Buguruni: Bwana harusi adai mahari baada ya kukimbiwa na bibi harusi aitwaye Asha

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
BWANA harusi aliyekimbiwa na bibi harusi, Omary Mohamed, amesema baada ya tukio hilo amelazimika kudai fedha zake za mahari ili aweze kuendelea na maisha yake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Omary alisema kwa sasa hawezi kusema lolote zaidi ya kusubiri kulipwa fedha zake madai ambayo ameyawasilisha kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule Manispaa ya Ubungo.

“Kwa sasa hatua ninayosubiri ni kulipwa fedha zangu. Na muda huu nipo nyumbani kwangu Buguruni Mtaa wa Ghana, lakini unanihoji badala hata kunitumia hata hela ya kahawa,” alisema kwa kifupi Omary.

Kauli ya bwana harusi huyo inatokana na tukio lililotokea juzi baada ya bibi harusi mtarajiwa aliyefahamika kwa jina la Asha Mohamed mkazi wa Kilungule Wilaya ya Ubungo kumkimbia bwana harusi na mshenga wake wakiwa wamepigwa butwaa.

Tukio hilo lilitokea saa 7 mchana jana ambapo bwana harusi mtarajiwa aliachwa …..
 
Ndio tatizo la bint kulazimishwa aolewe na fulani! Mwisho wa siku aibu
 
Bwana harusi yuko sahihi kuomba mali zake zirudi, kwa sababu mahari zilitolewa ili kupata mke, sasa mke hayupo. Kwa hiyo mkataba umevunjika na kila upande urudi kama walivyokuwa awali kabala ya mkataba (statu quo)
 
Inamana hadi sasa kunamambo ya kulazimaishana ndoa
Usishangae mkuu mm kuna dem nataka kumuoa kumbe dingi yake ashamchagulia mume. Dem kaja kustuka mzee anafanya mipango kimyakimya...
 
BWANA harusi aliyekimbiwa na bibi harusi, Omary Mohamed, amesema baada ya tukio hilo amelazimika kudai fedha zake za mahari ili aweze kuendelea na maisha yake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Omary alisema kwa sasa hawezi kusema lolote zaidi ya kusubiri kulipwa fedha zake madai ambayo ameyawasilisha kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule Manispaa ya Ubungo.

“Kwa sasa hatua ninayosubiri ni kulipwa fedha zangu. Na muda huu nipo nyumbani kwangu Buguruni Mtaa wa Ghana, lakini unanihoji badala hata kunitumia hata hela ya kahawa,” alisema kwa kifupi Omary.

Kauli ya bwana harusi huyo inatokana na tukio lililotokea juzi baada ya bibi harusi mtarajiwa aliyefahamika kwa jina la Asha Mohamed mkazi wa Kilungule Wilaya ya Ubungo kumkimbia bwana harusi na mshenga wake wakiwa wamepigwa butwaa.

Tukio hilo lilitokea saa 7 mchana jana ambapo bwana harusi mtarajiwa aliachwa …..

Mambo ya kulazimisha kuoa Mwanamke asiyekupenda ndo hayo sasa!
 
Back
Top Bottom