Bro wangu kanichosha sana, nampiga chini leo leo! Nimechoka!

jf atutatui matatizo ya kifamilia kama yenu tena uache kuchezea na kudharau jukwa ahili malizana na ndugu zako atuitaji hata kujua umwamwaga ujammwaga ..ukioa njoo tukufunde hayo ndiomambo tunasaidia ahumu mwisho utatanza kutuandikia jamani nimepigwa na mama yangu mzazi...then tukusaidieje???

hapo na wewe UMEROPOKA tu...vyote ulivyoandika sio kweli...unaelewa maana ya MAHUSIANO??
mkosoe kwa lingine kama lipo mkuu...
 
Welcome to the world.

ungekuwa karibu ningekuambia tukutane tudiskas hili tatizo, maana excatly kama umepitia nyumbani kwangu.
Ukimtimua atatia akili, tena unachofanya atafute chumba kimoja cheap, mlipie miezi 3 afu uondokane naye.
 
Nina kaka kama huyu
Ukikaa nae siku moja tu lazima akulize.
Kazi yake ni kuzunguka kwa ndugu na kuwaibia
Jitihada zote zimeshindikana na kila mmoja wetu ka give up.
Yeye ni wanawake,pombe nk
I know what you are going through bro.
Pole sana
OTIS
 
Watu kama hao vigumu kuchange, sasa kwa kuwa ni kaka yako mtafutie mwanamke mzuri afu muozeshe, kuna wanawake wana waongoza wanaume wana kwenda sawa :violin:
 
huyo ndugu yako noma sana.yaani yeye badala ya kubeba mizigo akawa anajaza lori zima vimwana?!! teh teh..

fukuzia mbali mi ilishawahi kunitokea kwa kaka yangu mtoto wa mama mkubwa.....sikuwa msamaha wala nini maana nilimbeba sana na kumsaida sana...nilipoona habebeki wala hashauriki NILIMFUKUZA....KWENDA ZAKE...mshenzi sana yule...yaani niliondoka mwezi tu baada ya kurudi nikakuta katoa picha zangu zote ukutani na ameweka zake. na rafiki zake hasa mademu anawaambia hapo ni kwake ..nilifika usiku kama saa 4 hivi nikakuta sebuleni watu kama 6..wasichana 3 na wavulana3 wanakunywa pombe.....nilichofanya nilimuita kistarabu chumbani kwangu nikamuuliza ''hapa ni baa?'' akajiuma uma maneno pale..nikamwambia nisiwaone hawa watu..wakajizoa na kuondoka...kesho yake nikakaa nae ...akawa kama amenielewa..baada ya siku mbili akarudia ushenzi wake..kwa kweli sikuwa na msamaha tena...nilimtimulia mbali sana....uvumilivu una kikomo...
 
Kwetu kuna usemi mmoja. "Hata kama nduguyo ni chizi kiasi gani, iko siku atakushindisha kutwa nzima ukimhangaikia"
 
si umuachie nyumba na usafir we usepe katafute vngne kwn naona umeshndwa kumtafutia nyumba ajitegemee we mlipie kodi tu wakati umeweza kufanya yote hayo.
 
Nina kaka kama huyu
Ukikaa nae siku moja tu lazima akulize.
Kazi yake ni kuzunguka kwa ndugu na kuwaibia
Jitihada zote zimeshindikana na kila mmoja wetu ka give up.
Yeye ni wanawake,pombe nk
I know what you are going through bro.
Pole sana
OTIS

halafu wachonganishi kinoma....
 
samahani, ni kwamba sijakuelewa au? ina maana analeta wanawake zake nyumbani kwako? kabisa nyumbani kwako? wewe unakuwa wapi? au unaruhusu? hauna sheria na kanuni za nyumba yako?

wema usizidi mzigo mkuu, huyo ni mtu mzima, mwambie akupishe aende mtaani akajifunze, tatizo anapata pa kula, kulala na ku**a ndo maana hawazi kesho yake itakuwaje........ mwambie ashike ustaarabu wake dunia ikimfunza atakaa chini atafakari mustakabali wa maisha yake...... najua una nia njema ya kumsaidia, lakini umsaidie mtu anayehitaji msaada, unaweza kumtafutia kazi akaishia kuharibu reputation yako...mwache arudi kwenye maisha aliyoyazoea...mwache arudi kwenye udalali

 
nadhani kwenye familia nyingi kuna mmoja lazima atakuwa pasua kichwa, sijui kwa nini...........



Nina kaka kama huyu
Ukikaa nae siku moja tu lazima akulize.
Kazi yake ni kuzunguka kwa ndugu na kuwaibia
Jitihada zote zimeshindikana na kila mmoja wetu ka give up.
Yeye ni wanawake,pombe nk
I know what you are going through bro.
Pole sana
OTIS
 
kwa kuwa familia yako inafahamu kuwa jamaa ni mtata,haambiliki na haeleweki,chochote utakacho kifanya wala hakita kufunga na isitoshe wewe ni wa 3 kuzaliwa ikimaanisha wapo wa 2 juu yako,kwa maana hiyo basi huna haja ya kumung'unya maneno na swala la wewe kuongea na ndugu zako kwani wanaelewa nini kinaendelea na mwisho wa siku unamtimuwa bro huku familia yako ikielewa.

