Bukoba: Kiongozi UVCCM wilayani Muleba akutwa amefariki kando ya barabara

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Bukoba. Mwili wa Jaspar Jasson, aliyekuwa katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kata ya Katoke Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera umekutwa pembeni mwa barabara ukiwa na alama shingoni.

Akizungumza leo Jumanne Februari 18, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema alama hizo ni kama za mtu aliyejinyonga.

Amebainisha kuwa mwili huo umekutwa katika kijiji cha Bisore wilayani Muleba jana Februari 17, 2020.

“Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho ambacho dalili za awali zinaonyesha mauaji yalifanyika eneo tofauti na mwili huo kutelekezwa pembeni mwa barabara,” amesema Kamanda Malimi.

Amesema uchunguzi wa awali wa kitabibu umebaini kuwa kifo hicho kimetokana na kukosa hewa.

Ameongeza uchunguzi wa daktari umebaini dalili zote za kujinyonga kwa kuwa alikuwa na michubuko shingoni, “pia alikutwa amejisaidia na kujikojolea.”

Amewaomba wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia upelelezi wa kifo hicho kujitokeza.

Chanzo: Mwananchi
 
Kama nawa ccm fasta uchunguzi utakamilika na wagusika watakamatwa ila angelikuwa upande mwingine ule uchunguzi ungeelea hadi mwaka huu uishe
 
Sasa kama alijinyonga, alifikaje hapo pembezoni mwa barabara? Au ndipo alipokatikia? Kama ndio, hiyo kamba aliitoaje na kuiweka wapi?
 
Kuna haja gani ya polisi kusema amekutwa 'amejisaidia na kujikojolea', nchi hii tunaajiri mbumbumbu kwenye kazi muhimu mno, alafu eti 'amejinyonga'!
 
Haya mambo ya kuhusisha vyama kwenye kila suala ni upumbavu. Sasa katibu wa chama kata alikuwa anajulikana kwa kiwango gani au alikuwa na effect zipi zilizofanya apate stress kichama hadi afe?

Sent using Smartika kitochi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom