Bukoba: Walimu wa Kolping English Medium wagoma kwa kutolipwa mishahara kwa miezi nane (8)

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Walimu na wafanyakazi wa shule za msingi na sekondari ya kolping inayomilikiwa na kanisa katoriki jimbo la Bukoba wamegoma tangu wiki iliyopita wakishinikiza uongozi kuwalipa malimbikizo ya mishahara ya miezi 8.

Hata hivyo kikao cha kuwaomba wafanyakazi hao kurudi kazini kimevunjika baada ya uongozi kuwasimamisha wenzao 12 wanaodhaniwa vinara wa mgomo huo.

Kolping ni shule maarufu kwa mkoa huo wa Kagera na licha ya kumilikiwa na kanisa lakini kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikifanya vibaya kutokana na kile kinacoelezwa kuwa mapato ya shule yanatumika kulipa wafanyakazi wa hoteli ya kolping na utitiri wa wafanyakazi katika shirika la kolping ambalo kimsingi halina chanzo cha mapato bali kutegemea tu ada za shule husika.

Chanzo: Redio Bukoba.

Mkurugenzi wa shule : 0787 21 29 57

Mhasibu Mkuu 0753 822070

Kwa atakaye taka kuthibtisha.

download2.jpg
download2.jpg
download1.jpg
 
Kuna mdogo wangu alikuwa anasoma hapo sekondari, alifaulu kidato cha 4 kutokana na uwezo wake binafsi lakini akikueleza mambo yanayoendelea hapo yanasikitisha, ada wanazolipa ni kubwa ila huduma zinazotolewa ni tofauti. Kiongozi wa shule ambaye ni padre anajaza ndugu zake hapo kazini, ila kuwalipa ndo shida
 
Huu ndo ujinga wa Private... One's future is not certain.!?

Na usikute hao walimu wala hawakua na mikataba.
 
Poor management. Lazima taasisi ife kwa uzembe wa viongozi.

Mapato ya Biashara inayoingiza hela ukiyatumua kulipa cost za biashara ingine isiyoingiza hela lazima ufeli tu..

Shule hiyo ingefata utaratibu wa mabenki isingefeli . Kwenye ma bank mfano NMB na wengineo kila branch inajitegemea.. usitegemee NMB temeke ilete faida kisha hiyo faida iendeshe NMB ilala isiyoleta faida... ndio maana branch zenye hasara zinafungwa fasta na wafanyakazi wanapigwa redundancy kama hakuna nafasi kwingine kwa kuwapeleka
 
Miezi nani haujalipwa wala huo sio mgomo, ni kuamua kuacha kuwakopesha muda wako...

Waliogoma ni Taasisi kuacha kuwalipa hao wahanga haki zao.
 
Walimu sijui hua wanafeli wapi, miezi nane hujalipwa bado upo tu? Unaishije?
 
Kwani Zile za kwenye Akaunti Ya Askofu Method. Kilaini, alizohongwa na Mafisadi wa EPA? Si wamuombe..zisaidie na yuko huko huko ?
 
Mapato ya Biashara inayoingiza hela ukiyatumua kulipa cost za biashara ingine isiyoingiza hela lazima ufeli tu..

Shule hiyo ingefata utaratibu wa mabenki isingefeli . Kwenye ma bank mfano NMB na wengineo kila branch inajitegemea.. usitegemee NMB temeke ilete faida kisha hiyo faida iendeshe NMB ilala isiyoleta faida... ndio maana branch zenye hasara zinafungwa fasta na wafanyakazi wanapigwa redundancy kama hakuna nafasi kwingine kwa kuwapeleka
Kwenye costing ama cost accounting kila eneo linapewa hasara yake na faida yake na lile eneo ambalo linafanya hasara kumbwa hua linafungwa.

Kwa maelezo ya wadau hapo juu ni kua cost centre ya hospitali haifanyi vizuri hivyo kanisa kutumia faida ya cost centre nyingine ya shule kufidia operational costs za hospitali, lazima ile centre inayotengemeza faida itatetereka iwapo centre ya hasara itakua ni hasara juu ya hasara kila mwaka.
 
Sisi taasisi yetu ni kichekesho cha karne. Ulishawahi kusainishwa mkataba uchwara usiojua nn kimeandikwa ndani? Ogopeni ukosefu wa ajira nyie. Taasisi yangu, 🙌
 
Duu!Hizi management Ni poor kabisa,Ila wangefanya kuongeza vyanzo vya mapato ili kila sekta ijitegemee ili uwepo usawa katika watumishi wake.
 
Makanisa yalianza kuingiwa na dosari baada ya kujiingiza kwenye biashara kisha watumishi wake kuingiwa na tamaa ya fedha na kuacha kazi zake za msingi za kupeleka injili kwa walioikosa
 
Makanisa yalianza kuingiwa na dosari baada ya kujiingiza kwenye biashara kisha watumishi wake kuingiwa na tamaa ya fedha na kuacha kazi zake za msingi za kupeleka injili kwa walioikosa
kweli kabisa
 
..."private sector ndiyo injini ya nchi yetu...." Mh. Samia S. Hassan , Rais wa JMT.
 
Back
Top Bottom