Kijana Msomali
Member
- May 10, 2012
- 92
- 71
Leo Mawaziri wa Fedha wa Nchi za Afrika ya Mashariki wataanza kusoma Bajeti za serikali zao kwa mwaka wa Fedha wa 2012/2013.
Waziri wa Fedha wa Tanzania Dr. William Mgimwa atasoma bajeti ya Tanzania kwa mwaka 2012/2013 leo Mjini Dodoma ambayo ni SH. 15 TRILLION, hii ni takriban Dolari za Kimarekani 9.43 Billion.
Bajeti ya Tanzania ya mwaka huu itakuwa na vipaombele saba, Vipao mbele vitano kati ya hivyo ni
1. Deni la Taifa ( Shs. 2.7 Trillion)
2.Wizara ya Ujenzi (Shs. 1 Trillion)
3.Wizara ya Ulinzi ( Shs. 920 Billion)
4.Wizara ya Elimu ( Shs. 721 Billion)
5.Wizara ya Nishati na Madini ( Shs. 641 Billion)
Kwa upande wa Kenya, Bajeti ya mwaka 2012/2013 ambayo itasomwa na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Njeru Githae ni Shilingi za Kenya 1.4 Trillion, ambazo ni takriban Dolari za Kimarekani 16.87 Billion.
Kipaombele kikubwa katika bajeti ya Kenya ya mwaka huu ni Wizara ya Ulinzi na Uslama, ambayo imepangiwa Shilingi za KENYA 13.4 Billion.
Tofauti ya Bajeti ya Kenya ( USD 16.87 BILLION) na ile ya Tanzania ( USD 9.43 BILLION) ni Dolari za Kimarekani 7.43 Billion.
Hii ina maana ya kuwa Bajeti ya Kenya inazidi ile ya Tanzania kwa 44%.
Nini implications ya tofauti hii kubwa katika masuala ya
1. Kuongeza pato la ndani la taifa (G.D.P)
2. Kupunguza mfumuko wa bei ( Inflation)
3. Kuongeza Ajira Nchini ( Job Creation)
4. Kupunguza Umaskini na Kuongeza Ustawi wa Jamii ( Poverty Eradication and Social Welfare Improvement)
5. Kupunguza tofauti za kipato miongoni mwa matabaka mbali mbali nchini (Income Gap Reduction).
6. Kuongeza ushindani wa Makampuni ya Tanzania katika soko la Afrika Mashariki.