Bukoba: Mahakama ya Rufaa ya Tanzania yabatilisha hukumu ya kunyongwa hadi kufa Mwalimu aliyemuua mwanafunzi kwa kipigo

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
885
1,000
Tarehe 17 Disemba 2020, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania katika kikao chake ilichoketi Bukoba, imebatilisha hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania katika kesi ya Mauaji Namba 56 ya 2018 kuwa Mwalimu RESPICIUS PATRICK @ MTANZANGIRA anyongwe mpaka kufa kwa kusababisha kifo cha mwanafunzi SPERIUS EDWARD, aliyedaiwa kufariki dunia kwa kipigo cha viboko.

Mahakama hiyo imebatilisha hukumu hiyo kupitia uamuzi ilioutoa katika Rufaa ya Jinai Namba 70 ya 2019 kwa kuona kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, Kifungu namba 265 na kifungu namba 298(1) vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 ya Sheria za Tanzania havikufuatwa ipasavyo na hivyo kufanya mchakato mzima wa usikilizwaji wa kesi kuwa batili.

Vifungu hivyo vinaitaka mahakama Kuu inaposikiliza mashauri ya jinai kuwa na washauri wa mahakama wasiopungua wawili watakaotoa msaada wa kufikia maamuzi katika kesi hiyo kupitia maoni yao (washauri) kwa jaji anayesikiliza kesi. Mahakama ya Rufaa imekubali kuwa wakati wa kusikiliza kesi hiyo, mahakama Kuu chini ya Jaji Mlacha ilikuwa na washauri watatu wa mahakama lakini washauri hawa ambao sio wataalamu wa sheria (lay persons) hawakuelezwa ipasavyo maana ya kesi hiyo na hivyo wakatoa ushauri pasipo kuwa na uelewa wa walichokishauri. Jaji Mwandambo alieleza kuwa, ukiukwaji wa masharti ya vifungu hivyo (hasa cha 295(1)) uliwanyima washauri hao wa mahakama nafasi ya kusikilizwa na kutoa ushauri na hivyo kuifanya kesi hiyo kuwa kama iliyosikilizwa pasipo usaidizi wa washauri wa mahakama jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania baada ya kubaini mapungufu hayo, ikitumia mamlaka iliyopewa kisheria chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Mamlaka ya Kirufani (AJA) Sura ya 141 Rejeo la 2019 ya kufanya marejeo (Review) kwa kesi mbalimbali, imeibatilisha hukumu hiyo na kuamuru usikilizwaji upya wa kesi hiyo mbele ya Jaji mwingine pamoja na washauri wengine wa mahakama. Hata hivyo, Mahakama hiyo imesema kuwa usikilizwaji huo upya wa kesi hiyo, hautamhusiha mwalimu HERIETH GERALD ambaye aliachiwa huru na Mahakama Kuu ya Tanzania kupitia hukumu ya hesi hiyo ya Mauaji Namba 56 ya 2018. Mwalimu Respicius ataendelewa kushikiliwa wakati akisubiri usikilizwaji upya wa kesi yake. Rufaa hii ilikuwa ikiendeshwa na wakili Remidiues Mbekomize akishirikiana na wakili Aneth Lwiza walimuwakilisha Mrufani na upande wa Serikali uliwakilishwa na mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Ngole.

Rejea hapa Respicius Patrick @ Mtanzangira vs Republic (Criminal Appeal No.70 of 2019) [2020] TZCA 1908; (17 December 2020) | Tanzania Legal Information Institute kwa nakala ya uamuzi wa Mahakama ya Rufaa katika Rufaa ya Jinai namba 70 ya 2019

