Buchosa: Mwanafunzi adaiwa kuchoma Mabweni ya Shule baada ya kusimamishwa Masomo

Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Nyehunge iliyoko wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, Lucas Moshi anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuchoma mabweni ya shule hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Sanyi Ganga ameyasema hayo Septemba 29, 2021 baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea uharibufu mkubwa na vifaa vya wanafunzi uliosababishwa na moto huo uliotokea Septemba 27 mwaka huu.

DC Ganga amesema mabweni mawili ya shule hiyo iliyopo katika halmashauri ya Buchosa yanayotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita yaliungua moto, hivyo wanafunzi hao kuhamishiwa chumba kimoja cha darasa kwa ajili kulala.

Amesema kabla ya mwanafunzi huyo kusimamishwa, alisimamishwa masomo na kutakiwa kufika shuleni na wazazi, lakini hakufanya hivyo, badala yake alikuwa akizunguka maeneo ya shule.

Mkuu wa shule hiyo, Adofu Domician amesema tukio hilo ambalo limetokea mara mbili kwa muda wa siku mbili limemshtua na kuomba Serikali ifanye uchunguzi kwa kina na kusaidia shule hiyo.

Amesema hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa Wala kupoteza maisha, mbali ya mali za wanafunzi zilizoteketea kwa moto zikiwemo nguo, madaftari pamoja na magodoro na kuiomba Serikali pamoja na wadau wa elimu kujitokeza kusaidia wanafunzi hao.

Amesema siku ya tukio, mwanafunzi huyo alikuwepo eneo la shule na ndipo alipokamatwa kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano na Polisi.

Mwananchi
Mkuu wa shule ni kilaza,

Umemsimamisha masomo mwanafunzi bila kumuesikodi kwa mzazi wake?
 
Wanamsingizia Dogo.
Kuna uwezekano Dogo amechoma kweli. Na kama hakutakiwa kuonekana eneo la shule yeye alikuwa anazunguka zunguka kufanya nini hapo?Huyu dogo yaonekana ana usela wa kizamani na anavuta bange pengine. Walimu na Mkuu wa shule siyo wapumbavu wamsingizie tu bila sababu. Huyu adhibitiwe atasema tu. Angeweza kusababisha madhara makubwa sana huyu
 
Mkuu wa shule ni kilaza,

Umemsimamisha masomo mwanafunzi bila kumuesikodi kwa mzazi wake?
Zamani wakati kwa shule za serikali ilikuwa mwanafunzi akisimamishwa masomo anapewa hiyo 'eskodi'unayosema hadi kwa wazazi wake. Siku hizi sidhani kama utaratibu huo bado upo. Na gharama atalipia nani hizo nauli maana utaratibu wa kusafiri kwa waranty ulikufa siku nyingi sana
 
Utaratibu ni mzazi anapigiwa simu anaitwa shuleni anakabidhiwa mtoto wake anaondoka naye.

Siku ya kurudi shule mzazi anapaswa aje naye shuleni kumkabidhisha na adhabu juu
 
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Nyehunge iliyoko wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, Lucas Moshi anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuchoma mabweni ya shule hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Sanyi Ganga ameyasema hayo Septemba 29, 2021 baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea uharibufu mkubwa na vifaa vya wanafunzi uliosababishwa na moto huo uliotokea Septemba 27 mwaka huu.

DC Ganga amesema mabweni mawili ya shule hiyo iliyopo katika halmashauri ya Buchosa yanayotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita yaliungua moto, hivyo wanafunzi hao kuhamishiwa chumba kimoja cha darasa kwa ajili kulala.

Amesema kabla ya mwanafunzi huyo kusimamishwa, alisimamishwa masomo na kutakiwa kufika shuleni na wazazi, lakini hakufanya hivyo, badala yake alikuwa akizunguka maeneo ya shule.

Mkuu wa shule hiyo, Adofu Domician amesema tukio hilo ambalo limetokea mara mbili kwa muda wa siku mbili limemshtua na kuomba Serikali ifanye uchunguzi kwa kina na kusaidia shule hiyo.

Amesema hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa Wala kupoteza maisha, mbali ya mali za wanafunzi zilizoteketea kwa moto zikiwemo nguo, madaftari pamoja na magodoro na kuiomba Serikali pamoja na wadau wa elimu kujitokeza kusaidia wanafunzi hao.

Amesema siku ya tukio, mwanafunzi huyo alikuwepo eneo la shule na ndipo alipokamatwa kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano na Polisi.

Mwananchi
Wazazi wake wajenge hiyo shule
 
Back
Top Bottom