Budget Speech of the 2012/2013 Fiscal Year

Budget 2012/2013 ndio hiyo ipo sokoni!.

Kila mwaka stori ni zile zile. Pamoja na hali ngumu ya maisha na uchumi kwa ujumla Budget zetu zinaendelea kila mwaka kumkandamiza mwananchi wa kawaida!. Najaribu kufikiria labda wanapokuwa kwenye hivyo vikao vyao vya budget ( sijui mwaka huu vimefanyikia wapi! ) wanajiangalia wao kwanza kwamba wao ndio wenye nchi na wengine kina sisi ni wapangaji katika nchi ya TZ.

Kweli wabunge ndio wawakilishi wetu bungeni, lakini kwenye ishu nyeti kama hii sidhani kama ni busara kuwategemea wabunge moja kwa moja katika kumtetea mwananchi wa kawaida sababu tunaelewa wabunge wetu wengi ndio walewale wanatetea masilahi yao binafsi kwanza then wananchi wao baadae.

Mi nafikiri wananchi tusikae kimya kusubiria tu watakavyolimaliza huko bungeni sababu sisi ndio waathirika wakubwa. sababu hii budget ikishapita basi ndio utakuwa mzigo wetu tena mkubwa kwa mwaka mwingine tena.

Mungu ibariki Tanzania na wapangaji wake.

kweli budget ipo SOKON,lakin haina mnunuz,,,,haina mteja na hmna mwenye nia ya kuinunua,,,reason BAJETI NI YAO SI YA WATANZANIA
 
Mgimwa nilikuwa na matumaini nawe but umeendeleza suala la kucopy na kupaste!
Utaleta kisingizio kuwa ulipewa mda mfupi!
 
Hili faili linanipa shida napata msg kama limekuwa corrupted.
Niongeomba kama inawezekana kutupandishia hapa Pdf. Sijui kama wenzangu wameweza kulifungua hilo faili la ms word (.doc)

Mwenyewe nimeshikwa na haja zote mbili baada ya kushindwa kudownload hii maneno!
 
Mwenyewe nimeshikwa na haja zote mbili baada ya kushindwa kudownload hii maneno!
Pole sana mkuu, nilichelewa kurejea tena hapa hata hivyo nimeishaiweka kwa PDF so bila shaka itafunguka...Nakutakia usomaji mwema.
 
Back
Top Bottom