Brigedia General SINDA (Dr Sinda) afariki dinia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Brigedia General SINDA (Dr Sinda) afariki dinia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Barubaru, Jul 18, 2011.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi.

  Napenda kuwapa taarifa kuwa ndugu yetu Brigadia General DR Ali Abdallah Sinda ambaye alikuwa mkuu wa Hospital ya Jeshi ya Lugalo huko Tanzania amefariki dunia jana huko kwake salasala Darisalaam.

  Daktari huyu ndio alikuwa amepata kuongezwa cheo kutoka Colonel kuwa Brigadia generai na kuwa Chief millitary medical officer. Na kwa sisi wanasheria tumesoma na mkewe SUBIRA HARUNA NDAE ( MRS SUBIRA SINDA) Ambaye ni Chief legal officer wizara ya Ardhi huko Darisalaam.

  Hakika Dada Subira Sinda ni mwenzetu tukiwa university kama dada yetu miaka miwili mbele na vile vile mwanasheria mahiri ndani ya Serikali ya Tanzania akiwa wizara ya Ardhi. Napenda kumpa pole sana kwa kufiwa na mumewe.

  Mimi binafsi na mume wangu wiki tatu zilizopita tulikuwa Darisalaam na tulikutana na huyu dada Sibira Sinda na tulizungumza sana na alitupa habari hizo njema za Mumewe.

  Hakika Mwenzetu ametangulia nasisi tupo nyuma yake, Jina la Mola lihimidiwe.

  Masikini Dada Subira amekuwa kizuka.

  Kwa niaba yangu binafsi na familia yangu na wanazuoni wote tuliosoma nawe Dada Subira hususan kitengo cha Sheria tunakupa Pole sana na Mola akupe ujasiri na subra kama jina lako kwa imani kuwa yeye ametangulia nasi tupo nyuma yake.

  Ni mimi
  Nasriyah Saleh Al Nahdi.
  Director Legal affairs and communications
  Qatar Petrolium.
  Doha
   
Loading...