Buchosa, Sengerema: Mwalimu asakwa kwa kuoa mwanafunzi

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Ofisa elimu sekondari wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Benjamin Siperato
Buchosa. Ofisa elimu sekondari wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Benjamin Siperato ameagiza mwalimu mmoja wa Sekondari ya Nyakasungwa kukamatwa na kuwekwa mahabusu baada ya kukaidi agizo la kumsalimisha ofisini kwake mwanafunzi anayedaiwa kumuoa.

Mwanafunzi huyo anayepaswa kuwa kidato cha tano mwaka huu, anadaiwa kuolewa na mwalimu wake tangu mwaka jana alipohitimu kidato cha nne.

Siperato alisema ofisi yake inaendelea kufuatilia kwa makini suala hilo huku akionya kuwa hatua zaidi zitachukuliwa dhidi ya mwalimu yeyote atajayekiuka maadili.

“Licha ya kuchukua hatua dhidi ya mwalimu, ofisi yangu inafanya kila linalowezekana kumsaidia mwanafunzi huyo aliyeathiriwa na kitendo cha mwalimu wake,” alisema Siperato.

Mwalimu huyo anatuhumiwa kumuoa aliyekuwa mwanafunzi wake mwaka jana ambaye alihitimu mwaka 2016 na kupata daraja la tatu la alama 25, hivyo kuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano shule moja iliyoko mkoani Tanga.

Naye mkazi wa kijiji cha Nyakasungwa, Faustine Juma aliunga mkono hatua zilizochuliwa na ofisa elimu za kumsweka ndani mwalimu na kuomba sheria ichukue mkondo wake.

Akizungumzia suala hilo, mkuu wa sekondari hiyo, Safari Mashimba alisema hana taarifa hiyo na kwamba anachofahamu alimuaga kuwa ameitwa wilayani.

Mwanasheria anayetoa msaada wa kisheria wilayani Sengerema, Victor Salala alisema kitendo alichofanya mwalimu huyo ni kosa hivyo anatakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha.

Mwalimu huyo alibainika kumuoa mwanafunzi baada ya baadhi ya wanakijiji wa Nyakasungwa kulalamika kuwa kilichofanyika ni kinyume cha maadili ya kazi yake.

Wanakijiji hao walisema mwalimu huyo akiwa mlezi wa mwanafunzi huyo anapaswa kuwajibishwa.

Awali, mwalimu huyo akizungumza mbele ya mratibu elimu kata ya Nyakasungwa, Mihigo Mazima alikiri kuishi na binti huyo.

Alisema aliamua kuishi naye baada ya familia yake kushindwa kumsomesha na kwamba, ana mpango wa kumpeleka shule baadaye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama alishamaliza kidato cha nne na alikuwa hajaingia kidato cha tano kosa liko wapi?
 
Wanakijiji hao walisema mwalimu huyo akiwa mlezi wa mwanafunzi huyo anapaswa kuwajibishwa.

Awali, mwalimu huyo akizungumza mbele ya mratibu elimu kata ya Nyakasungwa, Mihigo Mazima alikiri kuishi na binti huyo.

Alisema aliamua kuishi naye baada ya familia yake kushindwa kumsomesha na kwamba, ana mpango wa kumpeleka shule baadaye.

Enzi zile wanakijiji walichukizwa na aina hii ya uchafu kama vilw anavyochukiwa kibaka, vivyo hivyo walipaswa kufanya kwa mwalimu husika

Je somo la maadili vyuoni linatiliwa mkazo? au haya ni matokeo ya mtu kusomea ualimu kwakuwa amefanya vibaya mitihani na siyo anaipenda kazi toka moyoni mwake?
 
Ofisa elimu sekondari wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Benjamin Siperato
Buchosa. Ofisa elimu sekondari wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Benjamin Siperato ameagiza mwalimu mmoja wa Sekondari ya Nyakasungwa kukamatwa na kuwekwa mahabusu baada ya kukaidi agizo la kumsalimisha ofisini kwake mwanafunzi anayedaiwa kumuoa.

Mwanafunzi huyo anayepaswa kuwa kidato cha tano mwaka huu, anadaiwa kuolewa na mwalimu wake tangu mwaka jana alipohitimu kidato cha nne.

Siperato alisema ofisi yake inaendelea kufuatilia kwa makini suala hilo huku akionya kuwa hatua zaidi zitachukuliwa dhidi ya mwalimu yeyote atajayekiuka maadili.

“Licha ya kuchukua hatua dhidi ya mwalimu, ofisi yangu inafanya kila linalowezekana kumsaidia mwanafunzi huyo aliyeathiriwa na kitendo cha mwalimu wake,” alisema Siperato.

Mwalimu huyo anatuhumiwa kumuoa aliyekuwa mwanafunzi wake mwaka jana ambaye alihitimu mwaka 2016 na kupata daraja la tatu la alama 25, hivyo kuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano shule moja iliyoko mkoani Tanga.

Naye mkazi wa kijiji cha Nyakasungwa, Faustine Juma aliunga mkono hatua zilizochuliwa na ofisa elimu za kumsweka ndani mwalimu na kuomba sheria ichukue mkondo wake.

Akizungumzia suala hilo, mkuu wa sekondari hiyo, Safari Mashimba alisema hana taarifa hiyo na kwamba anachofahamu alimuaga kuwa ameitwa wilayani.

Mwanasheria anayetoa msaada wa kisheria wilayani Sengerema, Victor Salala alisema kitendo alichofanya mwalimu huyo ni kosa hivyo anatakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha.

Mwalimu huyo alibainika kumuoa mwanafunzi baada ya baadhi ya wanakijiji wa Nyakasungwa kulalamika kuwa kilichofanyika ni kinyume cha maadili ya kazi yake.

Wanakijiji hao walisema mwalimu huyo akiwa mlezi wa mwanafunzi huyo anapaswa kuwajibishwa.

Awali, mwalimu huyo akizungumza mbele ya mratibu elimu kata ya Nyakasungwa, Mihigo Mazima alikiri kuishi na binti huyo.

Alisema aliamua kuishi naye baada ya familia yake kushindwa kumsomesha na kwamba, ana mpango wa kumpeleka shule baadaye.

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani kwa kuweka hii habari kwenye jukwaa hili,mods naomba waihamishie jukwaa husika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyinyi mnakataza mimba au mnakataza kuoa maana sheria ikikosa tafsiri sahihi ni ujinga. Hivi hiyo sheria inatumika kwa aina gani ya mwanafunzi au inaangalia umri ? Pia msipende kuweka sheria zinazokataa mazingira jamii wanayoishi. Mfano wa sheria nyingi tulizo nazo zinafanya kazi mijini na sio vijijini, rejea kauli za watawala wetu.
 
Tatizo ni kwa kua tu ni mwalimu. Watu wanategemea walimu waishi kama malaika.
 
Back
Top Bottom