Bukoba: Halima Mdee akamatwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kuongea lugha ya uchochezi. Aachiwa kwa dhamana

Acha wamkamate alisema mkuu wa mkoa wa simiyu ni mwanamke sasa wache wamzalishe mgumba huyu

Namheshimu sana Mbunge Halima Mdee ila kama ni kweli alisema haya maneno uliyosema hapa dhidi ya Mkuu wa Mkoa nadhani atakuwa anastahili Kipindi Kigumu anachokipitia sasa. Hata kama tuna Chuki zetu za Kisiasa ila busara na hekima baina yetu na hasa katika Maneno ya Kutumia inahitajika mno. Huwezi Kudhalilisha Wanaume au Kumdhalilisha Mwanaume kwa Kiwango hicho halafu ukaachiwa tu uendelee Kutamba.
 
Hong Kong raia wameandamana kupinga amendment ya "Extradition Bill" kwa kudai mtuhumiwa atakosa fair trial. Tanzania imepitishwa Cyber Act 2015, Sheria ya vyombo vya habari, Written Law (Miscellaneous amendment No. 3), Sheria ya Takwimu na Mafao nk Wananchi kimya, ELIMU ×3.
 
Jeshi la Polisi limezingira ukumbi wa kikao cha semina ya kuwajengea Uwezo BAWACHA, na kumkamata Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa ambaye ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee

Halima Mdee, licha ya jana kuzuiwa kufanya mkutano akiwa mkoani Simiyu, leo Julai 14, 2019 ameendelea na ziara yake Bukoba na kuweza kukutana na Baraza la Wanawake wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera.

UPDATE
Polisi mkoani Kagera nchini Tanzania linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa chama kikuu cha upinzani nchini humo (Bawacha), Halima Mdee.

Polisi walimkamata Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe (Chadema) jana jioni Jumapili Julai 14m, 2019 mara baada ya kumaliza kikoa cha ndani cha wanawake kilichofanyika Bukoka mjini mkoani humo huku wengine wakiachiwa kwa dhamana.

CHADEMA wanadai Jeshi la Polisi Kagera wanadai wanasubiri maelekezo ya RPC, ambaye yuko kwenye msafara wa Rais Magufuli, kuamua hatma ya Halima Mdee wanayemshikilia tangu jana. RPC hajapokea simu za wasaidizi wake wanaosubiri amri hiyo kutoka juu

Mwenyekiti wa Bawacha mkoani Kagera ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Conchesta Rwamulaza akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Julai 15, 2019 amesema Mdee amekamatwa kwa sababu ambazo hazijatajwa.

Amesema kikao chao kilikuwa cha ndani na yeye alikuwa miongoni mwa waliohojiwa jana Jumapili kituo cha polisi Bukoba na kuachiwa.

Amesema kikao hicho kilihusu uchaguzi wa Bawacha Manispaa ya Bukoba na Mdee alikuwa ni miongoni mwa viongozi walioalikwa ambapo aliambatana na Katibu wa Baraza hilo, Grace Tendega.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha jana wamekusanyika kwa makundi nje ya kituo cha Polisi Bukoba wakifuatilia hatima ya dhamana ya Mbunge huyo.

Jitihada za Mwananchi kumpata kamanda wa Polisi mkoani humo hazijazaa matunda kwani ofisini kwake hayupo wala simu zake za mkononi hazipokelewi.
Yawezekana RPC naye anasubiri maekelezo kutoka juu! Je walienda kumkamata kwa maelekezo kutoka juu pia?
 
Rais wetu ni clever sana
Baadae hawa hawa anawachagua kwenye post nyeti za serikali wakiunga tu juhudi
Hawa wanastaili sana kuliko walee
Hongeraze
 
Namheshimu sana Mbunge Halima Mdee ila kama ni kweli alisema haya maneno uliyosema hapa dhidi ya Mkuu wa Mkoa nadhani atakuwa anastahili Kipindi Kigumu anachokipitia sasa. Hata kama tuna Chuki zetu za Kisiasa ila busara na hekima baina yetu na hasa katika Maneno ya Kutumia inahitajika mno. Huwezi Kudhalilisha Wanaume au Kumdhalilisha Mwanaume kwa Kiwango hicho halafu ukaachiwa tu uendelee Kutamba.
Umefikiria kuwa wanaosema au kuandika kuwa alisema hayo, ndiyo hakika wanasrma na kutoa sifa hizo dhidi ya huyo mkuu. Busara inatakiwa kuongoza.
 
Inasikitisha sana...

Kuna watu wanaongea matusi, kudhalilisha viongozi hadharani lakini hawachukuliwi hatua zozote zile...

Cc: mahondaw
 
Sasa wewe bwege kichwa cha habari kinasema kakamatwa halafu maelezo ukumbi umezingirwa. Nyumbu kwa kweli ni shida hasa
Hakuna cha kuzingirwa wala kukamatwa, wenyewe wanasema waliambiwa akimaliza kula akaripoti kituoni
 
Jeshi la Polisi limezingira ukumbi wa kikao cha semina ya kuwajengea Uwezo BAWACHA, na kumkamata Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa ambaye ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee

Halima Mdee, licha ya jana kuzuiwa kufanya mkutano akiwa mkoani Simiyu, leo Julai 14, 2019 ameendelea na ziara yake Bukoba na kuweza kukutana na Baraza la Wanawake wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera.

UPDATE
Polisi mkoani Kagera nchini Tanzania linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa chama kikuu cha upinzani nchini humo (Bawacha), Halima Mdee.

Polisi walimkamata Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe (Chadema) jana jioni Jumapili Julai 14m, 2019 mara baada ya kumaliza kikoa cha ndani cha wanawake kilichofanyika Bukoka mjini mkoani humo huku wengine wakiachiwa kwa dhamana.

CHADEMA wanadai Jeshi la Polisi Kagera wanadai wanasubiri maelekezo ya RPC, ambaye yuko kwenye msafara wa Rais Magufuli, kuamua hatma ya Halima Mdee wanayemshikilia tangu jana. RPC hajapokea simu za wasaidizi wake wanaosubiri amri hiyo kutoka juu

Mwenyekiti wa Bawacha mkoani Kagera ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Conchesta Rwamulaza akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Julai 15, 2019 amesema Mdee amekamatwa kwa sababu ambazo hazijatajwa.

Amesema kikao chao kilikuwa cha ndani na yeye alikuwa miongoni mwa waliohojiwa jana Jumapili kituo cha polisi Bukoba na kuachiwa.

Amesema kikao hicho kilihusu uchaguzi wa Bawacha Manispaa ya Bukoba na Mdee alikuwa ni miongoni mwa viongozi walioalikwa ambapo aliambatana na Katibu wa Baraza hilo, Grace Tendega.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha jana wamekusanyika kwa makundi nje ya kituo cha Polisi Bukoba wakifuatilia hatima ya dhamana ya Mbunge huyo.

Jitihada za Mwananchi kumpata kamanda wa Polisi mkoani humo hazijazaa matunda kwani ofisini kwake hayupo wala simu zake za mkononi hazipokelewi.

UPDATE
Jeshi la Polisi limemuachia Mbunge huyo wa Kawe aliyeshikiliwa tangu jana baada ya kudhaminiwa na Watu wawili‬

Ametakiwa kuripoti Kituoni hapo baada ya mwezi mmoja au muda wowote atakapohitajika‬
Intelijensia uchwara ni janga kwa taifa. Iweje inuse upinzani tu?
 
Back
Top Bottom