nakupa mfano mdogo tu ambao ni wa kweli

nina jamaa yangu nimesoma nae SUA,amejenga nyumba yake dodoma baada ya kumaliza kuijenga ikabidi amwite mdogo wake ili aweze kukaa nae,baada ya mwezi mmoja rafiki yangu huyo Z alitakiwa kwenda japan kupata mafunzo ya miezi 6 na alimwanchia mdogo wake nyumba na usafiri.
baada ya kumaliza miezi 6 Japan alirejea Dodoma cha kushangaza alikuta mdogo wake kauza nyumba na kuhamia morogoro,baada ya kuulizwa kwanini ameuza nyumba akadai kuwa ile nyumba ilikuwa ya familia na kwa kuwa yeye alipata nafasi ya kuwa Japani ilibidi aiuze ili apate mtaji wa kuanzia biashara

uzuri ni kwamba usafiri hauuza,alicho kifanya rafiki yangu Z ni kuchukua usafiri tena hadi mahakami na kusamehe pesa za nyumba iliyo uzwa

kwa upande wako

chochote cha weza tokea na kama huamini mpe mwaka mmoja bro wako kwani tayari amesha anza kuwaeleza hata shemeji zako kuwa usafiri na nyumba ni vyake.ukimpa chance ya kuwa pekeyake ktk nyumba hiyo utarudi hapa JF na kusema kulichotokea,kwani hawa ndugu zetu hawajui ugumu wa kutafuta na hata kuuza kitu kwa bei raisi si shida kwao

take care
 
huyo kaka yako ni sawa na kubeba gunia la mavi, lisipokushinda kwa harufu litakushinda kwa uzito,
 
Hata hivyo ujmejitahidi sana ( ukute lenyewe linaroho mbaya sana lisingeweza kubeba mtu), lkn usikate tamaa... Miaka 38 kwa watu wengine kweli wanakuwa hawajapevuka sawasawa....wahumu mno kuanza kujitambua, na pia kwa tabia zetu za kiafrika kaka yako anaweza asikusikilize kwa lolote lile akajua unamdharau tu na mambo kama hayo..., sasa basi, mtafutie mtu mzima kidogo, sio lazima awe ndugu yako..anaweza kuwa jirani,au kiongozi wa kidini mnayoamini, mueleze unavyompenda kakayo na unavyojisikia vibaya kwa tabia zake za kijinga! Ninaamini anaweza kurekebika....... Mwisho kabisa...akiendelea kukusumbua mfukuze tu nyumbani, tena kuwa siriasi!...mwache akapate taabu maana wakati mwingine taabu za dunia zinafundisha kuliko wazazi,ndugu,jamaa,nk.
 
Huyu ni kaka yangu kabisa, mama mmoja baba mmoja. Ana miaka 38 na kabla ya kuzaliwa mimi, walizaliwa kaka na dada zangu wengine 2, hivyo mimi ni mdogo wake wa 3, na hapo unaweza kujua tumepishana umri kiasi gani!

Haileweki. Alimaliza form akafeli. Wazazi walimlazimisha shule akakataa kata kata. Akawa anashinda anazurura na kufanya kazi za udalali huku akiishi kwa sisi wadogo zake. Alikuwa anakaa kwa kaka zangu mwanzo, akawa na tabia za ulevi wa kupindukia na kuiba vitu vidgo vidogo na kusumbua shemeji zake. Tumemkalisha vikao na kumuonya kashindwa kubadili tabia.

Kila mtu alimchoka tukaamua kumuacha na kuanza kuishi maisha kama chokoraa! Nilimuonea huruma, nikamchukua akae nyumbani kwangu. Nilijaribu kumfungulia miradi ikafa kwa maana ni muhongaji mzuri wa wanawake! Nilimpa hela aenda driving, na kupata leseni ili nifanyie mpango kazini kwangu akala hela zote na leseni hakupata. Niliamua kumtafutia leseni kwa juhudi zangu na kumpeleka akawe dereva kwenye kampuni moja kubwa ya kusafirisha mizigo, akaishia kutumia magari kubebea vimwana. Akafukuzwa kazi

Sasa kaanza tabia ya udokozi wa vitu vya ndani na kuuza na kuleta wanawake huku akiwadanganya kuwa nyumba na usafiri wangu vyote ni vyake, ila kaamua kuniachia mdogo wake. Na sasa kuna msichana wake kanitumia meseji eti kwa nini nang'ang'ania nyumba na usafiri wa kaka badala ya kujitafutia maisha yangu mwenyewe! Thats is to say, hata wasichana wake wanaamini kuwa mimi ndo ninaishi kwa kaka! Wananisumbua, eti nawabana! - Sijui wana upeo mdogo kiasi gani!

Sasa mtu kama huyu hasaidiki, nitampeleka wapi? Nampiga chini leo leo. Namfukuzia mbali! Nimechoka!
Naomba ushauri!


HorsePower

Mungu hawezi kukupa jaribu usiloweza kulitatua!unataka akaibe mitaani then wamuue?bora anakuibia wewe lasivyo angekuwa kauliwa
 
Miaka 38 jamani bado hajakuwa?
JK Nyerere aliposema Kikwete bado hajakomaa akumaanisha umri bali akili zake, kwahiyo usishangae wewe kuona miaka 38 ni mingi bali akili yaweza kuzidiwa na kijana wa miaka 20.
Mimi Secondary School nilikuwa na mshikaji tunasoma naye na alikuwa anajilipia ada yeye mwenyewe kwenye Private School, wakati tunafika form four mshikaji akanunuwa gari yake Land Rover 109,.....u can imagine now huyu jamaa maisha yake yamesimama ile mbaya. kuna watu wanazaliwa Talented hili halina ubishi.
 
Back
Top Bottom