Pia soma hapa Bukoba: Mahakama Kuu yamhukumu kunyongwa hadi kufa Mwalimu aliyemuua mwanafunzi kwa kipigo kwa tafsiri nzuri isiyo rasmi ya Hukumu kwa lugha ya Kiswahili
 
keisangora

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
1,598
2,000
Kama kesi inasikilizwa upya kwanini huyo aliachiwa nae aisisikilizwe upya? Daah haya mambo ya sheria bana Kwa hiyo hukumu batili daah
Yaani sheria huwa ni ushenzi mtupu yaani hakuna kanuni maalumu MTU anahukumu kulingana na matakwa yake.
Hakimu anakula pote pote.
Kiushauri kiushauri kiushari narudia kiushauri inashauliwa usije ukajihusissha na masuala ya polisi ama mahakama jitahidi sana mmalizane na MTU hata kama kujishusha jishushe
 
darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
5,252
2,000
Ajali kazini,
Walimu wawe makini na adhabu wanazotoa. Mambo mengi sasa hivi yamebadilika na Dunia imekuwa ya kiuanaharakati. Watoto wengi wana maradhi yaliyofichika.
Naamini Sheria zitampa hukumu anayostahili Mwalimu.
 
captain dunga

Senior Member
Jun 5, 2014
168
250
Mi nilijua huyu ng'ombe ameshanyongwa tayari....

Hivi hata yeye atakuwa na amani kweli hata akiachiwa.???

Anyongwe, Anyongwe, Anyongwe....
 
Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,277
2,000
Tarehe 17 Disemba 2020, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania katika kikao chake ilichoketi Bukoba, imebatilisha hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania katika kesi ya Mauaji Namba 56 ya 2018 kuwa Mwalimu RESPICIUS PATRICK @ MTANZANGIRA anyongwe mpaka kufa kwa kusababisha kifo cha mwanafunzi SPERIUS EDWARD, aliyedaiwa kufariki dunia kwa kipigo cha viboko.

Mahakama hiyo imebatilisha hukumu hiyo kupitia uamuzi ilioutoa katika Rufaa ya Jinai Namba 70 ya 2019 kwa kuona kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, Kifungu namba 265 na kifungu namba 298(1) vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 ya Sheria za Tanzania havikufuatwa ipasavyo na hivyo kufanya mchakato mzima wa usikilizwaji wa kesi kuwa batili.

Vifungu hivyo vinaitaka mahakama Kuu inaposikiliza mashauri ya jinai kuwa na washauri wa mahakama wasiopungua wawili watakaotoa msaada wa kufikia maamuzi katika kesi hiyo kupitia maoni yao (washauri) kwa jaji anayesikiliza kesi. Mahakama ya Rufaa imekubali kuwa wakati wa kusikiliza kesi hiyo, mahakama Kuu chini ya Jaji Mlacha ilikuwa na washauri watatu wa mahakama lakini washauri hawa ambao sio wataalamu wa sheria (lay persons) hawakuelezwa ipasavyo maana ya kesi hiyo na hivyo wakatoa ushauri pasipo kuwa na uelewa wa walichokishauri. Jaji Mwandambo alieleza kuwa, ukiukwaji wa masharti ya vifungu hivyo (hasa cha 295(1)) uliwanyima washauri hao wa mahakama nafasi ya kusikilizwa na kutoa ushauri na hivyo kuifanya kesi hiyo kuwa kama iliyosikilizwa pasipo usaidizi wa washauri wa mahakama jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania baada ya kubaini mapungufu hayo, ikitumia mamlaka iliyopewa kisheria chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Mamlaka ya Kirufani (AJA) Sura ya 141 Rejeo la 2019 ya kufanya marejeo (Review) kwa kesi mbalimbali, imeibatilisha hukumu hiyo na kuamuru usikilizwaji upya wa kesi hiyo mbele ya Jaji mwingine pamoja na washauri wengine wa mahakama. Hata hivyo, Mahakama hiyo imesema kuwa usikilizwaji huo upya wa kesi hiyo, hautamhusiha mwalimu HERIETH GERALD ambaye aliachiwa huru na Mahakama Kuu ya Tanzania kupitia hukumu ya hesi hiyo ya Mauaji Namba 56 ya 2018. Mwalimu Respicius ataendelewa kushikiliwa wakati akisubiri usikilizwaji upya wa kesi yake. Rufaa hii ilikuwa ikiendeshwa na wakili Remidiues Mbekomize akishirikiana na wakili Aneth Lwiza walimuwakilisha Mrufani na upande wa Serikali uliwakilishwa na mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Ngole.

