumbano, hana cha kupoteza.

Niliambiwa kuna diwani mmoja kutoka kijijini kwetu ni staunch supporter wa Meya huyu, nikirudi nyumbani mtafunga mikononi kamba ya mnazi awaeleze wana kijiji udiwani wake umesaidiaje kuendeleza munispaa ya Bukoba.

Kwa nini suala hili la ujenzi wa SOKO wasitafutwe raia/wafanyabiashara wenye uchungu wa kweli kuhusu maendeleo ya munispaa, likawekwa jopo la ku-mobilize watu wakatoa michango na kutafuta wafadhili, mbona wako wengi tu. Ningeshauri jopo hilo lisimamiwe na Mh. BUBA - nendeni mji wa MOSHI mkajifunze jinsi ya ku-run miji, kuna umuhimu mkubwa wa kuondokana na soko lililo jengwa enzi za Wajerumani.
 
Tumshukuru kwa kuwaambia watanzania hata wasiojua kuwa kuna JF inayowatoa roho.Wanaongeza publicity kwa watu huk mikoani ambao pengine kwa internet zaidi ya kusoma email kupitia hotmail.com na kutafuta scolarship hakuna kingine.sasa hwa watu wanawezajua JF kuliko hata kuijua yahoo na gmail na skypes.

Nico bwana, yaani nimecheka karibu nife! well said MKUU.
 
Hamis Kagasheki anahitaji kutambua kwamba zama hizi za IT hana pakujificha kamwe! akifanya jambo jema tutamsifia kwa kila namna ili umma wa watanzania uje kuna mtu anajali na anatenda yaliyo mema kwa niaba yao, bali akivurunda "tutamchanachana na kumuumbua kadri inavyostahili kwa kutumia kila medium at our disposal.

Long live JF for paying lip service to important causes.
 
Anakosea sana kuiponda Jf kwani sisi ndio inatupa kila kitu hapa,aombe radhi tafadhari.
 
Mkuu hivi Dr.Amani anatoka kijiji gani, Kagondo/Katoma, Burifani Kyaka au Minziro? Wakulahumiwa ni madiwani walio mchagua mtu ambaye uraia wake una utata, kama alipewa urai kihalali basi hasipewe Key Post, hawezi kuwa commited na Taifa letu 100% tuna msemo "EMBEHO TEYEBWA OWABO" tangu nisikie hizi ngojera za ujenzi wa soko la munispaa ya Bukoba miaka imepita sana bila ujenzi wowote, malumbano tu yasiyo kwisha - nakwambia hata kama wangefanikiwa kupata wakandarasi/wajenzi jamaa ange enda kutafuta ndugu zake Uganda kuwapa contract, tusije tukijidanganya HAPA!




Wazungu wana msemo "Action speaks VOLUME" kama anaweza kuwa na guts za kumgeuzia kibao KISIBANTE aliye msadia kupata Uraia (kama ni kweli), mtu mwenye traits kama hizo za kuwa kigeu geu unaweza kujuwa kesho atafanya nini? Tunawezaje kumpa mkoba wa kuendeleza mji wa BUKOBA kwa mtu ambaye anapendelea kuendeleza turmoil zaidi kuliko maendeleo ya kweli! - no wonder kuna vurugu tupu na malumbano, hana cha kupoteza.

Niliambiwa kuna diwani mmoja kutoka kijijini kwetu ni staunch supporter wa Meya huyu, nikirudi nyumbani mtafunga mikononi kamba ya mnazi awaeleze wana kijiji udiwani wake umesaidiaje kuendeleza munispaa ya Bukoba.

