Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,970
- 45,848
Nikupe hongera kwa kumaliza nafasi yako uliyopewa kwa weledi, umeitendea vyema sana nafasi uliyoaminiwa na Rais.
Sioni umuhimu sana wa kukupa pole kwakua kilichotokea sio tatizo ili upewe pole kwani kupokezana ndio utaratibu tunaoishi nao binadamu.
Nikija kwenye kauli zako ulizozitoa baada ya huduma yako kwetu sisi Watanzania kusitishwa , kwamba ni wewe ndiye uliyeitoa CCM kwenye shimo, ni wewe ndiye uliyekaa maporini kwa siku 28, huku wengine wakikaa bara wakinywa bia, na ni wewe ndiye uliyeipa ushindi CCM, hapo mkuu wangu kwa heshima nataka nikuambie tu kuwa umeteleza, na unatakiwa utuombe radhi.
Hakuna anayepinga wala atakaye sahau mchango wako kipindi cha uchaguzi uliopita na kwa kutambua mchango wako ndio maana Mh. Rais alikupa nafasi kwa kukuamini kuwa ni mtu makini mwenye uwezo wa kusimamia jambo likafanikiwa, ila ni kwa kauli ndogo tu kama hiyo ambayo inaweza kufuta kila kitu ambacho umewahi kukifanya na ukasahaulika kabisa.
Mkuu, kuna wazee katika hii nchi wametenda mambo mazito sana, lakini hawakuwahi hata maramoja kusimama na kusema ni "mimi" nimefanya hiki na kile, kwa uchache tu, Mwl. Nyerere toka naanza kumfahamu huyu mzee, sijawahi kumsikia akisema kuwa ni mimi ndiye niliyefanya hiki na kile ili apate recognition yetu, karume, kawawa and the likes, wazee wote hao, hakuna kati yao aliyesimama na kusema "NI MIMI" ila mambo yao na upendo wao bado unaishi katika mioyo ya watanzania siku zote kwakua walichagua kuwatumikia wananchi, na sio kujitumikia wao wenyewe.
U MIMI ni mbaya sana mkuu Nape, U MIMI unaonesha ubinafsi na kupenda kutukuka, U MIMI ni UBEPARI ambao ndio umekua chanzo cha kuliangamiza Taifa hili.
Sikupenda kuyaandika haya ila nimeona nikukumbushe kuwa, U MIMI huo ulioutangaza Ni sumu mbaya sana ambayo isipoachwa mapema itarithishwa kwa vizazi vijavyo kwamba mtu lazima ufanye jambo kwa faida yako tu , na sio kwa faida ya wote.
CCM inajengwa na wote, wanachama wote, ila tunapeana nafasi na kusaidiana hivyo ndivyo vitu vinavyoipa nafasi CCM mpaka sasa kwakuwa inaheshimu mchango wa kila mwanachama , kwani kila mtu anaumuhimu kwa chama kwa nafasi yake.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.