Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,606
- 1,956
Brigedia Jenerali Mbuge ameyasema hayo Februari 13, 2020 mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT mkoani Simiyu.
Ameongeza kuwa katika kukabiliana na changamoto hiyo, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limejipanga kuanzisha maduka ya vifaa vya Ujenzi vitakavyouzwa kwa bei ya jumla ili kuwezesha upatikanaji wa vifaa kwa urahisi, haraka na kwa bei nafuu ikilinganishwa na wazabuni wengine.
“Tatizo moja ninaloliona kwenye utekelezaji wa miradi ni vifaa kuuzwa kwa bei ya juu sana na kucheleweshwa, tumeamua kuwa na maduka ya vifaa ya jumla; tutatoa maelekezo kwa wakuu wa kanda za ujenzi watatupatia mahitaji yao, ili kuwawezesha kufanya kazi kwa wakati kama tunavyokubaliana na washitiri wetu,” alisema Brigedia Jenerali Mbuge.