Kwa nini suala hili la ujenzi wa SOKO wasitafutwe raia/wafanyabiashara wenye uchungu wa kweli kuhusu maendeleo ya munispaa, likawekwa jopo la ku-mobilize watu wakatoa michango na kutafuta wafadhili, mbona wako wengi tu. Ningeshauri jopo hilo lisimamiwe na Mh. BUBA - nendeni mji wa MOSHI mkajifunze jinsi ya ku-run miji, kuna umuhimu mkubwa wa kuondokana na soko lililo jengwa enzi za Wajerumani.
Bukyanagandi na wewe unakurupuka tu na hoja mfu.Tatizo la hapa ni ujinga wa Kagasheki na Wabunge walio wengi kutohudhuria vikao vya maamuzi katika Halmashauri kama baraza la madiwani na kamati za fedha na utawala ambavyo vyote hivyo vina pitisha utekelezaji wa kazi na shughuli za bajeti za Halmashauri.Pia Kagasheki ni mtu wa fitina kwa Mayor.Ninavyojua mimi Mbunge hawezi kuomba kuona mkataba kutoka ofisi ya Mkurugenzi/DED hakanyimwa hapo ni hila tu ndiyo maana Kagasheki hamshambulii Mkurugenzi wa Manispaa kuomba Pinda kumfukuza kazi kama kuna mkataba wa kifisadi maana Mkugugenzi ndiye mshauri mkuu wa Mayor katika mambo yote ya uendeshaji wa Halmashauri kwanini Kagasheki anapambana na Mayor peke yake ?,Kuna jambo hapo na tatizo ni kuona kagasheki anaporomoka viwango vya ushawishi anabaki kutengeneza majungu na wazee wanywa kahawa hapo tu mjini na walangila njaa tu hapo wanaomuona na kuomba msaada.Katika hoja za Kagasheki nitakuwa mtu wa mwisho kumuunga mkono kamwe.Namshauri Kagasheki aongoze bidii kwa haya mambo ya ahadi za ccm mwaka 2010 kwa wananchi wa Kagera
1.Upatikanaji wa meli kubwa kuziba pengo la meli ilizama ya MV.Bukoba ni ahadi ya Kikwete na ccm
2.Ujenzi na ukamilishaji wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Misenye.
 
Last edited by a moderator:
Well said mkuu
Hamis Kagasheki anahitaji kutambua kwamba zama hizi za IT hana pakujificha kamwe! akifanya jambo jema tutamsifia kwa kila namna ili umma wa watanzania uje kuna mtu anajali na anatenda yaliyo mema kwa niaba yao, bali akivurunda "tutamchanachana na kumuumbua kadri inavyostahili kwa kutumia kila medium at our disposal.

Long live JF for paying lip service to important causes.
 
Hivi tujiulize kama sisi watu wa kawaida kabisa tumepata habari ingawa sio rasimi kuwa huyu jamaa huenda anahusika na hii biashara sasa inakuwaje anapewa cheo licha ya kashifa kama hii kumwandama!Ina maana mkuu wa kaya hana habari au taarifa hizi?Au ndio kusema habari hizi ni uzushi mtupu?Ikija ikithibitika kuwa anahusika na biashara hii, huyu mkuu wa kaya tumpe adhabu gani zaidi ya kumtimua madarakani?

BAHADHI YA MICHEMKO YA MKUU WA KAYA
Mkuu wa kaya tangu aingie madaraka anachemka mara kwa mara katika kupata habari kupitia vyanzo vyake huko ikulu,
Mkuu wa kaya kashawai kumteua mkuu wa wilaya aliekuwa na kesi TAKUKURU, Mkuu wa kaya kashawahi kufungua hotel kwa mbwembwe siku ya pili ukuta ukavunjwa na wakala wa barabara nchini,

Mkuu wa kaya kapingwa changa la macho katika kutangaza makao makuu ya wilaya ya Butiama, Badala yawe Butiama kikachezeshwa cheusi chekundu ile kufunua KIABAKARI! hayaaa kaliwa,
Mkuu wa kaya huyu huyu katika kukabidhi gari la wagonjwa alitaka kuchezeshewa cheusi chekundu kufunua hayaaa! kapata kamtolea nje mkuu wa wilaya kumkabidhi gari la wagonjwa........!
 
Ohhhhhhhhh Jf sio waongo nimeshaanzisha thread yenye ushahidi wa VIDEO...........fuatilieni wala msijiumize vichwa
 
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Mjini, Hamis Kagasheki, ametangaza kutogombea ubunge katika uchaguzi mkuu mwakani.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano hivi karibuni mkoani Kigoma, kabla ya kuanza kwa ziara ya kukagua kambi mbalimbali za wakimbizi ambazo zimefungwa na zinazohitajika kufungwa kutokana na nchi walizotoka kwa sasa kuwa na hali ya utulivu, alisema hatogombea tena ubunge kwa sababu ana mambo mengi ya kufanya.

Kagasheki ambaye katika uchaguzi wa mwaka 2005 alipata ushindani mkubwa kutoka kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilfred Lwakatare, alisema hawezi kufanya kazi kwa presha huku kukiwa na kazi nyingine za kufanya ambazo hazina presha.

Alisema anaweza kuwa mtumishi mzuri wa jamii iwapo atafanya kazi bila msukumo kuliko hivi sasa akiwa mbunge ambapo amekuwa akiishi kwa presha.

"Kwa kweli ubunge sigombei tena, hiyo ni kazi ya presha, kila wakati unakuwa roho juu, lakini nimeona kuna kazi nyingine ambayo pia naweza nikafanya ya kuhudumia jamii bila ya kuwa na presha kama hii ambayo kwa sasa naifanya," alisema Kagasheki.

Alisema baada ya kumaliza kipindi chake cha ubunge mwaka 2010, atafanya shughuli nyingine ambazo ni muhimu kwa taifa, na kwamba atajitolea kuhudumia jamii kupitia kazi nyingine na si ubunge.

Akizungumzia kuhusu kuzagaa kwa silaha katika Mkoa wa Kigoma, hasa katika Wilaya ya Kibondo, alisema kuwa watajipanga kuhakikisha kuwa kunadhibitiwa.

Aidha, alikiri kuwapo na ukosefu wa vitendea kazi akitolea mfano wa magari, mafuta pamoja na vituo vya polisi, ambapo alikiri inaweza ikawa sababu kubwa ya kuongezeka kwa matukio ya ujambazi.


Source: Tanzania Daima.

Bila shaka Kagasheki amesoma alama za nyakati.

Si siri Wilfred Lwakatare wa CUF anakubalika zaidi Bukoba mjini kama si nguvu za dola kutumika vibaya Bwana Kagasheki asingekuwa mbunge.​

Last edited by Silencer; 22nd May 2009 at 19:53.​
 
Bwana Kagasheki,samahani mkuu humu JF unatumia ID gani.Pia nakuomba ujibu humu humu usiniitie mkutano wa hadhara bukoba au kwingineko.
 
Bukyanagandi na wewe unakurupuka tu na hoja mfu.Tatizo la hapa ni ujinga wa Kagasheki na Wabunge walio wengi kutohudhuria vikao vya maamuzi katika Halmashauri kama baraza la madiwani na kamati za fedha na utawala ambavyo vyote hivyo vina pitisha utekelezaji wa kazi na shughuli za bajeti za Halmashauri.Pia Kagasheki ni mtu wa fitina kwa Mayor.
Mkuu Kanga, hivi inaingia akilini kwamba Mh.Khamisi anaweza kumfitini Mayor ili iweje - amunyanganye Umeya wake? Amfitinishe mtu aliye msaidia kuomba uraia (kama ni kweli) it just doesn't add up - in my opinion. Mtu huitaji shahada ya sayansi ya roketi kujuwa kinacho endelea HAPA - "kulyangana nke nsenene" badala ya kushirikiana, mkoa unarudi nyuma kimaendeleo na watu tunazidi kuwa masikini wa kutupwa!!!

