Budget Speech of the 2012/2013 Fiscal Year

Hapo kwenye kupandisha kiwango cha PAYE ndipo inaonyesha ni kiasi gani hawa wataalamu wamewachoka wafanyakazi na walivyoishiwa ubunifu.
Nchi hii inaendeshwa kwa kodi za wafanyakazi pamoja na wala kilaji.
Huu utakuwa ni mwaka wa maumivu makali zaidi kuliko hata mwaka unaomalizika.
Shame on you Mgimwa, shame on you ccm.
 
HON. DR. WILLIAM AUGUSTAO MGIMWA (MP.),
INTRODUCING TO THE NATIONAL ASSEMBLY, THE ESTIMATES OF GOVERNMENT REVENUE AND EXPENDITURE
FOR THE FISCAL YEAR 2012/2013

Download the attachment to continue reading...

Hili faili linanipa shida napata msg kama limekuwa corrupted.
Niongeomba kama inawezekana kutupandishia hapa Pdf. Sijui kama wenzangu wameweza kulifungua hilo faili la ms word (.doc)
 
Napata the same problem. Please fix. nina njaa ya kujua PAYE imekaaje?

Mkuu Mlachake
Upande wa PAYE iko hivi
(i) "Adjust PAYE threshold as a result of enhancement of salary scales from Tshs 135,000 to Tshs 170,000".
 
Naona kupanda kwa gharama za kupiga simu au kutuma sms

"Increase Excise Duty on Airtime from 10 percent to 12 percent."

Wale tunaotegemea kuagiza magari toka japan imekula kwetu

"I propose to make amendments in the law that grants motor vehicle exemptions to various beneficiaries through Government Notices so that importation motor vehicles aged more than 8 years from the year of manufacture will now be subjected to the excise duty of 20 percent. The measure is intended to discourage importation of obsolete vehicles and preserve/protect environment." Kweli aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa.
Naendelea kuipiti......

Serikali ya ccm ilikuja kwa watanzania 2010 kuomba kazi ya kuwatumikia wananchi,kwa hiyo kwa tafsiri sahihi hawa ni wafanyakazi na watanzania ni mabosi wao.
Kwa hiyo kazi kubwa ya waajiriwa ccm ni kulinda watanzania na mali zao,kukusanya kodi,kusaini mikataba ya kimataifa kwa ajili ya watanzania na kukopa inapobidi kwa maslahi ya nchi.

Kinachonishangaza katika bajeti waajiriwa ccm kila sh 15 wanayopata kwa kodi,kwa misaada na kwa kukopa wao wafanyakazi wanakula 10 tajiri yao anabakiwa na sh 5 na vichekesho zaidi ni hapa,kwa kuwa wameshakula 75%na bosi 25% deni waliloingia bosi wao analipa 100% badala ya kugawana kama walivyogawana cash.

Kichekesho kingine badala wapate mapato kutoka katika rasilimali za nchi wanarudi kwa waajiriwa wao walewale,mchana wanawapa hela usiku wanawanyang'anya.
Huwezi kuongeza mishahara na kupandisha kodi ya bidhaa ukasema umemsaidia huyo mtu.

Nawakilisha wakuu.
 
Hapo kwenye bold ulitakiwa useme nawasilisha.
 
Budget 2012/2013 ndio hiyo ipo sokoni!.

Kila mwaka stori ni zile zile. Pamoja na hali ngumu ya maisha na uchumi kwa ujumla Budget zetu zinaendelea kila mwaka kumkandamiza mwananchi wa kawaida!. Najaribu kufikiria labda wanapokuwa kwenye hivyo vikao vyao vya budget ( sijui mwaka huu vimefanyikia wapi! ) wanajiangalia wao kwanza kwamba wao ndio wenye nchi na wengine kina sisi ni wapangaji katika nchi ya TZ.

Kweli wabunge ndio wawakilishi wetu bungeni, lakini kwenye ishu nyeti kama hii sidhani kama ni busara kuwategemea wabunge moja kwa moja katika kumtetea mwananchi wa kawaida sababu tunaelewa wabunge wetu wengi ndio walewale wanatetea masilahi yao binafsi kwanza then wananchi wao baadae.

Mi nafikiri wananchi tusikae kimya kusubiria tu watakavyolimaliza huko bungeni sababu sisi ndio waathirika wakubwa. sababu hii budget ikishapita basi ndio utakuwa mzigo wetu tena mkubwa kwa mwaka mwingine tena.

Mungu ibariki Tanzania na wapangaji wake.
 
Mi sikubali kuitwa mpangaji kwenye nchi yangu, itabidi kieleweke!!!.
 
Back
Top Bottom