Bro ametuachia Janga kubwa sana, sababu tu ni Upendo wake kwetu

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Ametuachia toto Jinga sana. Tumelikuza limefika miaka 30 linataka oa. Tunaliuza umejipanga una Tsh ngapi. Linasema halina hata shillingi. Bwege kabisa fala, zumbukuku, topolo kabisa.

Tunaliambia sasa wewe unatakaje kuoa huna kitu. Nenda kajipange linalia kuwa angekuwepo baba yake angeliozesha. So linapata taabu sababu baba yake hayupo. Kilaza, kiazi, kimburukutu, zebwa kabisa.

Linashinda tu kula chips mayai na kujaza kitambi huku limefuga ndevu kama beberu. Halihangaiki kwa lolote. Na kumbe linapewa michango na wenzie linakula. Tunashukuru tu nyumba liliachiwa na baba yake.

Ukilishauri tu jambo ambalo ni la kukaza linaangua kilio kuwa kama angekuwepo baba.... Mimi nawaambia ndugu tuachaneni nalo wananambia watu wataona tunamwacha sababu bro amefariki.

Lilivyo jinga lina take hiyo advantage....bwege, bulldozer, fala, kichomi, kichefuchefu kabisa....

Sometime tunasema heri bro angebaki yeye.... aaaarrgh...tusameheane tu.
 
Hujatumia lugha nzuri kwa mtoto wa mwenzako, kuwa na staha kidogo mkuu, muonee huruma mwana wa mwenzio, by the way wewe umeandaa mazingira gani kwa watoto wako ikiwa Israel ataitaka roho yako?

Ulipaswa kumuelewesha tu huyo kijana na sio kumuhusishanisha na marehemu!!
 
Mie nimefiwa na wazazi wangu wote wawili ningali mdogo na sikuachiwa hata hatua mbili za kiwanja, na nilikuwa napiga kazi za kufa mtu pale hom,na bado naonekana mimi mbwa, nilipomaliza tu darasa la saba nikaingia mtaani rasmi kukimbizana na life, yani kuna watu wana bahati sana hapa duniani
 
Hujatumia lugha nzuri kwa mtoto wa mwenzako,kuwa na staha kidogo mkuu,muonee huruma mwana wa mwenzio,by the way wewe umeandaa mazingira gani kwa watoto wako ikiwa Israel ataitaka roho yako?

Ulipaswa kumuelewesha tu huyo kijana na sio kumuhusishanisha na marehemu!!
On point huyu ndugu mtoa post hadi hapa inaonekana tayari anachuki na makasiriko juu ya mtoto wa marehem kaka yake na bad usikute dogo mzee wake alimuachia mali nying na jamaa wamemtaifisha kwa kumhadaa kuwa ndio amekuziwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujatumia lugha nzuri kwa mtoto wa mwenzako,kuwa na staha kidogo mkuu,muonee huruma mwana wa mwenzio,by the way wewe umeandaa mazingira gani kwa watoto wako ikiwa Israel ataitaka roho yako?

Ulipaswa kumuelewesha tu huyo kijana na sio kumuhusishanisha na marehemu!!
Ulitaka nitumie kiingereza?
Israel ndo nani?
 
Back
Top Bottom