Rejea hapa Respicius Patrick @ Mtanzangira vs Republic (Criminal Appeal No.70 of 2019) [2020] TZCA 1908; (17 December 2020) | Tanzania Legal Information Institute kwa nakala ya uamuzi wa Mahakama ya Rufaa katika Rufaa ya Jinai namba 70 ya 2019

Pia soma hapa Bukoba: Mahakama Kuu yamhukumu kunyongwa hadi kufa Mwalimu aliyemuua mwanafunzi kwa kipigo kwa tafsiri nzuri isiyo rasmi ya Hukumu kwa lugha ya Kiswahili
Kuna baadhi ya kazi zina kinga (bima) ya kumsaidia mhusika endapo atafanya jambo lolote la kuleta madhara. Mfano washauri wana bima inayoitwa "Indemnity" ambayo hufidia hasara aliyosababisha. Kwa walimu nao kuchapa ni sehemu ya kazi yao; kwa tukio lililotokea ingefaa wawe na bima ya kutoa fidia badala ya mwalimu kuadhibiwa. Mbona dereva akigonga mtu na kusababisha kifo hahukumiwi kunyongwa?

Hii kada ya ualimu na afya ziangaliwe namna ya kuhakikisha wahusika wanapoleta madhara wakati wa kutekeleza majukumu yao waliadhibiwa kama jambazi aliyevamiwa nyumba kwa mtu na kuua.
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,543

Tz yetu hii. Ninaelewa jurors au hao washauri, ni raia wa kawaida (kama ambavyo hapa JF tunatoa mawazo kulingana na uelewa wetu wa kawaida), na watatoa maamuzi ya ama mshitakiwa ana kosa au la, kulingana na ushahidi, au yote yaliyowasilishwa hapo mahakamani, ila mambo ya adhabu ni ya hakimu au jaji. Na hiyo inatoa nafasi kwa mtu yeyote awe sehemu ya kuhakikisha haki imetolewa kwa mshitakiwa, sio wawe wote ni wasomi wa sheria ambao kwa uelewa wao wanaweza kuelemea zaidi kwenye mambo ya sheria. Naona jsji msomi hapa anasema hivyo si sahihi. Tz ina safari ndefu sana kwenyecmasuala ya haki, ambayo sijui kama itafika.
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,543
2,000
Mi naona hata huyu mwl. Nae alifikia pabaya2, hivi viboko vinaweza kuua mtu kweli?
Duh.
Inategemea unapiga sehemu gani na kwa nguvu kiasi gani. Pia iangaliwe, alitumia fimbo au gongo. Muda unavyokwenda ndio kumbukumbu zinapotea.
 
yamo

Member
Nov 5, 2018
6
45
Sijasikia kama waliotoa hukumu kimakosa wanachukuliwa hatua,

Au mi ndo sijaelewa vizuri!.
 
Rainbow Veins

JF-Expert Member
May 24, 2017
9,580
2,000
Kuna baadhi ya kazi zina kinga (bima) ya kumsaidia mhusika endapo atafanya jambo lolote la kuleta madhara. Mfano washauri wana bima inayoitwa "Indemnity" ambayo hufidia hasara aliyosababisha. Kwa walimu nao kuchapa ni sehemu ya kazi yao; kwa tukio lililotokea ingefaa wawe na bima ya kutoa fidia badala ya mwalimu kuadhibiwa. Mbona dereva akigonga mtu na kusababisha kifo hahukumiwi kunyongwa?

Hii kada ya ualimu na afya ziangaliwe namna ya kuhakikisha wahusika wanapoleta madhara wakati wa kutekeleza majukumu yao waliadhibiwa kama jambazi aliyevamiwa nyumba kwa mtu na kuua.
Ngoja auliwe mwanao ndio utaandika hayo vizuri.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom