British open school idadi ya mabango kwenye magari na barabarani inatosha jaribuni kujiamini

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,230
29,608
Kama wewe ni mkazi au umewahi kufika jiji la dar es salaam basi neno British school si geni kwako kama hutembei basi kwenye TV utaona, kama huna TV basi barabarani utaona mibango Yao tena mikubwa utadhani inalipiwa kodi, kama hutazami kilichopo barabarani basi kwenye vituo vya stend ya daladala hadi kero kwenye magari ndousiseme mpaka matairi yanayokaaga nyuma yaani reserve tyres.
Nimejaribu kupiga mahesabu idadi ya matangazo wanayotoa kwa kasi tena bila mpangilio ni gharama kuliko gharama za uendeshaji wa shule yaani kwanzia usafi wa Choo mpaka mishahara.
Hakuna pingamizi kabisa, zaidi ya million Mia moja na upuuzi kwa mwaka zinateketea kwenye mabango. Sasa chaajabu zaidi shule yenyewe imejengwa kwa ukuta wa mbao na mabati kama tuition center za mgote.
Mimi ningewashauri yafuatayo sio tu kama mtazamaji Bali ualimu ni taaluma niliyonayo.
1: Mabango waachane nayo ni gharama. Watengeneze page zao kwenye mitandao ya kijamii
2: Wajaribu kucopy na kupest kwa Brothers academy ujanja anaotumia kupata idadi kubwa ya wanafunzi zaidi ya miatatu kila mwaka ilihali hana bango hata moja zaidi ya lile la ukonga nalo kwaajili yakuelekeza njia tu
3:Wapeleke matangazo Yao kwenye online media hata television pia particularly
millardiayo na ITV
4: Wafanye jitihada haraka iwezekanavyo pale mwenge wahame mazingira sirafiki kwa wanafunzi, wamebanwa waende kiluvya au kongowe nipazuri Sana
5:Lamwisho kabisa wabadili JINA LA shule. Neno British baadhi ya wazazi wanajua ni shule ya international yaani za wazungu kutoka London kumbe sio kweli ni shule ya makapuku tu watoto wanaosoma pale ni wamamantilie baba zao wanauza madafu na dawa za kunguni ambapo mmiliki wa shule ni dula anakaa tandale kwa tumbo
Zingatieni hayo Sina shida ya Asante yenu saizi naenda kazini
 
Ona mabango Yao
FB_IMG_16319987055717035.jpg
 
Watanzania tuachage mambo ya kizamani binafsi naomba nikuulize mleta mada uniambie kero unayoipata kutokana na hayo mabango unaweza kuta wamiliki wa hyo british ni vijana wasiokua na ajira ndio wanajiongeza we unaleta story zako za kingese jaribu kuwa Mzalendo lingekuwa bango la Mchina ungetulia kimyaa acha Wivu dada
 
Mbona enzi zetu za Mchikichini hakukuwa na mabango na wanafunzi tulikuwa wengi sana.
matangazo ya nguvu za kiume yameathiri saikolojia za wafanyabiashara wengi.

imefikia hatua wanaamini katika marketing kuliko hata ubora.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom