Bukoba: Mungu ashindwa kutokea Mahakamani kutoa ushahidi kwenye kesi inayomkabili Mchungaji Merchades Mugishagwe

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
752
3,096
Ushahidi wa kesi ya jinai inayomkabili mchungaji Merchades Mugishagwe na mkewe Agripina Maganja, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Bukoba umefungwa leo, baada ya shahidi namba tatu kwa upande wa washtakiwa aliyetajwa kuwa ni Mungu kutofika mahakamani hapo.

Mchungaji Merchades Mugishagwe ni baba aliyegoma kuwaandikisha shule watoto wake kwa madai kuwa imani yake haiamini katika elimu ya dunia.

Februari 2021 alikamatwa na polisi kwa amri ya mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawilo akidaiwa kukaidi agizo la kuwaandikisha watoto wake watatu shule.

Pia soma

Mungu.jpg
 
Ushahidi wa kesi ya jinai inayomkabili mchungaji Merchades Mugishagwe na mkewe Agripina Maganja, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Bukoba umefungwa leo, baada ya shahidi namba tatu kwa upande wa washtakiwa aliyetajwa kuwa ni Mungu kutofika mahakamani hapo.
Usilitaje bure Jina la Bwana Mungu wako.
Usilitumie jina la Mungu kwa njia isiyofaa.—Kutoka 20:7.
 
Ni haki kuamini unachokiamini, ila imani yako ikimkosesha mtu (minor) haki yake sidhani hata unayemuamini anakwambia ufanye hivyo (mtoto ana kila haki ya kwenda shule)

After all ya Kaisari muachie Kaisari
 
Back
Top Bottom