Brother wangu kama masihara ametimiza miaka 40 akiwa bado kula kulala

Ndio yupo kwao hivyo tayari na hadi thread umemuundia sijui je angekuwa kwenu/kwako ungemfanyaje...

Wazazzi wake wanamlisha wanamlaza na kila kitu wameona poa tu ila wewe sasa unaona kama kuna anayepunjikaz vile

Only for jokes above



Tuingie kwenye uhalisia sasa...
Hilo ni tatizo na wameliunda bomu hilo wazazi wake wenyewe (tena litawalipukia hata msiohusika). Kwakuwa ni kaka wa damu basi kumsaidia ni wajibu na katika kumshauri kwanza uzingatie vitu hivi;
1.Masters ya kile alichosomea
2.Kama ana mke/mchumba
3.Kama ana watoto
4.Kama ana kikazi chake cha deiwaka
5.Mtazamo/msimamo/malengo na matarajio yake
 
Chunguza vema, wasomi wana mambo. Usikute kwenye utafiti wake wa hiyo shahada ya umahiri, moja ya kitu alichojifunza ni hicho--kutokuanza kujitegemea mapema. Hvyo, huenda anatekeleza aliyojifunza kwa vitendo. Safi sana
Unamaanisha atatekeleza aliyojifunza akishakuwa mzee? 🤔
 
hapana umefika mbali ni ile buguzi na mama walikuwa hawaelewani na huyo bro alikuwa anashataki kuhusu sijui kunyimwa chakula

mzee wangu usimwambie kitu kuhusu ndugu zake wanajaa hapo home atakuja
We inaonekana ni mtoto wa nje tu! Mama yako aliolewa mke wa pili ama?
 
Kumfukuza mtoto akapange uswahilini kwa wachawi ndio kumfundisha maisha?

Kikubwa watoto wapelekwe shule na kumfundisha Plan B kama kilimo na biashara. Siku yupo vizuri atahama. Ila kumfukuza nyumbani kijana wangu ambaye katoka chuo na hana ajira hilo hapana. Akipata ajira ataondoka ila sio kumfukuza kama mbwa mtoto wangu wa kumzaa eti ndio kumkomaza.
Watu wenye roho za kichawi hao wanahisi kufukuza ndio solution! Mi watoto wangu wataishi home mpaka wachoke wao 😅 najua ajira zitakuwa hazipo ila ntajitahidi mie na mama yao tuwarithishe biashara mapema.
 
Kwa watoto kutoka familia Bora hiyo inawezekana ila kwa sisi watoto wa maskin n balaa hutoboi nakumbuka nlipofikisha miaka 19 tu pale home pakawa hapakaliki likaibuka bifu kubwa mm na faza yan akinikuta nimelala hadi saa mbili yanaanza maneno , akikuta naangalia Tv utaskia unaangalia tu hujui umeme unalipiwa vp, akikuta nmetangulia kula kabla ya wote utaskia unapenda kula tu ila hujui hata bei ya mchele.

Nikaanza kutafuta mishe mtaani nkichelewa kurud nakuta nmefungiwa geti na maelekezo yametolewa nisifunguliwe nilale hukohuko nlipoenda, wadogo zangu ndo wakawa wananifungulia kwa kuibaiba naingia kulala huku nanyata na asubuhi nasepa kabla yake, kwa dizain ile nisingetoboa hata 23 nkiwa home
Mzee kigogo aliamua kutumia mamlaka yake kukutimua kijanja😅
 
Wamama wa kiafrika hawa afu ukisepa ukajitafutie anapga smu mwanangu unahangaika s bora urudi nyumban, m ndo nlishaktaa kulelewa nishakua nipambane
Hahahahahah hakuna mama anayetaka mwanae ateseke ndio maana wale strong women hupambana ampenyeze mwanae kitengo mapema tu ili aishi vizuri hakuna raha kama mzazi kuona mtoto anafanikiwa kuwa na maisha yake mazuri tu, its a success story to them.

Sio umesomesha kwa gharama halafu mtoto anakuwa teja muokota makopo huku mama ni mhasibu mkuu wa BOT. Baba ni mwanasheria mkuu wa shirika labda NSSF. Kaa home tu kama kazi hakuna utapata tu, hii ndio kauli yao.
 
Back
Top Bottom