BRT ikitushinda tuachane na reli!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kama mwendokasi ikistushinda basi nasema hata tusipoteze fedha kutaka kujenga reli mpya kwani itakuwa ni miujiza kama tutaweza kuiendesha nayo pia (reli) baada ya miaka 10 itakuwa tu kama reli ya kati ya leo au TAZARA!

Hivyo BRT / DART ni lazima ifanikiwe kwani haihitaji uwezo mkubwa wa kuitunza kama reli.
 
Siku zote nyumba haianzi kujengwa kwenye linta au bati...

Nyumba inahitaji msingi mzuri.. Kama tulishaona elimu haina maana na tunaiendesha kisiasa siasa tukijua watoto wetu tutawapeleka kwenye shule nzuri binafsi zinazotoa elimu bora na vyuo tunawapeleka nje ya nchi na kuacha elimu yetu ikiendelea kuwa duni kila kukicha haya tunayoyaona kwenye DART ndio matunda yake.. Na sio huko tu, kila mahali ni ovyo.. Hata vyoo vya pale Airport Mwalimu Nyerere ni vichafu utafikiri vya stand ya Ubungo..

Nchi hii ifike mahali tuchague vipaumbele vitatu tu na bajeti yetu yote iende huko na ELIMU lazima iwepo.. Kujidanganya tutajenga viwanda wakati hiyo bajeti ya viwanda ni Billion 80 tu ni hadithi nyingine tunaenda kuifeli.. Tatizo letu kubwa nchi haina dira na tunapapatikia kufanya kila kitu kwa muda mmoja..

Kuna Methali inasema "MSHIKA VYOTE KWA PUPA HUKOSA VYOTE"
 
Naunga hoja, kwanza mimi nakwenda mbali zaidi na kusema hata tusema kwa miaka 5 kipaumbele kimoja tu labda kwa mfano tuseme Umeme, kila kitu kiende kwenye Umeme na ili miaka 5 ikiisha basi na tatizo la umeme linakuwa limekwisha!
Lkn hili la kutaka kufanya mambo mengi kwa wkt mmoja sijui kama tutafanikiwa, kwa mfano nina wasiwasi sana na hili la kujenga Reli Mpya ingawaje wengi hawatanielewa lkn sidhani kama tuko tayari kuendesha hizo Reli kwani hizi Reli zilikuwepo na zimekufa kwanza Reli ya kati na Ta-Mo-Ar halafu na sasa TAZARA nayo imekufa, sasa swali la kujiuliza ni kwanini hizi Reli zimekufa?
Bila ya kupata hilo jibu hata hizo mpya zitakufa pia kwani ni swala la muda tu, kama hakuna kilichobalika...
 
Na ajabu unaweza kukuta hata hilo swali wataalamu wetu hawakujiuliza kabla hata ya kuifufua hiyo reli yenyewe.. Mara nyingine tunajikuta tunaingia kwenye miradi ambayo hata hatujaifanyia utafiti wa kitaalamu eti kwasababu tu majirani zetu wanafanya hicho kitu..
 
Naunga hoja, kwanza mimi nakwenda mbali zaidi na kusema hata tusema kwa miaka 5 kipaumbele kimoja tu labda kwa mfano tuseme Umeme, kila kitu kiende kwenye Umeme na ili miaka 5 ikiisha basi na tatizo la umeme linakuwa limekwisha!
Lkn hili la kutaka kufanya mambo mengi kwa wkt mmoja sijui kama tutafanikiwa, kwa mfano nina wasiwasi sana na hili la kujenga Reli Mpya ingawaje wengi hawatanielewa lkn sidhani kama tuko tayari kuendesha hizo Reli kwani hizi Reli zilikuwepo na zimekufa kwanza Reli ya kati na Ta-Mo-Ar halafu na sasa TAZARA nayo imekufa, sasa swali la kujiuliza ni kwanini hizi Reli zimekufa?
Bila ya kupata hilo jibu hata hizo mpya zitakufa pia kwani ni swala la muda tu, kama hakuna kilichobalika...

Mkuu Leo umekuja kizalendo zaidi, safi sana. Haya ni maswali muhimu sana ambayo MTU yeyote mwenye akili timamu lazima ajiulize.

Tukishindwa kabisa, tuje na Sera bora za kuhakikisha nchi inanufaika na uwekezaji, tuwakabidhi haya mambo, sisi ni wazi kabisa tatizo lipo kwenye usimamizi na imeshatushinda.

Ni kitu gani cha serikali kinaendeshwa kwa ufanisi? Biashara za Bakhresa zinaendeshwa vizuri sana, Leo hii ukimkabidhi kivuko cha Kigamboni ataleta mapinduzi ya ajabu na ataingiza pesa sana, He huyu jamaa anapesa kuliko serikali au ana usimamizi mzuri?

Naunga mkono hoja, hii miradi ipitiwe kwa umakini kama INA tija, tuangalie tumekosea wapi na kujisahihisha badala ya kuongeza mizigo mipya wakati iliyopo inatushinda.
 
Naunga hoja, kwanza mimi nakwenda mbali zaidi na kusema hata tusema kwa miaka 5 kipaumbele kimoja tu labda kwa mfano tuseme Umeme, kila kitu kiende kwenye Umeme na ili miaka 5 ikiisha basi na tatizo la umeme linakuwa limekwisha!
Lkn hili la kutaka kufanya mambo mengi kwa wkt mmoja sijui kama tutafanikiwa, kwa mfano nina wasiwasi sana na hili la kujenga Reli Mpya ingawaje wengi hawatanielewa lkn sidhani kama tuko tayari kuendesha hizo Reli kwani hizi Reli zilikuwepo na zimekufa kwanza Reli ya kati na Ta-Mo-Ar halafu na sasa TAZARA nayo imekufa, sasa swali la kujiuliza ni kwanini hizi Reli zimekufa?
Bila ya kupata hilo jibu hata hizo mpya zitakufa pia kwani ni swala la muda tu, kama hakuna kilichobalika...

Hata swali kwanini viwanda vilikufa sidhani kama kuna mtu amejiuliza na kujibu honestly. Hata huu mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliokwisha sikumbuki kama watu walikaa na kkuchambua mafanikio na changamoto zake sincerely kabla ya kuembark kwenye huu mwingine. Bila kujiuliza maswali magumu huwezi kujirekebisha ulipokosea. Ndio maana wanakimbilia kuzima taa tusione wakiulizwa maswali bungeni. Mungu atuhurumie hatuna pa kuponea.
 
UDA,KAMATA,MABASI YA RAILWAYS,MABASI YA WATOTO WA SHULE DSM,RETCOS ZOTE

Ziko wapi na hili dude linaelekea huko huko,sababu licha kuwa hatujawahi kufanikiwa kwenye biashara yoyote ya usafiri huu ulianza kwa ujanja mwingi
 
Usimamizi mbovu, uzembe, ubadhilifu, wizi ni baadhi ya sababu za vifo vya mashirika ya umma. Kingine kinachoyauwa ni serikali yenyewe.
---- Kwenye kituo cha BRT pale Ubungo ukifika na noti ya sh1000 unaweza usipate tiketi, wakatisha tiketi wapo tu vidirishani wanakutizama wanadai hawana chenji, ukatafute pesa taslimu. Mtu anaamua kwenda kupanda daladala. Hawa wanajua kuwa hata wasipokuuzia tiketi mshahara wao upo palepale.
---- Kwenye vivuko; makusanyo yote yanapelekwa serikalini halafu huko serikalini kutoa pesa za kuvifanyia matengenezi vivuko ni shida hadi injini zinakuwa hoi bin taabani. Mfano kivuko cha Kigamboni. hata maboya ya kujiokolea yapo kwenye hali mbaya hususan yale ya kuvaa. Na kinabeba watu wengi mmno.
---- Inabidi ifike pahali watu wafanye kazi kibiashara, yaani mfanyakazi awekewe lengo, sio mradi siku iingie hata kama hujafanya kazi.
 
suala la sifa pia linachangia. kuna inshu ya kuwa na vipaumbele kama taifa,leo kila anaeingia madarakani anataka aonekane amefanya kitu unique bila kujali aliyetoka alikuwa na mipango gani na imeishia wapi. unawezaje kuzungumzia mapinduzi ya viwanda ilhali kilimo,umeme na elimu viko katika hali duni kabisa? tungeanzia chini kabisa kama taifa bado hatujachelewa. kuna mwaka nilisikiliza vipaumbele 11 vya serikali ya jk nikajua kumbe huwa vinatajwa tu kwa sababu huo ni utaratibu.
 
Haya mabasi ya mwendo Kasi ya kidumu Sana Ni miaka mitatu(3) kwa jinsi yanavyopata ajali kila kukicha.
 
Back
Top Bottom