BRN katika elimu ni kazi bure iwapo mwalimu akizidi kukandamizwa na kupuuzwa na kulipwa mshahara dun

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
0
Serikali kwa sasa imeamua kufanya mapindinduzi makubwa katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.Nimependezewa na elimu nayo kuwekwa katika mpango wa matokeo makubwa sasa Big Results Now (BRN).Katika BRN serikali imedhamiria kuboresha elimu kuanzia ufundishaji,vifaa vya kufundishia.kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi,na vyumba vya madarasa.

Nikija katika kuhakikisha haya yote,serikali imeamua kuboresha ukaguzi katika shule zake zote, za sekondari na shule za msingi pamoja na vyuo vyake mbalimbali.Hapa ninapenda kuchukua fursa hii kuipongeza serikali kwa jitihada zake za kuinua elimu nchini.

Kuhusu maslahi ya elimu.Nimetiwa moyo na ahadi ya mheshimiwa rais wetu,ndugu Jakaya M.Kikwete ya kubadilisha miundo ya mishahara ya walimu.Iwapo ahadi hii ya mheshimiwa rais ikitekelezwa basi elimu yetu itazidi kupanda.Kwani jitihada za serikali kuboresha elimu Tanzania itakuwa sawa na kusubiri usafiri wa treni baharini iwapo masilahi ya walimu yakipuuzwa.Kwa muda mrefu walimu wa shule za msingi na sekondari wamevunjika moyo wa kufanya kazi baada ya kuishi maisha ya dhiki na tabu kutokana na masilahi duni wanayopata kama malipo ya kazi yao.Hali hii imepelekea walimu hawa kutumia muda mwingi kufanya kazi za ziada ili wajiongezee kipato huku mahudhurio yao darasani yakiwa hafifu.

Walimu hawa wamekuwa wakigombana na wakuu wao wa shule na maafisa elimu kwa utoro wao makazini.Baadhi yao wamekuwa viburi sana na kuwa tayari kwa kufanywa chochote na waajiri wao kwani bakora ya maisha imewapiga hivyo kuwa tayari kwa chochote.Hawajutii hata wakifukuzwa kazi,kwani ugumu wa maisha umewapelekea mpaka wawe na ujasiri wa wa kusema lolote na liwe.Hawana cha kupoteza.Hii yote inatokana na walimu hawa kuathirika kisaikolijia kutokana na maslahi duni.Kibaya zaidi walimu hawa wanashuhudia watumishi wa kada nyingine wanaishi maisha ya neema wakilipwa mishahara minono na marupurupu kibao,wakati watumishi hao wana sifa zinazofanana na walimu hao.Na wote wanafanya kazi kwa muajiri mmoja.

Walimu hawa wanajilinganisha na watumishi wa Benki kuu, mamlaka ya mapato (TRA),mifuko ya hifadhi ya jamii kama vile NSSF,PPF,PSPF nakadhalika wanaolipwa vizuri kuliko walimu hawa.Je watapata wapi moyo wa kufanya kazi ?

Hata hivyo walimu hawa wamebakiza tumaini lao kwa mheshimiwa rais wetu kwa kudhamiria kuboresha maslahi ya walimu kwa kuanzia kubadili miundo ya kitumimishi ya walimu.HONGERA SANA M.RAIS KWA NIA YAKO YA KULETA MAPINDUZI YA ELIMU KWA KUAHIDI KUBADILI MIUNDO YA MISHAHARA YA WALIMU.

Napenda kutoa angalizo kwa serikali kuweka utaratibu wa kukutanisha maafisa elimu wote wa wilaya na mikoa na wadau wote wa elimu pamoja na walimu ngazi za wilaya na mkoa walau mara mbili kwa mwaka ili kupata fursa ya kujadili mustakabali wa elimu yetu na changamoto mbalimbali za elimu.Vile vile walimu wakuu waache kasumba ya kuwadharau walimu na kuwaona kama vidudu mtu.Dharau hii ya wakuu wa shule kwa walimu imekithiri sana katika shule mablimbali za sekondari nchini.
 

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,536
2,000
What you are talking is absolutely true, mind you even those officials know the root of educational problems though they pretend to be deafs as well as blinds while at the same time they are physically and mentally fine. Once they will be ready to solve problems facing teachers and education in particular is where mass examination failure will diminish.
 

riro23

JF-Expert Member
Sep 16, 2013
670
1,000
nasikia madaraja ya mishahara ya walimu wanabadilishwa kuanzia july, mwenye taarifa atujtuze
 

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
0
Hii itakuwa habari njema kwa walimu.Viwango hivi vipya vitakuwa na maana iwapo serikali ikipunguza kodi kwa walimu na kudhibiti mfumuko wa bei.
 

service

JF-Expert Member
May 22, 2014
2,940
2,000
TGTS A1 346,000
TGTS B1 394.000
TGTS C1 582,500
TGTS D1 639,000
TGTS E1 819,000
TGTS F1 1,053,000
TGTS G1 1,370,000
TGTS H1 1,784,000
TGTS I1 2,465,000, Hii ndio mishahara mipya iliyotokana na mjadala wa miaka karibu 5 kat ya CWT NA SERIKALI Inaanza kutumika Julai,2014. By MWL OLUOCH - KKM-CWT.Siku njema mwl mwenzangu.

mkuu kodi inamaliza mshahara wote!!!!!
 

riro23

JF-Expert Member
Sep 16, 2013
670
1,000
TGTS A1 346,000
TGTS B1 394.000
TGTS C1 582,500
TGTS D1 639,000
TGTS E1 819,000
TGTS F1 1,053,000
TGTS G1 1,370,000
TGTS H1 1,784,000
TGTS I1 2,465,000, Hii ndio mishahara mipya iliyotokana na mjadala wa miaka karibu 5 kat ya CWT NA SERIKALI Inaanza kutumika Julai,2014. By MWL OLUOCH - KKM-CWT.Siku njema mwl mwenzangu.

Kwahyo wale wa shahada itakuwa ngapi apo baada ya madaraja kubadlshwa?
 

mikagati

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
320
195
639000-589000=50000,Kwel bado kuna kasafari karefu. Upandaji madaraja kwenyewe hadi mtu uende kuwafuatilia kweli kweli, mana majibu wanayoyatoa hao TSD kwa kweli kinyaa.
 

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,536
2,000
What you are talking is absolutely true, mind you even those officials know the root of educational problems though they pretend to be deafs as well as blinds while at the same time they are physically and mentally fine. Once they will be ready to solve problems facing teachers and education in particular is where mass examination failure will diminish.
hypothetical outcomes with fake expectations. hao walimu wasiofundisha hata wakiongezewa hela kama hawajasimamiwa hawatafundisha. alafu kwani mtu unapoajiliwa kwa kuomba mwenyewe huku akijua mshahara mdogo kweli ana akili?
 

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,536
2,000
mkuu kodi inamaliza mshahara wote!!!!!
muwe mnatumia na akili basi, unafikiri huo mshahara unatokana na nini kama siyo kodi za watanzania? ama unataka hata kodi usilipe? ili akulipie nani? government budget runs at deficit alafu watu wanaona wakiambiwa walipe kodi wanaona wanaonewa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom