mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Jeshi la Polisi limezingira ukumbi wa kikao cha semina ya kuwajengea Uwezo BAWACHA, na kumkamata Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa ambaye ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee
Halima Mdee, licha ya jana kuzuiwa kufanya mkutano akiwa mkoani Simiyu, leo Julai 14, 2019 ameendelea na ziara yake Bukoba na kuweza kukutana na Baraza la Wanawake wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera.
UPDATE
Polisi mkoani Kagera nchini Tanzania linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa chama kikuu cha upinzani nchini humo (Bawacha), Halima Mdee.
Polisi walimkamata Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe (Chadema) jana jioni Jumapili Julai 14m, 2019 mara baada ya kumaliza kikoa cha ndani cha wanawake kilichofanyika Bukoka mjini mkoani humo huku wengine wakiachiwa kwa dhamana.
CHADEMA wanadai Jeshi la Polisi Kagera wanadai wanasubiri maelekezo ya RPC, ambaye yuko kwenye msafara wa Rais Magufuli, kuamua hatma ya Halima Mdee wanayemshikilia tangu jana. RPC hajapokea simu za wasaidizi wake wanaosubiri amri hiyo kutoka juu
Mwenyekiti wa Bawacha mkoani Kagera ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Conchesta Rwamulaza akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Julai 15, 2019 amesema Mdee amekamatwa kwa sababu ambazo hazijatajwa.
Amesema kikao chao kilikuwa cha ndani na yeye alikuwa miongoni mwa waliohojiwa jana Jumapili kituo cha polisi Bukoba na kuachiwa.
Amesema kikao hicho kilihusu uchaguzi wa Bawacha Manispaa ya Bukoba na Mdee alikuwa ni miongoni mwa viongozi walioalikwa ambapo aliambatana na Katibu wa Baraza hilo, Grace Tendega.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha jana wamekusanyika kwa makundi nje ya kituo cha Polisi Bukoba wakifuatilia hatima ya dhamana ya Mbunge huyo.
Jitihada za Mwananchi kumpata kamanda wa Polisi mkoani humo hazijazaa matunda kwani ofisini kwake hayupo wala simu zake za mkononi hazipokelewi.
UPDATE
Jeshi la Polisi limemuachia Mbunge huyo wa Kawe aliyeshikiliwa tangu jana baada ya kudhaminiwa na Watu wawili
Ametakiwa kuripoti Kituoni hapo baada ya mwezi mmoja au muda wowote atakapohitajika