Kitu kingine hata kama wabunge awahudhurii vikao vya maamuzi labda kwa kutingwa na kazi nyingi, kwa nini hawapatiwi minutes za mkutako ili waji-update kwa kile kilicho endelea ndani ya vikao - kuna haja gani ya kutokuwa transparent kwa kile kinacho endelea ndani ya vikao! Why should everything be shrouded in secrecy specifically inapokuja kwenye mambo ya MIKATABA?
Ninavyojua mimi Mbunge hawezi kuomba kuona mkataba kutoka ofisi ya Mkurugenzi/DED hakanyimwa hapo ni hila tu ndiyo maana Kagasheki hamshambulii Mkurugenzi wa Manispaa kuomba Pinda kumfukuza kazi kama kuna mkataba wa kifisadi maana Mkugugenzi ndiye mshauri mkuu wa Mayor katika mambo yote ya uendeshaji wa Halmashauri kwanini Kagasheki anapambana na Mayor peke yake
Hivi nani mwenye mamlaka/mahamuzi ya mwisho: Mkurugenzi wa Manispaa au Mayor? Nafikili Mh.Khamisi ana uzoefu mkubwa katika nyanja za uongozi na usimamizi wa projects hata za kwake mwenyewe i.e handon experience, sasa kwa nini watu waone ajabu anapotaka ku-zero in kwa Mayor badala ya Mkurugenzi wa Manispaa ili apate kilicho jili kwenye mikataba, oh yes apate taarifa from horse's mouth siyo kwamba anapambana naye au sijuhi kumshabulia, kwani kuna tatizo gani Mayor kuambiwa atoe maelezo kuhusu mikataba?? Kumbuka Mh.Khamis amewahi kufanya kazi Wizara ya mambo ya ndani kama naibu wa waziri, wewe unajuwa alikuwa ana inside information gani za kuaminika kuhusu mikataba yenyewe? Msiangalie mambo kijuu juu tu au kusukumwa na mambo ya partisianship.
Kuna jambo hapo na tatizo ni kuona Kagasheki anaporomoka viwango vya ushawishi anabaki kutengeneza majungu na wazee wanywa kahawa hapo tu mjini na walangila njaa tu hapo wanaomuona na kuomba msaada.Katika hoja za Kagasheki nitakuwa mtu wa mwisho kumuunga mkono kamwe
Hata sijuhi nikujibu nini kuhusu such unhelpful remarks!! Ni lini kampuni za Gallup, Synovate au Mori ziliwahi kuja Bukoba kuchukua opinion polls za wapiga kura wanao muhunga/kumkataa Mh. Khamisi mpaka ukawa na uhakika kwamba viwango vya ushawishi wake vinaporomoka exponentially!!! Hili la kusema wazee wa mjini waganga njaa wanakusanyana kwenda kunywa kahawa na Mh. Khamisi huku wakipika majungu na kuomba msaada kutoka kwake - statement hii imenishangaza/kunisikitisha sana, kwa mila za kiafrica nafikili unapaswa kuwaomba msamaha, unaweza kuwa na tofauti na Khamisi ki itikadi lakini siyo fresh kuwasema wazee vibaya, personally siamini kama kuna wazee wa design hiyo mjini Bukoba; nimekulia humo najuwa ninacho zungumza hapa.
Namshauri Kagasheki aongoze bidii kwa haya mambo ya ahadi za ccm mwaka 2010 kwa wananchi wa Kagera
Kama nia yetu ni kuendeleza mkoa wa Kagera, basi ushauri wako una mshiko - mshikamano wa namna hiyo ndio unahitajika kuendeleza mkoa wa Kagera siyo lazima kila kitu tuombe msaada kutoka Serikalini, na
manispaa ya Bukoba inapaswa kufuata mkondo huo huo, tusilete mambo ya kufitinishana, hila, majungu, no lwango logo!
1.Upatikanaji wa meli kubwa kuziba pengo la meli ilizama ya MV.Bukoba ni ahadi ya Kikwete na ccm
Kama nakumbuka vizuri miaka kama minne/mitano hivi niliwahi kwenda ofisini kwa Mbunge wa Kagera ambaye sitamtaja jina nikampa mapendekezo yangu kuhusu usafiri wa meli na mizigo na contact za wafadhili wanao weza kutoa misaada ya kusaidia katika hilo, sikuishia hapo nilimweleza miradi ambayo ingeweza kuinua mkoa wa Kagera ambayo iliwahi kufanyiwa utafiti tangu ukoloni, nikamweleza Project ambayo Serikali ya Sweden alikuwa imelidhia kutoa fedha kwenye miaka ya nyuma, mradi huo nilielezwa na mzee wangu ambaye alikuwa ashirikishwe na wengine walikuwa na Askofu Kibira, Babu yake Mh.Khamisi na wazee wengine walio kuwa wanajulikana mkoani Kagera, nasikia the late Sokoine aliufutilia mbali kwa maelekezo kutoka Serikali ya awamu ya kwanza!! Kwa ufupi - baada ya kumaliza kumueleza mbuge huyo kanambia nifanye "write up" nimpeleke ofisini kwake alafu angenihita for some clarification/discussion - nilitumia karibu siku nne kwenye k/board nikamwandikia kurasa ishirini nikaeleza karibu kila kitu cha muhimu, nikampelekea ofisini kwake - hakujibu chochote mpaka alipo ukosa ubunge na mimi sikuhangahika kwenda kumkumbusha, sijuhi alisahau au hakuona umuhimu wowote wa usafiri wa majini ziwa Victoria nilibaki nimeshikwa na butwaa!!!! Nimalizie kwa kusema wakati tunasubiri ahadi ya Kikwete kuhusu Meli na sisi tutafute watu wa kutusadia.
Ujenzi na ukamilishaji wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Misenye.
Mkuu mimi sikuona mantiki ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa pale Nyamkazi, fedha walizo tumia kulipua mawe/myamba ya zamzam zingeweza kutumika vizuri kama wangejenga UWANJA wa Omukajunguti - kwanza kule ni tambalale sana na ujenzi wake hauwezi kugharimu fedha nyingi, Mh. Khamisi hilo unapaswa kulivaria njuga, hilo likishindikana waende karibu na Kyetema vile vile pale kuna mchanga mwingi na ni tambalale sana kujenga uwanja mwisho ni karibu na Mgeza na penyewe ni tambalale sana - isipokuwa naona kama mji mnataka upanuke mpaka Mgeza -takwimu zote hizi nilipewa na mzee wangu.
 
Hana lolote huyo alipoingia wizarani alikuwa ataki safari za nje,kumbe ilikuwa zuga sasa hata za kwenye internet yupo.
 
Back
Top Bottom