Bukoba: Halima Mdee akamatwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kuongea lugha ya uchochezi. Aachiwa kwa dhamana

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Messages
689
Points
1,000

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2011
689 1,000
Jeshi la Polisi limezingira ukumbi wa kikao cha semina ya kuwajengea Uwezo BAWACHA, na kumkamata Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa ambaye ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee

Halima Mdee, licha ya jana kuzuiwa kufanya mkutano akiwa mkoani Simiyu, leo Julai 14, 2019 ameendelea na ziara yake Bukoba na kuweza kukutana na Baraza la Wanawake wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera.

UPDATE
Polisi mkoani Kagera nchini Tanzania linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa chama kikuu cha upinzani nchini humo (Bawacha), Halima Mdee.

Polisi walimkamata Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe (Chadema) jana jioni Jumapili Julai 14m, 2019 mara baada ya kumaliza kikoa cha ndani cha wanawake kilichofanyika Bukoka mjini mkoani humo huku wengine wakiachiwa kwa dhamana.

CHADEMA wanadai Jeshi la Polisi Kagera wanadai wanasubiri maelekezo ya RPC, ambaye yuko kwenye msafara wa Rais Magufuli, kuamua hatma ya Halima Mdee wanayemshikilia tangu jana. RPC hajapokea simu za wasaidizi wake wanaosubiri amri hiyo kutoka juu

Mwenyekiti wa Bawacha mkoani Kagera ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Conchesta Rwamulaza akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Julai 15, 2019 amesema Mdee amekamatwa kwa sababu ambazo hazijatajwa.

Amesema kikao chao kilikuwa cha ndani na yeye alikuwa miongoni mwa waliohojiwa jana Jumapili kituo cha polisi Bukoba na kuachiwa.

Amesema kikao hicho kilihusu uchaguzi wa Bawacha Manispaa ya Bukoba na Mdee alikuwa ni miongoni mwa viongozi walioalikwa ambapo aliambatana na Katibu wa Baraza hilo, Grace Tendega.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha jana wamekusanyika kwa makundi nje ya kituo cha Polisi Bukoba wakifuatilia hatima ya dhamana ya Mbunge huyo.

Jitihada za Mwananchi kumpata kamanda wa Polisi mkoani humo hazijazaa matunda kwani ofisini kwake hayupo wala simu zake za mkononi hazipokelewi.

UPDATE
Jeshi la Polisi limemuachia Mbunge huyo wa Kawe aliyeshikiliwa tangu jana baada ya kudhaminiwa na Watu wawili‬

Ametakiwa kuripoti Kituoni hapo baada ya mwezi mmoja au muda wowote atakapohitajika‬
 
Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Messages
4,269
Points
2,000

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2019
4,269 2,000
Jeshi la Polisi limezingira ukumbi wa kikao cha semina ya kuwajengea Uwezo BAWACHA, na kumkamata Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa ambaye ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee
Halima Mdee, licha ya jana kuzuiwa kufanya mkutano akiwa mkoani Simiyu, leo Julai 14, 2019 ameendelea na ziara yake Bukoba na kuweza kukutana na Baraza la Wanawake wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera.
Haya matukio muwe mnaya rekodi kwa ajili ya matumizi ya baadaye ,naona msululu wa wataokwenda the Hague na Yona .
 
state agent

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2019
Messages
1,273
Points
2,000

state agent

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2019
1,273 2,000
Acha wamkamate alisema mkuu wa mkoa wa simiyu ni mwanamke sasa wache wamzalishe mgumba huyu
Jeshi la Polisi limezingira ukumbi wa kikao cha semina ya kuwajengea Uwezo BAWACHA, na kumkamata Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa ambaye ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee

Halima Mdee, licha ya jana kuzuiwa kufanya mkutano akiwa mkoani Simiyu, leo Julai 14, 2019 ameendelea na ziara yake Bukoba na kuweza kukutana na Baraza la Wanawake wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera.
 
Ulimbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2009
Messages
2,265
Points
2,000

Ulimbo

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2009
2,265 2,000
Jeshi la Polisi limezingira ukumbi wa kikao cha semina ya kuwajengea Uwezo BAWACHA, na kumkamata Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa ambaye ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee

Halima Mdee, licha ya jana kuzuiwa kufanya mkutano akiwa mkoani Simiyu, leo Julai 14, 2019 ameendelea na ziara yake Bukoba na kuweza kukutana na Baraza la Wanawake wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera.
Hii CCM ni ya ajanu sana.
Jana wanawakewaccm walikuwa na mkutano la kumpongeza Rais kwa jinsi anavyoitekeleza ilani ya ccm. Cha ajabu mgeni wa heshima alikuwa mwanamume. Sasa sijui wanawake na wanaume wapi na wapi.
Chadema wao wakifanya mkutano kama huo ni kosa la jinai, ho mpliccm wanatumia nguvu kubwa kuwatawanya.

Kwa hali ilivya ni bora mahakama itoe tafsiri ya eno uchochozi na tuangalie kati ya viongozi wa ccm na viongozi wa vyama pinzani ni wepi wanatoa maneno ya kichochezi.

Ikibibi matukio yote/maneno yaliyo rekodiwa ya yatolewe tuone ukweli uko wapi.
 
Forum statistics

Threads 1,352,872
Members 518,197
Posts 33,068,209
Top