Bukoba: Wanafunzi, Mwalimu na Mlinzi wa Shule ya Katoro Islamic, Wafikishwa Mahakamani kwa mauaji

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,518
Nyundo za Kagera ni Kunyongwa namkumbuka yule ticha alichapa mwanafunzi akafa.

halafu wapo fasta hawanaga longolongo

=======

94F59B94-472D-494F-9C08-84FD1061A6B4.jpeg


Wanafunzi wanne, mwalimu pamoja na mlinzi wa Shule ya Sekondari Katoro Islamic, wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wakikabiliwa na tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo, Mood Muswadiku.

Wanaokabiliwa na kesi hiyo ya mauaji namba 18/2019 ni wanafunzi Husama Ramadhan (17), Sharifu Huled (19), Abdallah Juma (19) na Hussein Mussa (20), mwalimu Majaliwa Abud (35) na Badru Issa Tibagililwa (27) ambaye ni mlinzi. Kesi hiyo iliyotajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Manispaa ya Bukoba, Frola Kaijage, imeahirishwa hadi Septemba 16, na watuhumiwa hawakutakiwa kujibu kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kuisikiliza.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Chema Maswi, alidai mahakamani hapo kuwa mauaji hayo yalitokea Aprili 14, mwaka huu katika Shule ya Sekondari Katoro Islamic, Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera.

Watuhumiwa wamerudishwa rumande hadi hadi kesi hiyo itakapokuja kutajwa tena kwa siku itakayopangwa na mahakama.
 
Hatari, wanauana Waislam kwa Waislam!! Historia ya Mji wa Katoro wakazi 95% ni waislam wenye imani kali na wana roho mbaya sana. Wanatunyanyasa sana Wagalatia.
Nachelea kusema zaidi ila hiyo shule na vyuo vyake viangaliwe sana. Tusijesikia kuwa watoto wetu wamejiripua maana pale hatuelewi kinachoendelea. Je wakaguzi wa mashule na vyuo wanatembelea pale?
 
Udhalilishaji na ubakaji bado ni tatizo Pemba
January 21, 2018 Zanzibar Daima HABARI

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetakiwa kutoa elimu ya afya ya uzazi kisiwani Pemba ili kuokoa kizazi kutokana na kukua kwa wimbi la kuingiliana kinyume cha maumbile.

Kauli hiyo imetolewa na washiriki wa mafunzo ya Elimu ya afya ya Uzazi na Elimu kwa mtoto wa kike yanayoendelea Micheweni, Kisiwani Pemba.

Wakichangia mada ya afya ya Uzazi, mshiriki kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali anayeratibu masuala ya Jinsia, Hidaya Khamisi amesema kwamba takwimu za udhalilishaji za hivi karibuni zinaonesha Kisiwa cha Pemba hususan wilaya ya Wete inaongoza kwa asilimia 70 kwa vitendo vya ulawiti na ubakaji.
Amesema vitendo hivyo vinasababisha fedheha katika jamii na kukatisha ndoto za mtoto kufikia malengo yake maishani.

Wakionyesha ukubwa wa tatizo washiriki wamesema kuwa kwa hivi sasa si shuleni, kwenye madrasa wala nyumbani ni mahali salama kwa watoto wa kiume na wa kike kwani kwa sababu si ajabu kumwona mtu anayeheshimika katika jamii hususan mzazi wa kiume akifanya mapenzi na watoto wake wa kuwazaa.

Hivi karibuni mkazi mmoja wa shehia ya Kiungoni Kimango, Hamad Omari Hamad mwenye miaka 56 alikamtwa na polisi kutokana na vitendo vya ubakaji alivyowafanyia watoto wake watatu akiwemo mtoto mdogo wa miaka minne na mmoja wao kupewa mimba na baba huyo.

Utafiti uliofanyika wilaya ya Wete mwaka 2016 kuhusiana na masuala ya unyanyasaji wa watoto iligundulika kwamba darasa zima lenye watoto 60 walisema kwamba wanataka wawekewe mazingira ili wasidhalilishwe kwa sababu watoto wote darasa hilo wamefanyiwa vitendo vya udhalilishaji hususan kulawitiwa.

Aidha ripoti nyingine kutoka shule moja wilayani Micheweni kwa mujibu wa Meneja wa kituo cha Redio Jamii Micheweni, Ali Kombo imeonyesha kwamba kati ya wanafunzi 60 ni wanafunzi 10 tu ambao walikuwa bado hawajafanyiwa udhalilishaji wa kingono.

Mafunzo ya Elimu ya Afya ya Uzazi na Elimu kwa mtoto wa kike yanayoendeshwa na UNESCO yana lengo la kuunda vikundi vya vijana shuleni na kina mama watayarishaji vipindi vya redio kwa kushirikiana na Redio Jamii Micheweni, ambavyo vitasambaza elimu rika kwa vijana na kina Mama.

cc: FaizaFoxy
 
kama kawaida ya jamii yetu, tunasubiri madhara yatokee ndio tunakurupuka kutafuta ufumbuzi!
  • Shule ina sare kama za Afghanistan, tunaangalia tunasema ni uhuru wa kuabudu
  • Watoto darasani wanakaa kwa kutenganishwa wasichana kwa wavulana, tunakenua meno eti ni imani yao nk.

Huu ujinga inabidi sisi kama jamii tuwajibike nao, watuhumiwa waachiwe huru maana mtafunga wangapi? Muulize mtu yeyote anayeifahamu Katoro, shida sio shule bali ni tabia ya jamii kufuga ujinga kwa kisingizio cha dini..Wachache mtakaoelewa nazungumzia nini>
 
Na nyie
Kuna dini nyingine zingebaki tu Huko Pwani huku Bara zinaleta Shida, Hivi zaidi ya hiyo dini Mwarabu hakuleta kingine?
Na nyie mijitu ya bara ondokeni pwani.

Mijitu ya hovyo hovyo tu hatuwataki huku rudini kwenu.
 
kama kawaida ya jamii yetu, tunasubiri madhara yatokee ndio tunakurupuka kutafuta ufumbuzi!
  • Shule ina sare kama za Afghanistan, tunaangalia tunasema ni uhuru wa kuhabudu
  • Watoto darasani wanakaa kwa kutenganishwa wasichana kwa wavulana, tunakenua meno eti ni imani yao nk.

Huu ujinga inabidi sisi kama jamii tuwajibike nao, watuhumiwa waachiwe huru maana mtafunga wangapi? Muulize mtu yeyote anayeifahamu Katoro, shida sio shule bali ni tabia ya jamii kufuga ujinga kwa kisingizio cha dini..Wachache mtakaoelewa nazungumzia nini>
Hii ni katoro ya wapi mkuu ya geita au wapi huko
 
Back
Top Bottom