Bukoba: Mke afia gesti akiwa na mchepuko

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
1.png

Mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa) anayedaiwa ni mke wa mtu, amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Bukoba, akiwa na mwanaume mwingine anayesemekana ni hawara yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa, watu hao walienda katika nyumba hiyo ya kulala wageni iliyopo eneo la Hamugembe Januari 3, mwaka huu na kuchukua chumba namba nane.

Alisema siku iliyofuata saa 6:00 mchana, polisi walipokea taarifa kutoka kwa wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni kuwa katika chumba hicho kuna watu waliingia jana yake lakini hadi muda huo mlango wa chumba ulikuwa haujafunguliwa na kuna ukimya uliowatia hofu.

Alisema wahudumu hao waliambatana na polisi na walipofika eneo la nyumba hiyo walimkuta mmiliki wake ambaye alitoa funguo za akiba na kufungua chumba hicho.
“Polisi walipofungua chumba walikuta godoro liko chini lakini kitandani lilipopaswa kuwa kulikuwa na mwili wa mwanamke ukiwa umefunikwa shuka na kuuchukua kwenda kuuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera,” alisema.

Kamanda huyo wa polisi mkoa wa Kagera, alisema mtu aliyekuwa pamoja na mwanamke huyo (jina linahifadhiwa) ambaye ni dereva wa basi la abiria linalofanya safari zake kati ya Bukoba na Mwanza, hakukutwa katika chumba hicho na alifunga mlango kwa nje na kuondoka na funguo.

Hata hiyo, alisema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana lakini kutokana na taarifa walizopata kutoka kwa msaidizi wa dereva huyo wamefanikiwa kumpata mtu aliyejitambulisha kuwa ni mume wa marehemu.

Kamanda Ollomi aliongeza kusema kuwa, mume wa marehemu mkazi wa Butimba, jijini Mwanza, amepatikana na kukabidhiwa mwili wa mkewe, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea na kwamba wafanyakazi wawili wa nyumba hiyo ya kulala wageni wanashikiliwa na polisi kwa upelelezi zaidi lakini pia kwa kitendo cha kuficha taarifa za wageni wanaolala katika nyumba hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Jamanieeeeeeeeehh.., chonde chooonde michepuko siyo dili...., bakini njia kuu jamani, Hebu ona sasa
 
Duh!

Nampa pole huyo mama. Umemkuta mwisho mbaya mno. Amekufa na ushahidi wa kumweka mafikio mabaya.

Tumuombe Mungu atujaalie mwisho mwema.
Mpe pole mume kwa kukabidhiwa maiti ya mkewe aliyefia katika shughuli za mchepuko. Si ajabu yeye mume akiwa katika mihangaiko ya kutafuta mahitaji ya familia. Aliyekufa hana pole kwani hana hisia na hajui linaloendelea duniani. Kwakweli huyo mume atakuwa katika fedheha kubwa kupolea msiba wa kifo cha aibu namna hiyo
 
ona sasa mwisho wake ulivyokuwa MUNGU amlaze mahali anapostahili
 
Hili jambo ni la kusikia kwa jirani tu usiombe likakutokea.Huwa kila nikiria kuna waqt naona bora nichagame peke yangu kuliko kutafuta mchepuko kisha yanatokea hayo.
Hapo hata kama kafa kwa ugonjwa wake ila lazima uisaidie polisi bila malipo.
 
Hakuna ushahidi km waliingia hapo kuzini. Ndio maana godoro likawa chini (huenda walilala sehemu tofauti).
Sio wote wanaoingia gesti wa jinsia tofauti wanaingia kuzini.
Sawa Binti Magufuli, wewe ulilala kwenye chaga, mwenzio alilala chini kwenye godoro, alikuwa akikupa msaada tu baada ya kukosa sehem ya kulala. Mzinzi akitetea maiti ya mzinzi mwenzake.
 
Njia kuu inafoleni michepuko ndo dili, pengine walikutana kwa mazungumzo ya bizines Na sio kudungana
 
Back
Top Bottom