Bukoba: Aliyekuwa Meneja wa Ngara Farmers, Humphrey Kachecheba ajiua kutokana na msongo wa mawazo baada ya upotevu wa Tsh milioni 889

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
KMalimi1 (1).jpg

Aliyekuwa Meneja wa Chama cha Ushirika cha Ngara Farmers, Humphrey Kachecheba (50), amekutwa amefariki kwa kujiua kwenye nyumba ya wageni ya New Praise iliyopo Hamgembe Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Meneja huyo anadaiwa kujiua kutokana na kukabiliwa na msongo wa mawazo unaotokana na kufukuzwa kazi na kufunguliwa kesi mahakamani kwa upotevu Sh milioni 889, mali ya chama hicho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema meneja huyo wa zamani wa chama hicho cha Ushirika aligundulika ameshafariki Februari 3, mwaka huu saa tatu usiku akiwa chumba namba cha nyumba hiyo ya wageni.

Amesema uchunguzi wa awali wa Polisi, Kachecheba ambaye alikuwa mkazi wa Bunazi Kyaka alichukua chumba katika nyumba hiyo ya wageni tangu Januari 29 mwaka huu saa nne asubuhi akitokea Wilaya ya Ngara alikokuwa akifanyia kazi na aliendelea kuishi hapo hadi alipogundulika akiwa amefariki Februari 3 mwaka huu.

“Kwa muda wote inadaiwa alikuwa anashinda ndani ya chumba hicho amelala kila siku na kutoka saa mbili usiku na kurudi saa nne usiku.

“Chanzo halisi bado kinachunguzwa lakini hata hivyo kuna ushahidi mkubwa kuwa alijiua kwa sumu kutokana na msongo wa mawazo kufuatia kufukuzwa kazi na mwajiri wake jambo ambalo limethibitishwa na barua aliyokutwa nayo.

Mwili wa Kachecheba uligunduliwa na mhudumu na nyumba hiyo ya wageni, Odetha Edmund wakati alipotaka kufanya usafi ndani ya chumba hicho, baada ya kugonga mlango bila kupata majibu kutoka kwa mteja wake huku mlango ukiwa umefungwa kwa ndani.

Chanzo: Mtanzania
 
CCM Bana. Niliona mwanalumumba Barbaosa kwenye avatar kaweka picha ya marehemu Kobe akimaanisha ana uchungu sana na kifo chake wakati juzi alikuwa na wanaccm wenzake wakishangilia maamuzi ya wanaccm kumnyima Zitto haki ya kuishi.
Anajifanya kusikitika kuliko msiba wa ndg yake
Labda anamjua kobe

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM Bana. Niliona mwanalumumba Barbaosa kwenye avatar kaweka picha ya marehemu Kobe akimaanisha ana uchungu sana na kifo chake wakati juzi alikuwa na wanaccm wenzake wakishangilia maamuzi ya wanaccm kumnyima Zitto haki ya kuishi.
Barbarosa hawezi kuwa katili wa kiwango hicho bwashee!
 
Polisi kwanini wamefikia hitimisho mapema la kuwa ni msongo wa mawazo, je kama hakuhusika na upotevu huo ila ni watu wengine ambao walihisi atawataja na hivyo kumuwahi?

Polisi wasikimbie majukumu yao ya upelelezi wajipe muda kutafuta chanzo halisi cha kifo
 
Back
Top Bottom